Wednesday, May 17, 2017

MARIA SHARAPOVA AEUNGULIWA FRENCH OPEN


Mchezaji nyota wa Mchezo wa Tenisi wa nchini Urusi, Maria Sharapova, amenyimwa kadi maalumu ya kuingia kwenye mashindano ya wazi ya Ufaransa maarufu kama ‘French Open’ yanayotarajiwa kuanza katikati ya Mwezi huu.
Mkuu wa shirikisho wa mchezo wa Tensis nchini Ufaransa, Bernard Giudicelli Ferrandini, alikanusha zaidi ya mara mbili kuwa mchezaji huyo hatoweza kushiriki mashindano hayo na kusema
“Mwaliko huo ungeliweza kutolewa kwa mchezaji ambaye ametoka kuwa majeruhi lakini sio kwa aliyefungiwa kwa kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli”
“Samahani sana Maria, samahani na kwa mashabiki zake”.
“Pengine nitakuwa nimewaangusha, pengine pia nitakuwa nimemkwaza , lakini ni jukumu langu, wajibu wangu,kuhakikisha ninalinda viwango vya wachezaji katika michezo pasipo shaka yoyote kwamba pengine ametumia madawa ama la kutokana na matokeo.”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, na mshindi mara tano wa Grand Slam , aligundulika kutumua madawa yaliyopigwa marufuku michezoni mwaka 2016 katika mashindano ya wazi ya Australia.

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...