Tuesday, June 20, 2017

EFM RADIO KUSAKATA KABUMBU NA WASANII WA BONGO FLEVA KANDA YA ZIWA


 

Na Ripota wa Globu ya Jamii
Zaidi ya wasanii kumi na mbili wa timu ya bongo fleva kusakata kabumbu na wadau wao wakubwa wa redio E-fm siku ya Jumamosi tarehe 25/06/2017 katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza katika mwendelezo wa kutambulisha masafa mapya ya  EFM Radio  ya 91.3 fm Mwanza.
  
Kwa mujibu wa taharifa iliyotlewa na afisa uhisiano wa kituo hicho, Jesca Mwanyika amesema kuwa  wakali hao wa bongo fleva na Efm redio watashiriki katika mtanange huo ili kuipa jamii hamasa  katika kujikita kwenye michezo mbalimbali ili kuimarisha afya zao na kuepuka hatari ya kupata magojwa yasioambukizwa.

“ mechi hii ni sehemu ya utaratibu wa E-fm ya kuwafikia wadau wao kama ilivyoada yao, vilevile kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kuwekeza katika michezo ili kuhamasisha na kuvumbua vipaji vipya katika jamii” amesema Mwanyika .

Mechi hiyo itaenda sambamba na mazoezi ya mbio za mwendo pole (jogging) zikiongozwa na Efm jogging club, Kubandika stika vyombo vya moto, na kuweka kifaa cha kuongeza masafa  katika redio za daladala kwa madereva hamsini wa kwanza kufika uwanjani.

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...