Friday, July 28, 2017

KIWANDA CHA NONDO CHA UNIQUE STEEL CHAJIPANGA KATIKA KATIKA UWEKZAJI KUHUDUMIA BOMBA LA MAFUTA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kiwanda cha uzalishaji wa nondo cha 
Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga kimesema kimejipanga kufanya uwekzaji mkubwa hili kuweza kutumia fursa ya uwepo wa ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Tanga mpka Uganda kutumia malighafi kutoka kiwandani hapo.

Hayo yamesemwa na Mhasibu Mkuu wa kiwanda hicho, Sikander Omar  alipokuwa  akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho Jijini Tanga.

 Omar amesema kuwa Wakati Serikali ikipambana kuhakikisha viwanda vinakua nchini, baadhi ya viwanda vilivyopo vimekuwa vikikumbana na changamoto mbalimbali zinazozuia uzalishaji kwa wakati.

"Moja ya changamoto hizo ni kukatika katika kwa umeme bila taarifa jambo linalotia hasara wakati wa uzalishaji. 
Mbali na hilo patikanaji wa mikopo kwa ajili ya kuwekeza zaidi imekuwa ni changamoto kwaoanapambana kukiboresha kiwanda hicho lakini umeme kutokuwa wa uhakika imekuwa changamoto".Amesema Omar.

Amesema kwa sasa wanazalisha hadi tani 60 za nondo ambazo nyingi huuzwa mkoa wa Arusha.
Akizungumzia changamoto zilizopo msimamizi wa kiwanda hicho, Jagjeet Singh alisema umeme unapokatika wakati wa uzalishaji inakuwa ni hasara kwao kwa kuwa mtambo wa kuyeyusha chuma hupoa na vyuma vilivyokuwa vinayeyuka ili kutoa nondo huganda.

 Kiwanda hicho ambacho kilikuwa cha Serikali na kuzinduliwa Julai 21, 1971 kilisimama na kuanza uzalishaji tena hivi karibuni baada ya kuchukuliwa na mwekezaji huyo.

Omar amesema hivi sasa wako katika mchakato wa kutafuta mkopo ili kukiongezea nguvu kiweze kuzalisha zaidi na kutoa huduma katika mikoa zaidi ya Tanga na Arusha ambalo ndilo soko kubwa lao lilipo kwa sasa.

 

 
 Mhasibu Mkuu wa kiwanda cha Nondo cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga, Sikander Omar akizungumza na Wandishi wa Habari waliotembelea kiwanda chake kuanagalia hali ya uzalishaji
 Watendaji wa kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga wakiwaonyesha waaandishi wa habari sehemu ya kuzalishia Nondo ambayo imesimama kutokana na matatizo ya Umeme
 Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi Boniface Meena akiangalia moja ya Nondo zinazozalishwa na Kiwanda cha Unique Steel Rolling Mills kilichopo Tanga

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...