DC SINYAMULE ; AMEWATAKA VIJANA KUWA WAZALENDO



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule  amewataka Vijana kuwa wazalendo hili kuweza kuyaenzi yale yote yaliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kipindi cha uhai wake .

hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule alipokuwa akitoa mada  kwa vijana iliyohusu  "Kijana na Uzalendo"  kwa Vijana wa Ukwata zaidi ya 1000 wa Wilaya ya  Same na uzinduzi wa Kitabu kilichohusu Maisha ya Mwalimu Nyerere.

"Mwl. Nyerere alivyokuwa mzalendo na mpaka sasa ndiye Mtanzania wa kwanza aliyeonyesha Uzalendo wa kiwango cha juu kabisa akifuatiwa na Rais wetu wa sasa Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli hivyo nyie Vijana Mnapaswa kuenenda kama viongozi wetu hawa wanavyotutaka hili tuwe na Taifa la Wachapakazi na Wazalendo" amesema Sinyamule. 


katika Uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Kijana kwa ajili ya kuelimusha vijana wa kike kujitambua na kuchukua hatua muhimu kwa ajili ya mustakabali wao wa baadaye  kinachokwenda kwa jina la  " A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".


Mara baada ya kuzindua kitabu hicho mkuu wa Wilaya hiyo aliweza kununua vitabu 51 na kuagizwa visambazwe kwenye shule zote 51 za Sekondari Wilaya ya Same, viwekwe maktaba ili wanafunzi waweze kuvisoma 

Aidha Dc Sinyamule alimpongeza  mwandishi wa kitabu hicho Elihuruma kwa uandishi huo na kumtaka aendelee kuandika vitabu vingi zaidi kwa faida ya Vijana na watanzania kwa ujumla.
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
 Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizungumza wakati akitoa mada kwa Vijana wa Ukwata Wilaya hiyo na kabla ya kuzindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule akizindua kitabu cha A NOBLE GIRL OF NOWDAYS".
Wanafunzi wa UKWATA wamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Same juu ya mada ya Uzalendo

Post a Comment

Previous Post Next Post