Saturday, June 17, 2017

HAKI ZA WATOTO INATAKIWA KUTEKELEZWA KATIKA KUJENGA TAIFA LENYE FURAHANa Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika amesema jamii inatakiwa kutekeleza haki za watoto katika kujenga taifa lenye furaha.

Lalika ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika  iliyoadhimimisha katika viwanja vya shule ya Msingi Mwanambaya wilayani Mkuranga mkoani Pwani, amesema kuna changamoto ya mimba katika wilaya na kufanya watoto wa kike wakose haki ya kupata elimu.

Amesema suala la mimba halitaweza kuvumilika kutokana na  kukosesha watoto wa kike kukosa elimu huku wazazi kushiriki vitendo hivyo kulipwa fedha na wale waliowapa ujauzito.

Dk. Lalika Amesema watoto wenye mahitaji maalumu wanatakiwa kuwa na miundombinu ya elimu rafiki kwani watoto wote ni sawa.
 Amesema watoto wanatakiwa kupewa ulinzi, pamoja na kupewa fursa sawa kwa mtoto wa kiume na kike na kuachana tamaduni za kutoa fursa ya elimu kwa mtoto wa kiume.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mtoto wa Afrika ni Maendeleo Endelevu 2030 Imarisha Ulinzi na Fursa sawa kwa Watoto.
Kesi zote zinazohusiana na masuala ya mimba zisikilizwe katika mahakama za mwanzo kama kutokana na muongozo wa serikali kwa vyombo vinavyohusika kupeleka kesi hizo zianaze kusikilizwa kuanzia Juni 1.

Mtoto anatakiwa kufanya kazi zinazoendana na umri wake na sio za kumfanya mtoto atwete kutokana na kuwa Tanzania imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya umoja wa mataifa.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, MhandisiMshamu Munde amesema  wazazi wametakiwa kuwa karibu na watoto kwa kila hatua kuwachia walimu  pekee yao hatuwezi kufika katika mtoto kuwa na elimu bora.

Munde amesema kuwa kwa michezo walionyesha ikiwemo Bunge la Watoto ni ishara kuwa walichosema ni kufanyia kazi.

Nae Afisa Maendeleo y Jamii Wilaya ya Mkuranga, Peter Nambuinga amesema wamepokea kesi kati ya kesi hizo zilisuluhishwa  na kesi 32 zilifikishwa mahakamani  na kupatiwa ufumbuzi.

Nambuinga amesema kesi za ubakaji na Ulawiti katika mwaka jana zilikuwa 12 ambazo zilishuhughulikiwa kwa wathumiwa kufikishwa mahakamani.

Mkuu wa Kitengo cha Dawati la jinsia na Watoto , Kulwa Kilongola Polisi wa Dawati la Jinsia,  amesema kuwa wazazi wa Mkuranga hawatoi ushirikiano pale polisi wanapotaka ushahidi wa jambo ambalo limetokea.

Katika maadhimisho ya siku Mtoto Afrika katika Wilaya ya Mkuranga wametoa msaada mbalimbali kwa watu  wenye mahitaji  maalumu ikiwemo kupatiwa watoto kadi huduma za Afya za (CHF) , Daftari, magodoro Baiskeli , mashuka.

Waliotoa msaada huo ni pamoja na Mke wa Mbunge wa Mkuranga, Mariam Ulega ambaye ametoa  vitu vyenye  thamani ya zaidi  ya sh. milioni moja.
Mariam amesema kuwa masuala yanayohusu watoto ni mengi hivyo yanahitaji ushirikiano katika kuanda taifa la leo la watoto.

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalila akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

 .Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
  Mke wa Mbunge  wa Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza katika siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimto matone  ya Chanjo ya vitamin A katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Steven Mwandambo akitoa maelezo juu chanjo vitamin A kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika  katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimkabidhi baiskeli mtoto mwenye Ulemavu , Kibibi Khamis katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga, Dk. Severine Lalika akimkabidhi  Godoro  mtoto mwenye Ualubino,Nasma Ally  katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo.
 ehemu ya watoto wakiwa katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika iliyofanyika katika Viwanja vya Shule Msingi Mwanambaya leo. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...