Tuesday, August 8, 2017

DAWASCO WAZINDUA HUDUMA YA MAJI MTANDAONI
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASCO),limezindua mfumo mpya wa Mawasiliano ambao unalenga kumrahisisha mteja kupata na kutoa taharifa.

akizungumza na Waandishi wa Habari  Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO , Kiula Kingu amesema lengo la mfumo huu ni kumuweka mteja karibu kihuduma.

"Smartphone itamuwezesha kila mwananchi kupakua huduma hii hili aweze kupata huduma kwa kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO Ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajiri mteja atatumiwa neno la Siri"amesema Kingu.

Naye Meneja uhusiano wa DAWASCO ,Everlasting Lyaro amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuuttumia na hauna gharama zozote .
amesema kuwa mfumo huo utamrahiusishia mteja kutumia kwa kupata taharifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi ,taharifa za lini mteja alifungiwa huduma za maji zikiwamo ankara ya mwezi .

amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji ,bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahii kwenye mfumo huo na DAWASCO.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO , Kiula Kingu  akionyesha mfumo wa Huduma Mtandaoni unavyofanya kupitia simu  za mkononi
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO , Kiula Kingu  akizungumza na Waandishi wa Habari
 Meneja uhusiano wa DAWASCO ,Everlasting Lyaro , akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kuzindua huduma ya simu mtandaoni
Waandishiwa habari waliohudhuria mkutano huo 

No comments:

Post a Comment

TANESCO YAWATOA HOFU WATEJA WAKE JUU YA MFUMO WA UNUNUZI WA LUKU

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Shirika la Umeme Tanzania Tanesco limewatoa hofu wateja wake juu ya mfumo wa ununuzi wa Umeme kwa ...