CHUO CHA SHENYANG CHA CHINA YATOA UFADHILI KWA AIR TANZANIA NA NIT

 Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akimkabidhi hati ya ufadhili wa masomo  Mkurugenzi wa shirika la ndege nchini Air Tanzania,Ladislaus Matindi  kwa  ajili ya wafanyakazi wa shirika hilo watakotakiwa kwenda kusoma China




Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Chuo kikuu cha shenyang kutoka nchini China kimeahidi kutoa ushirikiano na Shirika la ndege la Aira Tanzania kwa kutoa msaada wa kuwasomesha wafanyakazi wa kampuni hiyohili waweze kumudu ushindani wa soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa malezi wa chuo cha Shenyang, Shi Guangda katika mkutano ulioandaliwa na Tasisi ya Global Education Link kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma urubani  na Masuala ya anga katika chuo hicho.

“tangu Rais wetu wa China alipofika hapa tumekuwa na mahusiano makubwa na na nchi hizi mbili hivyo kwa kuanza kama chuo chetu tutatoa ufadhili kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Air Tanzania na kubadilishana  mafunzo katika chuo cha uasafirishaji cha NIT na Shenyang” Amesema Guangda .

Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Tanzania,Ladislaus Matindi ameishukuru tasisi ya Global Education Link kwa kuweza kuwaunganisha na chuo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa msaada mkubwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa shirika hilo.

Matindi ametaja kuwa upatikanaji wa nafasi hiyo itasaidia kutoa motisha kwa vijana wetu ambao wanafanya kazi katika shirika hilo na wengine ambao wako nje kuwa na hamu ya kusoma masuala ya usafirishaji .

Kwa upande wake mkurugenzi wa Global Education link , AbduMalik Molell alitumia fursa hiyo kuzungumza na wazazi hao juu ya swala la bima ya wanafunzi amabo wanasoma chuo hicho katika swala zima la matibabu na majanga mengine ambayo yatawakuta wanafunzi



 Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Air Tanzania Ladislaus Matindi akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasoma masuala ya Anga nchini China
 Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akifafanua jambo kuhusu masuala ya bima ya matibabu kwa wazazi ambao wamefika katika mkutano huo
 Mlezi wa wanafunzi kutoka chuo Shenyang, akizungumza juu ya mazingira na ufadhili walio utoa nchini kwa shirika la ndege

 Afisa Biashara mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara upande wa Tantrade, Stephene Kobelo akizungumza na wazazi juu ya namna watoto wanavyotakiwa kuitangaza nchi
 Baadhi ya Wazazi ambao wamefika katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini juu ya swala zima la bima ya matibabu kwa wanafunzi
 Baadhi ya wakurugenzi wa wenza wa Tasisi ya Global Education Link wakisikiliza
 Mmoja wa wazazi akichangia jambo juu ya kuboresha bima ya wanafunzi wanaosoma China
Wazazi na baadhi ya ndugu ambao watoto wao wanasoma nchini China wakifatilia mkutano

Post a Comment

Previous Post Next Post