Monday, August 7, 2017

WAZIRI MAGHEMBE ASHUSHA TOZO ZA BARABARA KWA MITI YA MIKARATUSI IRINGA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amepunguza bei ya  miti aina mikaratusi kuanzia mwaka huu ambapo ada ya tozo za barabara imepunguzwa kutoka shilingi 35,000 hadi shilingi 17,800.
Waziri Maghembe amefikia hatua hiyo mara baada ya wadau kumuomba Waziri aweze kupunguza bei ya miti hiyo.
Wakati huo huo Waziri Maghembe amepiga marufuku kwa wanavijiji waojaribu kumega eneo la msitu kwa ajili ya shughuli nyingine
"Hakuna kipande chochote cha ardhi katika shamba hili kitakachochukuliwa kwa ajili ya shughuli nje ya hii inayofanyika kwa sasa
nasisitiza vijiji viendelee kupata fedha za mgawo wa miti ili watumie kwa shughuli za maendeleo." amesema Maghembe

Wadau wa Shamba la miti la Sao Hill wamempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Maghembe kwa utaratibu mzuri wa ugawaji wa malighafi ya miti kwa kuwa umesaidia kuwaondoa madalali waliokuwa wanapewa mgawo na kisha wao kuwauzia wenye viwanda kwa bei ya juu.

 Waziri Maghembe amesema kuwa ugawaji wa malighafi ya miti kwa mwaka huu umefanywa kwenye wenye viwanda tu ili kuhakikisha wanakuwa na malighafi ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza viwanda
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda hivyo wadau hao wasiishie kupasua mbao pekee wahakikishe wanatengeneza bidhaa kama vile samani katika viwanda vyao.
Amesema lengo la Serikali siyo kuishia kugawa malighafi ya miti na kupasua mbao, bali ni kutengeneza  viwanda vya mazao ya mbao
Katika hatua nyingine, Waziri Maghembe amewaagiza wadau  wanaotumisa misumeno aina ya Ding dong kuacha mara moja kwa ina ufanisi hafifu na zinapoteza kiasi kikubwa cha magogo badaala yake waanze kutumia za kisasa.


Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa utaratibu uliotumika mwaka huu wa ugawaji wa malighafi umekuwa mwarobaini wa kupunguza malalamiko kwa wadau ukilinganisha na miaka iliyopita
Aidha, aliawapongeza wafanyabiashara na wadau wa shamaba hilo kwa kulipa kodi stahiki za Serikali
 Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill katika kikao kilichofanyika jana mjini Mafinga Mkoani Iringa

Baadhi ya Wadau wa Shamba la Miti wa Sao Hill wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe katika mkutano uliofanyika mjini Mafinga mkoani Iringa

No comments:

Post a Comment

ROSEMARY LUHAMO KUTOKA DODOMA AKABIDHIWA MAMILIONI YAKE NA UMOJA SPESHO

 Mshindi wa Shindano la Moja Spesho, Rosemary  Luhamo akiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa pesa zake kupitia Benki ya CRDB na Kampun...