MAKAMU WA RAIS AFUNGA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE TANZANIA (TPFNET)


Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameliagiza jeshi la la Polisi nchini, kuendelea kuwapa kipaumbele askari wa kike katika mafunzo mbalimbali hili waweze kukabiiana na  vitendo vya uhalifu mpya ambao umeanza kushika hatamu ukiwemo ugaidi, uchochezi, uhafidhina, wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao, utakatishaji wa fedha haramu, ujangili, usafirishaji wa dawa za kulevya na makosa mengine yanayovuka mipaka.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ame sema hayo le  jijini Dar es Salaam, alipokuwa kifunga  maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania(TPF NET)  katika viwanja vya chuo cha Polisi Kurasini yaliyokuwa na kauli mbiu ‘Usalama Wetu ni Mtaji wa Maendeleo, Tokomeza Uhalifu Kuwezesha Uchumi wa Viwanda”.

 “Tumeona juhudi zenu kwa kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yaliyokuwa korofi ila ni jukumu lenu pia kuhakikisha kuwa mnakabaliana na vitendo hivi vya uhalifu ili kuhskikisha havivurugi hali ya amani na kuhatarisha usalama wa nchi”amesema .

Ameweka wazi  kuwa ni wazi kwamba shughuli za kiuchumi zitafanyika kikamilifu iwapo nchi itakuwa tulivu na yenye amani na kwamba amani na utulivu huo ndiyo utaleta kuaminiana na kukubaliana miongoni mwa wananchi na wawekezaji, hivyo suala la ulinzi na usalama ni muhimu katika maendeleo na ustawi wa nchi.


“Changamoto hizi bado ni kubwa  mno kwa baadhi yetu yanayotuzunguka  kutokana na imani iliyojengeka kwa wananchi kuwa matukio haya. Mara nyingi yakifika polisi wengine hushauriwa kuyamaliza nje ya dola ili kuficha kile kinachoonekana kwamba ni aibu jambo hilo linapojuliaka na watu wengi na hivyo kumnyima mhanga haki yake kisheria” alisema.

Alisema pamoja na kwamba jeshi hilo limejenga madawati ya jinsia ili kukabiliana na tatizo hilo lakini kuna umuhimu wa kuzidisha utoaji wa elimu kwa jamii ili kuwaelewesha kuwa wasiwe waoga wala wasione aibu kuripoti matukio hayo.


Hata hivyo alisema, Serikali inajitahidi kuboresha jeshi la polisi kwa kuendelea kulipatia vitendea kazi na itazidi kufanya hivyo kulingana na bajeti iliyopo sambamba na kushirikiana na wadau wenye nia njema ya kuwasaidiia
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kufunga mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Ahmad Masauni wakati wa mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Ahmad Masauni akizungumza wakati wa mahadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride Maalum la Askari wa Kike Tanzania wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Inspector Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema akizungumza wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Askari wa kike nchini wakipita na bango wakati wa Maandamano Maalum kwenye mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Askari wa kike wakiw akatika gwaride maalum wakipita mbele ya  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam

Askari wa kike wakiw akatika gwaride maalum wakipita mbele ya  Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa askari wa kike kutoka kikosi cha usalama Barabarani jinsi wanvyofanya kazi wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,akipokea zawadi kutoka kwa muwakilishi wa Halotel Tanzania wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
 Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akionesha kitabu chwa muongozo juu ya Dawati la kijinsia wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam
Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikabidhi zawadi kwa Mkuu wa kituo cha Polisi Mpwapwa , Mrakibu Msaidizi wa Polisi , Mohamed Mhina wakati wa mahadhimisho ya  miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam




Post a Comment

Previous Post Next Post