Wednesday, June 21, 2017

MAALIM SEIF AONGOZA ARAMBEE YA MADRASSA MUUMINI KIWALANI KUWEZESHA KUPATIKANA MILIONI SABA

 Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiongoza Arambee ya uchangiaji wa Madrasa  Kiwalani Temeke jijini Dar es Salaam ampapo aliwezesha kupatika kwafedha zaidi ya Milioni 7 kwa ajili ya ununuzi wa kiwanja kipya cha Madrasa hiyo

Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita  akizungumza wakati alipokuwakitoa ahadi yake ya Milioni moja kwa ajili ya Madrasa hiyo na aliweza kuwasilisha shilingi laki tano papo hapo na kuongeza ahadi ya bati 70 na mifuko 50 ya Saruji.


Diwani wa  Kata Mianzini , Kassim Mshamu ambaye ndio mlezi wa Madrasa ya Muunin Islamiya akiwakaribisha wageni katika arambee yakuchangia madrasa

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akikabidhi mchango wake wa shilingi laki tatu katika rambee ya kuchangia Madrassa ya  Muumini Islamiya iIliyopo kiwalani Dar es Salaam
Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akikabidhi mchango wake kwa  Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa ajili ya  Muumini islamiyaSheikh Anuary Jongo  akitoa  Darasa juu ya waslamu na umuhimu wa kuchangia nyumba za ibada hili waweze kujenga ukaribu na Mungu hasa katika kumi hili la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhani
 Sehemu ya washiriki wa arambee hiyo wakipata futari iliyoandaliwa na Madrasa Muumin Islamiya
  Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiteta na Mkurugenzi wa uchaguzi wa Chama Cha Wananchi CUF , Shaweji Mketo
 Sehemu ya watoto wa Madrasa ya Muumini Islamiya  wakipata futari mara baada ya kumalizika kwa arambeehiyo


 Vijana wa Kiislamu wakitoa Nashid kwa ajili ya kuleta burudani kwa watu waliofika katika arambee hiyo

sehemu ya vijana wa Madrassa ya Muumin Islamiya wakinyosha mikono wakati wa utambulisho

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...