Saturday, June 17, 2017

MSHINDI WA WA MASHINDAO YA QURAN KUPEWA DOLA 25,000 ZA KIMAREKANI


.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania, Sheikh Othman Ally Kaporo (kushoto) akizungumza na  waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee. kuliani Katibu wa Kamati ya maandalinzi ya mashindano hayo.Na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ally Kaporo amesema kuwa jumuiya hiyo imetenga kiasi cha dola za kimarekani elfu 25 kwa ajili ya washindi watakaoibuka kwenye mashindano ya kimataifa ya kusoma Qur-an ambayo yanayotaraji kufanyika siku ya Jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Sheikh Kaporo ameeleza kuwa mashindano hayo ya sita kimataifa tangu waanze kuratibu yanataraji kuzishirikisha nchi 18 ambazo ni Kenya, Uganda, Mali, Nigeria, Algeria, South Africa, Bangladesh, Sudan, Kuwait, Libya, Djibouti, UAE, Russia Federation, USA, Yemen, UK, Dubai, Tanzania Bara na Visiwani (Zanzibar). Muhamedi Saidi 
Ambapo ameeleza kuwa matarajio yao yalikuwa ni ushiriki wa nchi 35 lakini baadhi yao ziliomba udhuru wa kutohudhuria kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wao.
Sheikh Kaporo amesema mgeni wa heshima katika mashindano hayo atakuwa Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddy akiambatana na mlezi wa Jumuiya hiyo Alhaj Ally Hassan Mwinyi Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sheikh Kaporo ametoa wito kwa watanzania kuhudhuria mashindano hayo na kujitokeza kwa wingi ukizingatia huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo katika kumi la mwisho iliteremka Qur-an tukufu hivyo ni vyema wakahudhuria ili waweze kupata ujira kutoka kwa mola wao (Allah).

Mshiriki wa Tanzania Omary Abdallah Salum, ambaye amewaomba watanzania kuwaombea dua kwa wingi ili waweze kupata ushindi.

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...