Sunday, January 8, 2017

MCHENGERWA:BAADHI VIONGOZI SERIKALINI NI WAFUGAJI NDIO MAANA WANASHINDWA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO.


Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa wa tatu toka kushoto akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mgomba Kati katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitaftia ufumbuzi.

MBUNGE wa Rufiji ,Mohamed Mchengerwa (CCM),amesema viongozi wengi serikalini ni wafugaji  ndio maana wanashindwa kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikisababisha madhara makubwa kwa wananchi kila kukicha.


Mchengerwa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mgomba kati ambao walieleza jinsi wafugaji wanavyoingiza mifugo hao katika mashamba ya wananchi wakati wakiwa hawajavuna mazao yao na kwamba kila walikokuwa wanapeleka kilio chao  wafugaji wanatoa rushwa wanashinda kesi.


"Wafugaji wanatuumiza mno lakini haya yote ni kwasababu viongozi wengi ni wafugaji hivyo wanashindwa kuingilia kati suala hili badala yake wanaacha wananchi wauane kila kukicha,utafika wakati tutashindwa kuyavumilia haya, tunakufa njaa na umasikini kwasababu ya watu"alisema na kuongeza kuwa


 "Yametokea matukio makubwa ya kuuliwa wananchi wawili katika kijiji cha Kilimani mwezi uliopita lakini sikuona kiongozi yeyote serikalini aliyetolea tamko au hata kufika eneo la tukio vivyo hivyo hata kwa yule mwananchi wa Morogoro aliyechomwa mkuki shingoni ukatokea mgongoni viongozi wametulia tu"Alisema sio Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ,Charles Tizeba ,Naibu wake William Ole Nasha wala Makatibu wakuu wao wawili waliofika katika maeneo yaliyoathirika au hata kutolea matamko ya makatazo dhidu ya jambo hilo na kwamba hayo ndio matunda ya viongozi wengi kuwa wafugaji hivyo kushindwa kuja na njia as kutafuta suluhisho za kudumu.


Alisema  suala la kuwepo kwa mifugo Rufiji limetokana na rushwa iliyotolewa kwa viongozi waliokuwepo madarakani miaka ya 2005 kutokana na kuwa walitoa mifugo kwenye bonde ili lisiharibike na kupeleka katika bonde lingine ili kuua wananchi wa maeneo hayo.


"Mifugo hapa kwetu ilikuja Mwaka 2005 ilihamishwa kutoka bonde la Ihefu Iringa kwakuwa lilikuwa linaharibika lakini cha kushangaza ikaletwa katika bonde la Rufiji ili liharibike na sisi wananchi wa huku tupate shida na ndicho kinachotokea Leo hii "alisema Mchengerwa


Alieleza kuwa amechaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuwawakilisha vyema kwa kutetea maslahi yao na ndicho anachokifanya na kwamba hatarudi nyuma katika kudai haki na maendeleo ya Rufiji  kwani wamekuwa nyuma kwa miaka mingi  kutokana na kukosa wawakilishi wenye nia ya dhati ya kuwasaidia.

JAMBO LEO WALIVYOUPOKEA MWAKA MPYA 2017


 Wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo linalochapishwa na Kampuni ya Quality Media Group Limited wakiwa na furaha wakati wa hafla ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2017 kwenye Ukumbi wa Ground Zero, Kurasini Dar es Salaam juzi.
 Wakigongeana ikiwa ni ishara ya kutakiana heri ya Mwaka Mpya wa 2017
 Wakicheza kwa furaha muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Kamati ya hafla hiyo ambaye ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti hilo, Richard Mwaikenda akimtambulisha Mkurugenzi wa Gound Zero Lounge, Juma Pinto kwa madereva wa Kampuni Mama ya Quality Group Limited (QGL), Salumu (kushoto) na Ramadhan
 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa akisalimiana na Juma Pinto. Kushoto ni Mhariri Mwandamizi wa gazeti hilo, Leon Bahati.
 Wajumbe wa Kamati ya Sherehe hiyo wakijadiliana kuweka mambo sawa. Kutoka kushoto ni Zahoro Mlanzi, Grace Sima, Asha Kigundula na Neema Mgonja.
 Katibu wa Kamati ya Sehetrehe, Neema Mgonja (aliyesimama) akiwapa utaratibu wa maakuli wajumbe. Kutoka kushoto ni Mwnyekiti wa Kamati hiyo, Richard Mwaikenda, Grace Sima, Jemmah Makamba na Dalila Sharif
 Mhariri wa Habari wa Jambo Leo, Kachenje 9kulia0 akitaniana na Mhariri Mwandamizi, Frank Balile na Mhariri Mwandamizi wa Jambo Leo Wikiend, Said Mwishehe.
 Ni furaha kwa wote
 Sasa ni wakati wa msosi.

 Charity James na Charles Jemes wakiserebuka
 Ni msosi, vinywaji kwa kwenda mbele
 Mpigapicha wa gazeti la Jambo Leo, Janeth Shekunde akimlisha ndafu Asha Kigundula ambaye alikuwa mweka hazina wa kamati hiyo ilifanikisha sherehe hiyo
 Mpigapicha wa gazeti la Jambo Leo, Khamisi Mussa (kulia0 na Frank Balile wakila nyama choma ya mbuzi
 Chief Sub Editor wa Jambo Leo, Joseph Kulangwa akicheza muziki na Stelah Kessy  pamoja na Charity James
 Sasa ni wakati wa supu ya mbuzi
 Ni furaha, furaha, furahaaaaaaaa
 Mwaikenda akiwa na Jemmah Makamba (katikati) pamoja na Dalila Sharif
 Baadhi ya waandishi wa kike wa Jambo Leo wakiwa na sura zenye bashaha wakati wa hesrehe hiyo
 Sasa ni mwendo mdundo
 Mhariri Mtendaji wa Jambo Leo, Mwess (katikati) akifurahi na baadhi ya waandishi wa habari wa gazeti hilo
 Mmoja wa Wakurugenzi wa Ground Zero Lounge, Benny Kisaka akisalimiana na Mhariri wa Jambo Leo, Kachenje. Kushoto ni Mhariri Mwandamizi wa gazeti hilo, Mashaka Mgeta na Kulangwa.
 Maakuli, maakuli, maakuli
 Mwesa na Bahati wakiwa na furaha
 Mwaikenda akiserebuka na Jemmah
 Kachenje na Charity ni muziki tu
Wasanifu kurasa wa gazeti hilo wakipata supu ya mbuzi. Kutoka kulia ni Grace Sima, Robert na Khamisi Kumbuka

WAZIRI MKUU AAGIZA MAAFISA WANNE WAKAMATWE*Ni kwa tuhuma za uzembe na upotevu korosho zaidi ya tani 2,000
* Wapelekwa Masasi chini ya ulinzi wakajibu tuhuma zinazowakabili

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji awakamate maafisa wanne na kuhakikisha wanapelekwa Masasi chini ya ulinzi ili wajibu tuhuma za upotevu wa tani 2, 138 za korosho.

Maafisa hao ni Kaimu Meneja Mkuu Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi (MAMCU), Bw. Kelvin Rajab na Meneja Tawi wa MAMCU, Bw. Lawrence Njozi. Wengine ni wakurugenzi wa kampuni ya YURAP ya Masasi inayohusika na uhifadhi wa mazao kwenye maghala, Bw. Yusuph Namkukula na Bw. Ramadhani Namakweto.

Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo kwenye kikao alichokiitisha Songea mjini jana jioni (Jumamosi, Januari 7, 2017) baina ya watendaji kutoka Bodi ya Korosho Tanzania, MAMCU, wamiliki wa ghala la BUCO – Masasi na kikundi cha wakulima sita waliowawakilisha wenzao kutoka vyama vya msingi (AMCOS) za wilaya za Mtwara na Masasi.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu alitaka apatiwe maelezo ya kina ni wapi zilipo hizo tani 2,138 za korosho wakati taarifa waliyompatia viongozi hao jana inaonyesha kuwa waliuza korosho zote na hakuna hata kilo moja ambayo haijanunuliwa katika mnada wa tano uliofanyika Novemba 10, mwaka jana.

Kaimu Meneja Mkuu wa MAMCU, Bw. Kelvin Rajab alikiri mbele ya Waziri Mkuu kwamba korosho zote ziliuzwa na zilishalipwa an wanunuzi wa mnda wa tano lakini akadai hakupewa taarifa ya kukosekana kwa kiasi hicho cha korosho. Naye mmiliki wa ghala la BUCO, Bw. Ramadhan Namakweto alikiri kupokelewa kwa korosho hizo ghalani kwake lakini akashindwa kutoa maelezo ni kwa nini hazionekani zilipo.

“Tangu mnada wa tano, mmekwishafanya minada mingine mitano hadi kufikia mnada wa 10. Kama kweli hizo korosho zipo ghalani, ni kwa nini korosho za hawa wakulima hazijatolewa ghalani na kuuzwa katika minada iliyofuata huku taarifa yenu ya fedha kuwa mlishazipokea na kuziuza?” alihoji Waziri Mkuu bila kupata majibu ya kueleweka.

Tuhuma zinazowakabili maafisa hao wanne ni kuwalipa kilo pungufu ya zile zilizowasilishwa ghalani, wakulima wa korosho katika wilaya ya Masasi na kutowapa maelezo yoyote juu ya upungufu huo. Mfano ni kufanya makato ya unyaufu kwa wakulima wa chama cha msingi CHAMALI kinyume na maagizo ya Serikali.

Nyingine ni kutowalipa fedha kwa wakati wakulima waliouza korosho kwenye mnada wa tano wa tarehe 10 Novemba 2016 na kutokutoa maelezo yoyote licha ya kuwa MAMCU ilishauza korosho hizo kwenye minada iliyofuatia na kupokea malipo.Nyingine ni kutopelekwa mnadani kwa makusudi kwa tani 2,138 za korosho zilizokuwa katika maghala ya Mtandi na BUCO tangu Novemba 11, mwka jana; kutokutolewa taarifa ya kuwepo korosho hizo kwa mamlaka husika na kuwasababishia hasara wananchi.

Tuhuma nyingine ni kushindwa kufuatilia malipo ya korosho ya tani 1,156,262 ambazo ziliuzwa kwenye mnada wa 10 uliofanyika Desemba 21, 2016. Korosho hizo zilinunuliwa na Maviga East Africa (tani 503,297); Machinga Transport (tani 104,200); Tastey (319,576) na Saweya Impex (tani (229,189).

Kutokana na mapungufu hayo, Waziri Mkuu aliagiza watu hao wapelekwe Masasi chini ya ulinzi ili uchunguzi ufanyike na pia amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) afanye ukaguzi wa hesabu za MAMCU na kujiridhisha kiasi cha korosho kilichonunuliwa; fedha zilizolipwa na kuingia akaunti za MAMCU; kiasi cha fedha zilizolipwa kwa vyama vya msingi na wananchi kwa ulinganifu na bei ya korosho kwa kila mnada husika.

Mapema, wakisoma risala yao kwa Waziri Mkuu, wakulima hao walisema wana kero nyingi sana kama vile kutolipwa fedha zao kwa wakati; kutoeleweka mahali zilipo korosho ambazo walishaziuza kwa MAMCU, kukatwa makato ya unyaufu ambayo Serikali ilikwishapiga marufuku na kutosikilizwa malalamiko yao na viongozi wa MAMCU pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya.

“Makubaliano yalikuwa ni kwamba mkulima atapewa fedha yake siku sita baada ya mnada kufanyika lakini hivi sasa baadhi yetu tumeuza korosho tangu Oktoba, mwaka jana lakini hadi imefika Januari hii bado hatujalipwa. Pia kuna makato yaliyoondolewa kwenye mfumo, kwa mfano unyaufu lakini wao wameyaacha na unapoenda kuuza wanahesabu na kukukata kuwa utalipia gharama za unyaufu,” alisema msoma risala Bw. Sylvester Mtimbe ambaye pia ni mkulima kutoka AMCOS ya Chiungutwa.

Wakulima hao wa korosho kutoka Masasi mkoani Mtwara walikutana Januari 3, 2017 katika kijiji cha Chiungutwa na kuazimia kuwa wangeandamana hadi Dar es Salaam ili wawasilishe kilio chao kwa Waziri Mkuu au kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli.

Kwa kutambua umbali uliopo kutoka Masasi hadi Dar es Salaam na kwamba yeye hakuwepo katika siku waliyopanga kwenda huko, Waziri Mkuu aliamua kuwaita wakulima hao wamfuate Songea ambako alikuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, JANUARI 8, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuhoji Kaimu Meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika Masasi Mtwara (MAMCU) Bwana Kelvin Rajabu kuhusiana na upotevu wa koroshozaidi ya tani 2000 Waziri mkuu alifanya kikao na Bodi ya korosho pamoja na baadhi ya wanaushirika Mamcu kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Ikulu ndogo Mkoani Ruvuma
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Zuberi Mwombeji akiwatarifu Maofisa wa Mamcu na Yurap wako chini ya ulinzi wa polisi kuhusiana na upotevu wa korosho tani 2000 kulia mwenye kaunda suti Kaimu meneja mamcu Bwana Kelvin Rajabu anayefuatia Mkurugenzi wa YURAP inayojishughulisha nauhifadhi korosho katika Ghala la BUCO Masasi Bwana Yusuf Namkula anayefuatia Mkurugenzi mwenzake Bwana Ramadhan Nama na Meneja tawi la Mamcu Bwana Lawrence Njozi
Watuhumiwa wakipelekwa kupanda gari la polisi kwa ajili yakuwapeleka rumande
Kaimu Meneja wa Mamcu bwana Kelvin Rajabu akipanda gari la polisi tayari kwakwenda rumande.Picha na Chris Mfinanga

DKT. SHEIN AZINDUA SOKO LA MATUNDA NA OFISI YA BARAZA LA MJI WETE PEMBA

DKT. SHEIN AZINDUA SOKO LA MATUNDA NA OFISI YA BARAZA LA MJI WETE PEMBA

Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa Soko la Matunda na Ofisi ya Baraza la Mji la Wete katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman (wa pili kushoto).

Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid wakati alipolitembelea Soko la Matunda Wete Mjini Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kulizindua rasmi leo katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapungia mkono Wananchi wa Wilaya ya Wete leo baada ya kulizindua rasmi Soko la Matunda na Ofisi ta Baraza la Mji Wete Mkoa wa Kaskazini ikiwa ni katika Shamara shamra za Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar,(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Nd,Radhiya Rashid.
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika viwanja vya Soko la Matunda Wete leo katika Uzinduzi rasmi wa Soko hilo sambamba na Ofisi ya Baraza la Mji Wete, katika sherehe za shamara shamara za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika viwanja vya Soko la Matunda Wete leo katika Uzinduzi rasmi wa Soko hilo sambamba na Ofisi ya Baraza la Mji Wete, katika sherehe za shamara shamara za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapindzi Zanzibar.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 9, 2017


BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...