Friday, June 23, 2017

WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA SEMINA YA TAKWIMU HURIA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akizungumza na wadau wa Takwimu wakati wa Semina ya upatikanaji  wa Takwimu huria  katika ofsi za Serikali  iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH  Kijitonyama , ambapo wadau wa takwimu walijadili umuhimu wa Takwimu Huria  ili kuwawezesha wananchi  kupanga maendeleo yaokulingana na takwimu halisi.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) , Dkt. Albina Chuwa  akizungumza wakati wa Semina ya Takwimu huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wadau wa Takwimu walipata kujadili umuhimu wa upatikanaji  wa Takwimu huria katika ngazi mbalimbali

 Mkurugenzi wa Usimamizi wa huduma za Umma na Utendaji  kutoka Benki ya Dunia nchini, Jim Brumby akizungumza na wadau wa  takwimu juu ya umuhimu wa upatikanaji  wa takwimu huria katika kupanga mipango ya maendeleo.
 Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu nchini kutoka Ofis ya Taifa ya Takwimu a,Irenius Ruyobya akitoa neno la shukrani kwa wadau waliofika katika semina  ya Takwimu huria iliyofanyika  katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wadau kutoka sekta za serikali na binafsi walioshiriki katika Semina hiyo
Mtaalamu mkuu wa Utawala kutoka Benki ya Dunia Tanzania , Verena Luise   akizungumza wakati wa Semina hiyo kwa wadau wa Takwimu huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  Mkuu wa Twaweza nchini ,Aidan Eyakuze akionyesha ni jinsi gani watanzania wachache waliotembelea Takwimu huria na nini kinahitajika hili kila mtu aweze kuzifikia hizo Takwimu.
 Mshauri Mwelekezi wa Takwimu huria ,Rose Aiko  akizungumza juu ya umuhimu wa Takwimu huria kwa wadau walioshiriki semina  hiyo katika ukumbi wa CSOTECH Kijitonyama.
Sehemu ya Washiriki wa semina ya Takwimu huru wakiwa wanasikiliza kwa Makini

No comments:

Post a Comment

MWIJAGE MGENI RASMI KONGAMANO LA VIWANDA MNMA

Na Humphrey Shao, Globu Ya jamii Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano kuhusu Maende...