Monday, June 5, 2017

MAMLAKA YA DAWA ZA KULEVYA YAKAMATA TENA KONTENA MBILI ZENYE KEMIKALI BASHIRIFU

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya imekamata kontena mbili zilizobeba kemikali bashirifu zilizokuwa tayari kwa kuingizwa nchini katika eneo la bandari kavu ya Ami Tabata Relini.

Zoezi hilo la ukamataji huo ambalo liliongozwa na kamishna  Mamlaka ya kupambana na Kudhibiti dawa hizo Siang’a akiwa ameongoza  na maofisa wa nagazi za juu.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukaguzi wa kemikali hizo Kamishna Msaidiz wa ukaguzi wa kemikali jinai , Mamuya amesema kuwa mzigo huo ni mwendelezo wa mzigo wa kampuni ya Tecno Scientific ambayo ilikuwa ikifanyia shughuli zake katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam
Amesema hapo awali waliweza kukamata lita 10,000 na mzigo ulikouwa umeingizwa katika bandari ya Dar es Salaam ulikuwa lita zaidi ya 6000 zikitokea nchini ufaransa.
Ametaja kuwa mamlaka inaendelea na uchunguzi wa kuzichunguza kemikali hizo hili kubaini kama zimefuata njia sahii ya kuingia nchini .
Amesema kuwa ikibainika kuwakemikali hizo zimeingia kinyume cha sheria wanao husika watapelekwa mahakamani.


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a akiangalia moja ya ya kemikali bashirifu katika eneo la bandari kavu ya Ami Tabata jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya watendaji wa  Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),  wakikagua kemikali ziliozpo ndani ya maboksi na kuchukua sample 
 mzigo wa kaemkali bashirifu ukipakuliwa ndani ya kontena katika eneo la bandari kavu ya Ami tabata jijini Dar es Salaam
 Kamishna Msaidzi wa ukaguzi kemikali jinai wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya  akiweka alama maboksi yaliyokutwa na kemikali bashirifu 


 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Siang'a  akiangalia mzigo wa kemikali bashirifu
 Mmiliki wa Kiwanda cha Tecno Scientific  akiwa amekaa katika eneo la bandari kavu akiangalia mzigo wake unavyokaguliwa
wafanyakazi wa TRA na  Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), wakikagua siri za kufungia kontena hili waweze kulifungua

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...