Saturday, January 21, 2017

45 AMERICAN PRESIDENT INAUGURATION

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYANaibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu   kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari  lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele  ni   Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia)  na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

NAIBU MEYA ILALA AWATAKA WENYE VIWANDA KULINDA MASLAHI YA WAFANYAKAZINaibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary  Kumbilamoto akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha ZENUFA.Mkurugenzi wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akizungumza na wadau wa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho na muonekano wa alama mpya.Afisa Tarafa Ilala , Edita Samson akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.


Mkurugenzi mtendaji wa bohari ya Dawa nchini(MSD), Laurean Rugambwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto amewataka wenye viwanda kulinda maslahi ya wafanyakazi kabla ya serikali kuingilia kati.
Kumbilamoto amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kiwanda cha dawa cha ZENUFA kilichopo kata ya Kipawa.

“tunashukuru kwa ujenzi wa kiwandahiki na kuweza kuongeza ajira kwa vijana wetu kama ilivyo sera ya serikali kuwa nchi ya viwanda lakini kikubwa ninacho waomba muweze kuangalia maslahi ya wafanyakazi kuliko kusubiri msumbuliwe na serikali”amesema Kumbilamoto.

Ametaja kuwa itakuwa jambo la aibu kuona mkuu wa mkoa au Meya ama Naibu Meya anakuja tena kiwandani hapa kwa ajili ya kuja kusuluhisha mgogoro wa kiwanda na wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa boahari ya dawa nchini, Raurean Rugambwa amesema kuwa serikali imejipanga kuakikisha inasaidina na wawekezaji wa viwanda vya dawa kwa kuwa hakikishia uakika wa soko.

Ametajakuwa kwa sasa serikali yako imekuwa ikiagiza dawa kwa asilimia 90% kutoka nje ya nchi kutokana na upungufu wa viwanda vya dawa hapa nchini.

Hivyo amewataka wawekezaji kujitokeza katika uwekezaji mpya wa viwanda vya dawa katika mpangomaalumu wa mashirikiano na serikali(PP).


wananchi na wadau waliofika katika uzinduzi huo wakifatilia kwa makini matukio yanayoendelea

Mkurugenzi wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akiwaonyesha wageni waliofika kiwandani hapo sehemu ya kiwanda hicho ambacho kinazalisha dawa aina ya Zenufa.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam,Ramadhani Madabida akizungumza jambo na mmoja wa watumsihi kutoka MSD waliofika katika uzinduzi wa kiwanda hicho.

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa ...