WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Kanda ya Kaskazini.
Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.
Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .
Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.

Post a Comment

Previous Post Next Post