Thursday, August 10, 2017

NMB yaendelea kung'ara Maonesho ya Nane Nane, Arusha na MorogoroNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto - Dr. Hamisi Kigwangala akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Meneja wa NMB kanda ya Mashariki – Aikansia Muro baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Maonyesho ya Nane Nane Mjini Morogoro. Kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa NMB kwa serikali – Aneth Kwayu na kulia ni Meneja wa tawi la NMB Wami – William Kaitara.

Meneja Mikopo wa NMB mkoa wa Arusha, Oscar Rwechungura (kushoto) akipokea kombe la ushindi wa kwanza kwa taasisi za fedha kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo.

Baadhi ya wafanakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi.

Picha ya kumbukumbu baada ya ushindi.

BENKI ya NMB imeendelea kufanya vizuri kwenye maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika kanda mbalimbali nchini. NMB Imeshika Nafasi ya kwanza kati ya taasisi za kifedha kwenye mikoa ya Arusha na Morogoro huku ikishika Nafasi ya tatu katika mkoa wa Dodoma.
Benki ya NMB inashiriki katika maonesho ya Nane Nane maarufu kwa wakulima kwenye mikoa sita ya Lindi, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha na Mwanza. Miongoni mwa malengo ya NMB ni kuhakikisha inarahisisha zaidi na kuchochea maendeleo ya kilimo na kuwaendeleza wakulima nchini.

Wafanyakazi wa benki ya NMB wakifurahia kombe lao walilokabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha.

Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo.

Mgeni rasmi katika kilele cha Maonesho ya Nane Nane mkoani Mbeya, Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, MHE. George Simbachawene akimkabidhi zawadi mmoja wa waliotembelea banda la NMB katika maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

MWENGE WA UHURU WAINGIA GAIRO NA KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA MILIONI MIASABA NA ZAIDI

 Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Morogoro Regina Chonjo mara ulipofika katika eneo la Ma...