Saturday, June 17, 2017

DC MJEMA AWAONYA WALE WANAOSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI MBONDOLE

Mkuu wa  Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Habari na kuwatahadharisha wale wote ambao wamekua wakichochea migogoro ya Ardhi katika Mtaa wa Mbondole kwa Muhaya eneo kata ya Msongola jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya amesema atawachukulia hatua za kisheria wale wote wanaotoa taharifa za uongo kuwa hukumu ya kubomolewa eneo hilo limetoka hivyo watu hao wanatakiwa waondoke wakati hukumu hiyo inataraji kutoka tarehe 28 June 2017.

 aidha ametoa wito kwa wakazi wa Mbondole kuwa wapole na kuacha kufata maneno ya Matapeli ambao wamekuwa wakiwadanganya kuwa eneo hilo hukumu imetoka na kutaja kuwa mtu anayewatisha wanatakiwa wamwambie awaonyeshe hukumu iliyo tayari hivyo kama ana hukumu wamlete ofisini kwake hili  taratibu za kisheria zifuatwe.


Sehemu ya mji Mbondole  kwa Muhaya ambayo mtu mmoja amejitokeza na kusema eneo hilo lake na kuwadanganya kuwa hukumu ya mahakama imetoka hivyo wanatakiwa waondoke
Wananchi wa Mbondole wakiwa wameshika mabango na kuandamana kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka

Wakazi wa Mbondole wakiwa wameshika bango kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka  mahakamni hivyo waondoke eneo hilo
Sehemu ya Wananchi wa Mbondole ambao walikusanyika na kuandamana kupinga kubomolewa nyumba zao mara baada ya kutolewa taharifa ya uongo kuwa  hukumu ya kubomolewa imetoka  mahakamani  hili waondoke katika eneo hilo

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...