Thursday, May 25, 2017

UVCCM WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA HATUA ALIZOCHUKUA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Kaimu Katibu mkuu wa Umoja waa  Vijana wa Chama caMapinduzi(UVCMM), Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  na uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye masalhi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

 Shaka amesema hayo leo mapema jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa tamko la UVCCM kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli katika kupambana ma utoroshwaji wa rasilimali za nchi kwa uzembe wa watanzania wachache.

Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi 

“Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma.tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja 

      Amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM unaiomba kwa dhati Serikali yetu ianze kuipitia upya mikataba yote ya madini ili kubaini kama ni yenye manufaa na maslahi mapana  kwa umma na kumuomba Rais Dk John Magufuli kuwaweka pembeni wasaidizi wake wote ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi huku baadhi yao wakiona muhali kupambana na ufisadi. 

       Ameweka wazi kuwa UVCCM Inasisitiza kuwa Watendaji wote waliokuwa na dhamana na ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine kupoteza mapato na kulitia hasara Taifa, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao haraka . 

Amesema wao wanaishauri Serikali kuendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua Viongozi na watendaji wa serikali ambao watabainika kumiliki mali, utajiri na vitega uchumi ambavyo havitokani na mapato yasiolingana na vipato vyao wataifishwe kama ilivyofanyika mwaka 1967 baada ya kutangazwa Azimio la Arusha .


“Vijana wote tunaishauri serikali yetu isikubali na isiafiki  mali za umma zitumike kwa maslahi binafsi badala yake kila miliki ya serikali na mali ya umma ifahamike  kuwa kila mwananchi ana haki kufaidika nayo ambayo ni sehemu ya matunda ya Uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar”.

Alimaliza kwa kusema kuwa  Umoja wa Vijana wa CCM unawataka wana CCM na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Serikali yake katika mapambano dhidi ya vikundi vya rushwa, ufisadi na uzembe kwa baadhi ya watendaji  ili kuleta maendeleo endelevu katika taifa letu.  
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa maamuzi aliyochukua.
 Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwa na Viongozi wa ngazi za juu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akicheza muziki na baadhi ya wanachama wa UVCCM
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwa amebebwa juu  na Vijana wa CCM
Sehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili  katika ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
 smsehemu ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  wakiwa na furaha kubwa sana
 ehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
 Mabango ya kumpongeza Rais Magufuli


No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...