MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mt Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivuka moja ya sehemu ambazo zina maji katika bonde la mto Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha Dar es Salaam na kuleta madhara kwa wakazi hao
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza katika maeneo ya bonde la Mto Msimbazi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuza maembe.




Na Ripota wa globu ya jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Makonda amesema ahayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa kaitembelea maeneo hayo.

"la kwanza katika ngazi ya mkoa kulingana na utabiri wa hali mvua zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50 maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili usema kinga ni bora kuliko tiba "Aamesema Makonda

amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia hili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi hili kupunguza Madhara.

amesema hayo yanayo onekana leo ni tabia mabaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunavyoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi la pili tunaambiwa tuhakikishe kuwa atuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga

ametaja kuwa maji hayo mengi utokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa pwani hasa katika eneo la kisarawe na kuhitaji kupita katika mto huu hivyo ukijengwa ndipo madhara haya ayataonekana.

Post a Comment

Previous Post Next Post