Tuesday, August 15, 2017

LUKUVI AKABIDHI HATI ZA KIMILA 2100 KATIKA KIJIJI CHA NYANGE WILAYA YA KILOMBERO

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii , Kilombero
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaonya wale wote watakao chukua hati za Kimila na kuwauzia watu waliopo miji sehemu ya maeneo hayo ambayo yamepimwa na Serikali na kusema kuwa  Serikali haitawatoza kodi wananchi wanaomiliki ardhi za kimila badala yake maofisa ardhi wawatoze kodi wenye hati za miaka 99 za kumiliki mashamba makubwa ya biashara.
 
Hayo yamesemwa jana na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki za kimila zaidi ya 2000  katika Kijiji cha Nyange wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro  kupitia Mradi wa Uwezeshaji Umilikishaji Ardhi (LTSP).

Lukuvi amesema  hatimiliki hizo zipo kwa lengo la kulinda ardhi ya vijiji husika na kwamba walanguzi wa ardhi hawatapata nafasi kwa kuwa ardhi iliyopimwa haitaweza kununulika kwa mtu ambaye sio wa kijiji hicho.

Amesema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya udalali wa ardhi lakini kutokana na ulinzi uliowekwa katika hatimiliki hizo, hawataweza kwa kuwa ardhi haitanunulika.

"Hili ni agizo kutoka kwa Rais Dk John Magufuli kwamba wananchi wote watakaopatiwa hatimiliki za kimila wasitozwe kodi isipokuwa wale wenye mashamba makubwa ya biashara ambao watatozwa kila ekari Sh 1,000.  Kwa kuwa hamtalipa kodi, basi fedha hiyo muitumie kuzalisha zaidi kwa manufaa yenu ya baadae," alisema Lukuvi na kuongeza;

"Ardhi iliyopangwa na kupimwa hata kama ardhi ni ndogo  inathamani kubwa zaidi ya mtu mwenye eneo kubwa ambalo halina hatimiliki."
Alisisitiza kuwa wananchi waliopewa hatimiliki za kimila wanakopesheka hivyo, benki zote zifungue milango na kuwapatia mikopo stahiki ili kuendeleza mashamba yao na kujiunua kiuchumi.

Alieleza kuwa maofisa wa serikali wanapaswa kueleza namna ya kuzalisha mazao mengi kuliko awali na kwamba ardhi isibadilishwe matumizi kama ni ya kilimo au ufugaji itumike kama ilivyotakiwa.

Lukuvi amesema katika miaka hiyo wanatarajia kutoa hati za kimila 300,000 kwa wananchi na kwamba kwa sasa asilimia 20 pekee ya ardhi ndio imepimwa na kupangwa.
LTSP ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Mashirika ya maendeleo ya Denmark kupitia Shirika la DANIDA, Sweden kupitia Shirika la SIDA na Uingereza kupitia Shirika la UKaid kwa Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro.
Mradi huo umeanza kazi ya kupima, kubainisha mpango wa matumizi ya ardhi Julai mwaka jana.

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi ,akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Nyange Kabla ya kuanza zoezi la Ugawaji hati za Kimila kwa wakzi wa Kijiji Hicho ambao wamepimiwa kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akiwa na Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Masijala ya Kijiji Cha Nyange ambayo itakuwa inatunza kumbukumbu ya hati
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi  akimkabidhi hati yake Mkazi wa Kijiji Cha Nyange , Bibi Clesencia Namuhoni  wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard  akizungumza na wakazi wa kijijii cha nyange juu ya umuhimu wa kumiliki hati za kimila katika kujiendeleza kiuchumi  wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 

 Mratibu wa Programu ya Godfrey Machabe mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
 Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi  na Wageni kutoka balozi mbalimbali wakisaini Vitabu vya wageni mara walipowasili katika kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilomber
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
 Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Morogoro Mch Getrude Rwakare akiuhutubia  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk .Kebwe Stephene Kebwe, akihutubia  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA
  Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Nyange wakifatilia hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA


 Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nyange Wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro  wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo
Wafanyakazi wa mradi wa mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support  Programme) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Lukuvi na Wadau wa Maendeleo

No comments:

Post a Comment

TFS NA WADAU WAANZA SAFARI YA KUELEKEA MISITU YA AMANI

 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Mariam Kobelo akigawa Vipeperushi kwa Wakazi wa Dar es Salaam amb...