TIB WAANZA KAZI SAA 24 BANDARINI KWA MUDA WA SAA 24

 Mkurugenzi wa  Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kufanya kazi saa 24 Bandari ya Dar es Salaam 
 Mkurugenzi  mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege  , Theresia Soka  akizungumzia ubora wa huduma hizo
  watendaji wa   Benki ya Biashara ya TIB  

Sehemu ya Waandishi wa Habari walifika katika  mkutano huo

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
Katika kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli benki ya biashara ya TIB imeanzisha huduma za kibenki kwa masaa 24 katika tawi dogo la benki hiyo lililopo katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa  Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege amesema huduma hiyo inawawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbali mbali pamoja na tozo zote za bandari.
 Amesema hivi karibuni TIB benki na TRA ziliingia mkataba kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ambapo mtu akilipa kodi kupitia mfumo huo katika tawi lolote la benki hiyo, taarifa zake zitaonekana moja kwa moja kwenye mtandao wa TRA.
Amesema kuwa, benki hiyo ya biashara (TIB), ndiyo benki pekee yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za TPA hivyo mwananchi atakapolipia tozo yoyote bandarini taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wake hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine za utoaji mizigo kwa haraka zaidi.
“TIB bank inatoa huduma mbali mbali kutokana na mahitaji ya mteja, zikiwemo za akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya muda mfupi na muda wa kati dhamana za kibenki uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni na shughuli zote za kibenki”, amesema Nyabundege.


Aidha amesema, benki hiyo ya kibiashara yenye matawi 6 nchini,  Dar esSalaam matatu, Mwanza, Arusha na Mbeya inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na pia inatoa huduma kwa watu binafsi taasisi binafsi na serikali.

Post a Comment

Previous Post Next Post