Monday, July 24, 2017

MAWAKILI WA SERIKALI WAMWAGA TUNDU LISSU NA ARUDISHWA RUMANDE

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu kuendelea kusota rumande  hadi Julai 27 mwaka huu ambapo inatarajia kutoa uamuzi kuhusiana na  mapingamizi ya dhamana yaliyowasilishwa.

Lissu ambaye anawakilishwa na jopo la mawakili 18, amefishwa mahakamani hapo leo na kusomewa mashitaka ya kutoa lugha ya uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Hatua hiyo ya kurudishwa rumande kwa Lissu, imetokana na upande wa mashitaka kuomba mahakama kupinga dhamana ya mshitakiwa huku upande wa utetezi katika kesi hiyo, wakiomba mahakama kutoa dhamana.

Akiwasilisha mapingamizi hayo,  Wakili wa Serikali, Simon Wankyo ameiomba mahakama kupinga dhamana dhidi ya Lissu kwani anakesi zingine za mashtaka ya uchochezi zaidi nne mahakamani hapo.

Amesema, matamshi yaliyotamkwa na mshtakiwa siyo ya  kawaida kwani yanaweza sababisha chuki baina ya watanzania na mamlaka mbalimbali na kupelekea chuki ambapi matokeo yake sio madogo endapo ataachiwa kwa dhamana kwani yanagusa ukabila, udini na ukanda. 

Pia aliieleza mahakama hiyo kuwa iangalie suala hilo la kumnyima dhamana kwa kuwa wanaamini amekuwa akifanya hivyo kwa kuwa yupo nje.

Hata hivyo, jopo la mawakili wa Lissu, wakiongozqa na Fatma Karume alidai kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa na kwamba upande wa mashitaka wasilazimishe mahakama kumnyima dhamana kwa kuwa hawajakamilisha upelelezi.

Aliongez mahakama itambue kuwa Lissu ni chama cha upinzani na kwamba serikali ndio imewakilishwa kuieleza mahakama kwamba mshitakiwa ametoa maneno ya uchochezi.

Pia alidai kuwa kesi zote zinazomkabili Lissu zimeletwa kuanzia mwaka 2016 na mpaka sasa hakuna hata moja iliyoisha ambapo zote zimetokana na mshitakiwa kupaza sauti.

"Kutokana na kesi hizi upande wa serikali ndio unataka kumdhuru Lissu kwa kuwa anapopaza sauti ndipo anakamatwa na suala la chuki kidini, Lissu ni Mkatoliki kama walivyo viongozi wengine wa serikali," alidai Karume.


Baada ya kuwasilisha hoja mbali mbali, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 27, mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi.

Akisoma mashitaka hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai mshitakiwa alitenda  kosa hilo Julai 17, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni, Dar es Salaam na kutoa maneno yenye chuki yafuatayo

‘’Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ni ya kibaguzi wa kifamilia, kikabila, kikanda na kidini. Vibali vya kazi work permit vinatolewa kwa wamishenari wa kikatoliki tu huku madhehebu mengine yakielezwa kupanga foleni uhamiaji…

‘’Viongozi wakuu wa serikali, wanachaguliwa kutoka kwenye familia, kabila na ukanda …Acheni woga pazeni sauti…kila mmoja wetu tukawaambie wale ambao bado wanampa msaada wa pesa Magufuli na serikali yake kama tulivyowaambia wakati wa serikali ya makaburu, hii serikali isusiwe na jumuiya ya Kimataifa, isusiwe kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia kwa sababu ya utawala huu wa kibaguzi..yeye ni diktekta Uchwara’’ maneno ambayo yanalenga kuleta chuki ndani ya jamii.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na amerudishwa rumande

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu akiwa katika gari ya Polisi akirudishwa Rumande mara baada ya kukosa Dhamana katika kesi yake ya Uchochezi unaoleta chuki katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu  akishuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu mara baada ya kuletwa na jeshi la Polisi
 Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu, akizungumza na Makachero wa Polisi kabla ya kuingia Mahabusu
 Mwanasheria wa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu , Fatma Karume akiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo
 Mawakili wa mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu ,a uchocheziake  wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa kusikilizwa kwa kesi yake ya Uchochezi
 Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu  akielekezwa kwa kukaa na Askari wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Askari wa jeshi la Polisi wakiwa katika harakati za kuwatawanya wafuasi wa Chadema ambao walisambaa nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...