TAKUKURU YAMTIA MBARONI DIWANI WA CHADEMA KATA YA MSIGANI KWA RUSHWA





Diwani Kata ya Msigani, Ubungo, Israel Mushi ( 48 ) na Mrasimu ramani wa Manispaa ya Ubungo, Francis Mwanjela Peter ( 28 ) wamekamatwa na Tasisi ya kuzia na kupambana na Rushwa nchini 'TAKUKURU' Mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa  Sh.5,000,000/=.

kwa mujibu wa taharifa iliyotolewa na Mkuu wa  TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni Teddy Mjangira amesema kuwa Watuhumiwa walikamatwa Julai 12, 2017 baada ya kupokea kiasi hicho cha pesa toka kwa mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa na ambaye mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa alitakiwa  na watuhumiwa kuwapa  rushwa ya Sh.10,000,000/=

Watuhumiwa walishawishi na kupokea rushwa ili waweze kutoa ushawishi kwa wajumbe wa kamati ya mipango miji  inashughulikia maombi ya kubadilisha michoro, kubadilisha matumizi ya kiwanja na kupitisha kibali cha ujenzi katika Manispaa ya Ubungo.

Uchunguzi wa tuhuma unaendelea na Watuhumiwa ambao wanatuhumiwa kutenda makosa kinyume na kifungu namba 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 wamepewa dhamana.

Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Bi.T. MNJAGIRA anawaasa Viongozi wote wa Umma, Wanasiasa na Watumishi wote wa Serikali, kuheshimu nyadhifa zao na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria bila kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Pia, anatoa wito kwa  Wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na  vitendo vya rushwa ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria, Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumezuia vitendo hivyo visiendelee kujitokeza katika Jamii

 

Post a Comment

Previous Post Next Post