Friday, June 9, 2017

SPESHOZ TANZANIA YAINGIA MKATABA NA TIMU YA LIPULI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkataba wake na timu ya soka ya Lipuli ya Mkoani Iringa
 Mwenyekiti wa Lipuli ,Abu Changawa akisaini mkataba wa vifa na kampuni ya Speshoz Tanzania ambayo itatoa vifaa vya michezo kwa timu hiyo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Speshoz Tanzania ,Jeffrey Jessey  na  Mwenyekiti wa Lipuli ,Abu Changawa  wakisaini Mkataba wa Vifaa vya Michezo

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Kampuni ya uuzaji wa vifaa vya Michezo ya ,Speshoz Tanzania imeingia mkataba wa kutoa vifaa vya Michezo  kwa timu ya Soka ya Lipuli ambayo imepanda kucheza ligi kuu ya Vodacom Tanzania.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa timu hiyo mkurugenzi wa Speshoz Tanzania,Jeffrey Jessey amesema mkataba huo ambao ni wa zaidi ya Milioni 30 utawawezesha kuuza jezi za Lipuli na kuwagawia vifaa vyote vya mazoezi.

“mkataba huu utaweza kuisadia timu hii kuwa na vifaa vya uhakika na vya kisasa ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na morali na kuhimili ushindani na timu mkubwa” Amesema Jessey.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Lipuli, Abu Changawa amesema kuwa mkataba huo ni moja ya vitu ambavyo vitasaidia timu hiyo kuwa na vifaa vya uhakika.

Amesema kuwa kampuni hiyo imewapa masharti kuwa timu hiyo ikifanikiwa kubaki sita bora basi wataongeza udhamini katika msimu ujao.


Changawa amesema  ni vyema makampuni mengine yakajitokeza kusaidia timu hiyo kwa upande wa udhamini hili iweze kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...