Monday, August 7, 2017

ROSE MMBAGA ASHINDA TUNZO YA MWANAMKE MWENYE USHAWISHI MAREKANI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Msichana wa kitanzania Rose Mmbaga ameweza kushinda tunzo ya Mwanamke mwenye Ushawishi ‘Women in Events  Hall of Fame’ ya nchini Marekani na kuwa ni Mwafrika pekee katika kusaidia vijana na masuala ya Mazingira.


Mmbaga amesema kuwa ameshinda tunzo  hiyo kutokana na uwezo wake wa ushawishi katika kazi za kijamii ambazo amezifanya nchi nzima.


Amesema kuwa  Safari yake  ilianza na kujitolea kwa takribani miaka mitatu baada ya kuona ajira zinasumbua, na alianza na VSO international kwenye mradi wa International Citizen Service alafu nikajiunga na Restless development katika  mradi wa kijana tung’are kazini chini ya International Citizen Service programu kwa takribani miezi sita na tena nikaenda Raleigh Tanzania kwenye mradi wa Expedition.


“nilijenga shule kusaidia watoto yatima,mashirika yote nilishirikiana na vijana kutoka ndani na nje ya nchi na miradi ilifadhiliwa na DFID yani serikali ya wingereza.Haikua rahisi lakini leo hii naweza kuona matunda ya kujitolea katika jamii yangu.”amesema Rose.


kupitia safari yangu leo hii nimeweza kupata tuzo ya kimataifa kutoka Association for women in events,Hall of fame kama “Woman of Influence”(Mwanamke mwenye ushawishi) ambayo walioniwezesha ni  watu ambao wanafahamu kazi yangu na nilioshirikiana nao katika  kazi zangu haswa vijana wa kitanzania na wengi wao ni wale waliojitolea

Amesema pongezi zinamwendea mwanaharakati wa kuwasaidia wanawake duniani Mandy Sanghera ameweza kuwa wa kwanza kuninominate jina langu kati ya wanawake wengi na leo hii ninamshukuru kwa kupitia yeye nimeweza kushinda

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...