TAFITI ;SERIKALI INAPOTEZA MABILIONI KUTOKANA RUSHWA NA UFISADI KWENYE BAJETI

 Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji  wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakizindua Ripoti hiyo, wakiwa na Wabunge
 Kamati ya Viongozi wa dini ya Masuala ya haki za Binadamu ,Kiuchumi na uadilifu katika Uumbaji  wakizindua Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani? wakiwa na wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakionyesha Vitabu juu mara baada ya uzinduzi
 Profesa ,Honest Ngowi akifafanua juu ya Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
 Askofu Stephene Munga akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mapitio ya Ripoti ya Swali la Dola Bilioni moja ,Tanzania inaendelea kupoteza fedha kiasi gani?
 Mbunge    wa Msalala , Ezekiel Maige akizungumza wakati wa kuchangia  mapitio ya ripoti hiyo  
 Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrad Kigola akichangia mada
 Sehemu ya washiriki wa mkutano huo

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

Tafiti mpya iliyozinduliwa leo inasema serikali inapoteza fedha zaidi ya Sh trillion 4 kwa mwaka kutokana na misamaha na ukwepaji wa kodi.
 Pia repoti inasema serikali inasema serikali inapoteza  Dola za kimarekani 1.3 biloni (2.9 trilion) kutokana na rushwa na ufisadi katika bajeti ya Taifa.

Hayo yamesemwa na Profesa  Honest Ngowi alipokuwa akiwasilisha matokeo ya utafiti na mapitio ya ripoti ya swali la dola bilioni moja na kuja na swali Tanzania inapoteza kiasi gani cha fedha?.

Profesa Ngowi katika mapitio hayo amepata kutaja kuwa , Mfumo wa ulipaji kodi , Mlipa kodi,Misamaha ya kodi ,Utroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato,Ukwepaji kodi, Madhara na Gharama za upotevu na kutokusanywa kodi ipasavyo ni moja ya mambo yanayochangia kupotea kwa fedha hii.

“Tatizo la utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upotevu wa mapato limeangaliwa upya katika utafiti huu na kubaini kuwa Tanzania bado inapoteza mapato kwa njia ya utoroshaji fedha zilizopatikana kwa njia zisizo halali ,Zinaondoshwa nchini visivyo na kutumiwa isivyo halali” amesema Prof Ngowi.

Ametaja kuwa fedha hizo zinaweza kuwa ni fedha zitokanazo na biashara haramu kama biashara ya kulevya , biashara haramu mipakani ,uharamia ,usafirishaji binadamu ,mapato kutokana na ukwepaji kodi na mapato yatokanayo na rushwa.
Amesema kuwa sambamba na utoroshwaji wa fedha ,tatizo la kutoa taharifa za uongo wa bei 

Post a Comment

Previous Post Next Post