VINGUNGUTI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

 Naibu Meya wa Manispaa  ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa mtaa miembeni katika kikao cha kamati ya shule.
 Baadhi ya Wananchi na Wazazi wakiwa wamekaa kwa makini wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala
 Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembeni,Idaya Ndevumbili akizungumza na wazazi wa shiule hiyo
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya rangikwa kamati ya shule ya msingi miembeni


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu.

Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule msingi miembeni kata ya Vingunguti .

“lazima niwambie ukweli hili swala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka hili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto.

Kumbilamoto ametolea uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu amabapo alikuwa mapumzikoni hivi karibuni hivyo anasema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni.

Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza .

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo huo

Post a Comment

Previous Post Next Post