Mtoto wa Aga
Khan Princes Zahra Aga Khan azindua huduma mpya ya huduma za gharama na fuu kwa
wagonjwa na Maabara ya kisasa katika Hospitali
ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi huo Meneja mawasiliano wa Hospitali hiyo Olayce Lotha amesema kuwa
maabara hiyo itasaidia kutoa majibu ya vipimo ambavyo vililazimika kupelekwa
nje na kurudi hili waendelee na matibabu.
“tumetengeneza
mfano wa vitanda 20 ambavyo vitaonekana katika mradi huu, pia kwa sasa maabara
hii mpya itaweza kutoa majibu yote ya vipimo vya kansa na magonjwa mengine sugu
ambayo yalikuwa lazima yakapimwe nje ya nchi” amesema Lotha.
Amesema wodi
hizo kwa sasa zitaweza kuchukua watu wanne kwa pamoja kwa gharama nafuu tofauti
na zile wodi zingine ambazo zilikuwa zinachukua mtu mmoja mmoja kwa gharama ya
hali ya juu.
Amesema
mradi huo umetokana fedha kutoka Msaada kutoka kwa Tasisi ya Maendeleo ya
ufaransa (FDA) ambayo imetoa Bilioni 120 na bilioni 60 kutoka Aga Khan Development Network.