UNHCR YAWAWEZESHA WAKIMBIZI WENYE MAHITAJI MAALUM KUKABILIANA NA CHANAGAMOTO ZA MAISHA NDANI YA KAMBI YA NDUTA WILAYA KIBONDO MKOANI KIGOMA

Ujumbe wa Wanahabari na wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la  Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)  Wakiwa na Maofisa wa Shirika la Help Age International wakizungumza na Kikongwe cha Miaka 80 ambaye anapata huduma za kijamii kutoka UNHCR Kupitia  Shirika la Help age ndani ya Kambi ya Wakimbizi ya Nduta Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma. Wazee na Walemavu katika Kambi hizo za wakaimbizi wamekuwa na Changamoto kubwa ya kuweza kujipatia mahaitaji ya kila siku na kufanya shughuli zingine za kuwaingizia kipato hili waweze kujikimu hivyo UNHCR Kupitia Mashirika Saidizi imekuwa ikitoa  Msaada kwa makundi hayo maalum
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) wa Masuala ya Ustawi wa Jamii, Grace Atim akionyesha Jiko la Mafuta ya taa linalotumiwa na  Kikongwe wa Miaka 80 ndani ya nyumba yake iliyopo ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nduta Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma jiko hilo limekuwa msaada kwake kwani hawezi tena kutembea umbali mrefu ndani ya kambi kwenda kutafuta nishati ya kupikia.
 Mmoja wa walemavu waishio ndani ya kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambaye ana uwezo wa kufanya kazi za useremala, akieleza namna ambavyo Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa kushirikiana na Help Age International walivyomuwezesha kuendeleza shughuli hizo kwa lengo la kuweza kijikimu kimaisha baada ya kujengewa uwezo. 

 
 Mmoja wa wazee wanaowezeshwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia taasisi ya Help Age Interanational jinsi ya kusuka viti vya asili akipokea maelekezo kutoka kwa Afisa wa Masuala ya Ustawi wa Jamii (UNHCR), Grace Atim. Lengo la kutoa mafunzo mbalimbali kwa nadharia na vitendo kwa wakimbizi waishio ndani ya kambi za wakimbizi ni ili kuwawezesha kuwa na shughuli za kujiongezea kipato pindi watakaporejea katika nchi zao.
Watumishi wa Shirika la Help Age International wakiwa wanaingia katika moja ya nyumba ya Mkimbizi mwenye mahitaji maalumu ndani ya kambi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma. Watumishi hao wamekuwa wakitembelea nyumba za watu wenye mahitaji maalum kila siku hili kubaini ni changamoto gani wanakabiliana nazo ndani ya kambi hiyo 


Baadhi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wakimsikiliza mwalimu katika kambi ya Wakimbizi ya Nduta Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma
--









Post a Comment

Previous Post Next Post