Thursday, July 6, 2017

WATU WAZIDI KUMIMINIKA NIDA WAONGEZA MASHINE ZA KUTOLEA VITAMBULISHO SABASABA

 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakiwa wanawaandaa watu kupiga picha katika eneo la Nje mara baada ya watu kujaa ndani na kulazimika  kuongeza mashine ndani ya maonesho ya Sabasaba ambapo itaji la watu kupata vitambulisho vya Tiafa limekuwa kubwa
 Msululu wa watu wakiwa katika eneo la nje ya banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakisubiri kupatiwa huduma kwa ajili ya kupata vitambulisho ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Sabasaba
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Hifadhi  hati  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa 'NIDA' ,Rose Mdami  akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam aliyefika kupata huduma ya Kitambulisho cha Taifa katika banda lao lililopo  katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba
Foleni ya kupata vitambulisho katika banda la ndani la NIDA ikiwa imeshika kasi kuliko kawaida hali iliyowalazimu kuongeza vifaa na watumishi wa kufanyakazi katika Viwanja vya Sabasaba
Afisa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Said Said akiwa amezungukwa na wateja mbalimbali  waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba katika eneo la nje na kuwapa maelzo namna ya kupata Vitambulisho vya Taifa
Wakazi wa jiji wakiwa wamekaa chini wakisubiri foleni yao ifike hiuli waweze kuchukua Vitambulisho vya Taifa kutoka NIDA
Maofisa  kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), akiwa Wamezungukwa na wateja mbalimbali  waliofika kupata vitambulisho vya Taifa. katika viwanja vya Maonesho Sabasaba

No comments:

Post a Comment

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA NI TISHIO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI

                         Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii  Serikali imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa ...