KIPINDI CHA 360 KURUSHWA MUBASHARA KUTOKA KATIKA HIFADHI ZA SERENGETI NA NGORONGORO

 Afisa uhusiano wa Tanapa Pascal Shelutete akizungumza na watangazaji wa kipindi cha 360 cha Clouds Tv ambao wamewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya kipindi katika mbuga za Ngorongoro na Serengeti
 Watangazaji wa kipindi cha 360 cha Clouds Tv wakijadili jambo kabla ya kupanda kwenye magari kwa ajili ya kuelekea mbugani
 Watangazaji wa kipindi cha Clouds 360 wakiongozwa na Sam Sasari wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Arusha


Watangazaji wa kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Tv wamewasili mikoani Arusha jioni hii kwa ajili ya ziara katika hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.

Kipindi kilichoendelea kujizolea umaarufu cha 360 kinataraji kurushwa moja kwa moja kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Serengeti kikiongozwa na watangazaji wake Baby Kabaye, Sam Sasali, Hassan Ngoma na James Tupa tupa.


Couple ya washindi ambao wamewasili kwa ajili ya safari katika mbuga hizo za Wanyamapamoja na timu nzima ya 360

Post a Comment

Previous Post Next Post