Friday, June 9, 2017

CTI Bajeti imekidhi mahitaji muhimu yapongeza bajeti ya 2017/2018

 Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini(CTI),Dk Samuel Nyantahe akizungumza na waandishi wa haabri juu ya Mtazamo wa Bajeti  kutoka tasis
  Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini(CTI),Dk Samuel Nyantahe akiwa na mjumbe wa tasisi hiyo Leodgar Tenga wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari(Picha zote Humphrey Shao)
Sehemu ya Wjumbe wa Shirikisho la Viwanda nchini CTI wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ,(Picha zote  na Humphrey Shao)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI) limesema bajeti ya mwaka huu ni nzuri na imekidhi mahitaji yote muhimu ikiwa ni pamoja  changamoto za wafanyabiashara kupata majibu.
Akizungumza leo  na waandishi e wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CTI, Dk. Samuel Nyantahe amesema bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango ni bajeti ambayo imegusa changamoto za wafanyabiashara walizokuwa wanazilalamikia.
Amesema  awali wafanyabiashara walikuwa wanalalamika kuwapo kwa kodi zisizokuwa na maana hivyo kwa sasa kumekuwapo na unafuu.
“Lakini Serikali kuongeza kodi katika bidhaa zinazozalishwa hapa nchini sambamba na zile zitokazo nje kidogo haijakaa sawa, walipaswa kuweka kipaumbele bidhaa za ndani kama vile ambavyo hawajaongeza kodi katika maji ya hapa nchini,” alisema Dk. Nyantahe.
Dk. Nyantahe amesema changamoto iliyopo sasa ni Serikali kuongeza uwigo wa ukusanyaji wa kodi katika kufanya bajeti hiyo iweze kutekelezeka kwa kuongezeka kwa kodi ya majengo.

Aidha amesema hatua ya serikali kuondoa kodi ya leseni katika magari na kuongeza katika mafuta ni jambo jema lakini kuna badhi ya watanzania watakuwa wanakatwa pindi watakapokuwa wanakwenda kununua mafuta wakati hawana magari.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...