Saturday, May 20, 2017

DOGO JANJA ; MUZIKI WANGU NI LEVEL ZA KINA JAYZ

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amejitamba na kusema ingawa yeye ni mdogo lakini muziki anaofanya ni mkubwa kiasi kwamba watu wanaoweza kuufanya ni level za Jay Z.
Dogo Janja
Msanii huyo akipiga stori na Magic Fm amesema kwanza yeye si mtu wa kushirikishwa au kushirisha wasanii hovyo hovyo katika nyimbo zake, bali yeye anadeal na zile serious project tu.
“Mtoto anafanya muziki wa mtu mzima, muziki ninaofanya mimi angetakiwa afanye mtu kama Jay Z lakini ndio nafanya mimi, ni hatari sana,” amesema na kuongeza.
“Mimi kwanza sifanyi kolabo, kama nitafanya ni zile zipo serious, sio zile kuna kaverse kapo hapa njo ufanye, kama unafiti ibuka. Mimi nafanya project kama ya Chindo ametoka Marekani straight L. A (Los Angeles), mimi nikatoka straight froma Dar es Salaam tukakutana Arusha tukashoot video Kijenge, madirector wanne kutoka nje, tumemaliza mimi nikasepa kuendelea na mitikasi mwana akala flight to L.A,” amemaliza kwa kusema.

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...