WORLD MERIT TANZANIA YAJIPANGA KUMRUDISHA RAIS TRUMP KATIKA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akimpongeza Kiongozi wa World Merit Tanzania , Rose Mmbaga  katika siku ya kilele cha Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tasisi isiyo ya Kiserikali inayojiusisha na utunzaji wa Mazingira nchini ya Word Merit Tanzania  imesema ipo katika kampeni maalum ya kuhakikisha kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anatambua uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi Duniani kwa kuanzisha kampeni ya GREEN TRUMP.

Hayo yamesemwa kiongozi wa shirika hilo nchini Tanzania , Rose Mmbaga alipokuwa akizungumza na Ripota wa globu ya Jamii wakati wakufunga siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana.

“kwa sasa tumeamua kuwa na kampeni moja ambayo inakwenda kwa jina la ‘GREEN TRUMP’ Ambayo itawakutanisha vijana wanaojitolea kwa kupanda miti nchi nzima hili waweze kumuaminisha Rais wa Marekani kuwa mapinduzi ya kijani yanawezekana  licha ya kiongozi huyu kujitoa katika ule mkataba wa Paris” amesema Mmbaga.

Ameongeza kuwa yeye kama kiongozi kijana ameamua kujikita katika kuhamasisha swala la mazingira hili aweze kusaidia vijana wengine kuingia katika mapambano haya hili nchi yetu iweze kujikinga na majanga mbalimbali.

Amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakileta majanga mengi sana nchini ikiwemo suala kurudisha maendeleo nyuma kwa kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa gharama kubwa kutoka katika fedha za watanzania.

Alimaliza kwa kusema kuwa ufike wakati wa Vijana sasa kutambua na kuheshimu mazingira hili yaweze kututunza kwa ajili ya kizazi chetu cha baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akiwa katika picha yapamoja na Vijana wa World Merit Tanzania ambao wamejitolea kutunza Mazingira nchini

Post a Comment

Previous Post Next Post