Thursday, February 2, 2017

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA UJENZI WA BARABARA ZINAZOPITISHA MAGARI MACHACHE


Mhandisi Ven Ndyamaka kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) akizungumza na waandisi kutoka mikoa mbalimbali nchini


waandisi mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo .Katibu mkuu wizara ujenzi na mawasiliano-ujenzi, Joseph Nyamuhanga akihutubia wakandarasi waliofika katika kongamano hilo la wahandisi.Katibu mkuu wizara ujenzi na mawasiliano-ujenzi, Joseph Nyamuhanga akikabidhi nyaraka kwa Mhandisi Ven Ndyamaka kutoka TANROADS.


Katibu mkuu wizara ujenzi na mawasiliano-ujenzi, Joseph Nyamuhanga akikabidhi nyaraka kwa mwakilishi wa DFID,Amanda Duff.

. Katibu mkuu wizara ujenzi na mawasiliano-ujenzi, Joseph Nyamuhanga akikabidhi nyaraka kwa Dk Christina Katibu mkuu wizara ujenzi na mawasiliano-ujenzi, Joseph Nyamuhanga akikabidhi nyaraka Kayoza kutoka TANROAD.

SERIKALI YAZINDUA MWONGOZO WA UJENZI WA BARABARA ZINAZOPITISHA
MAGARI MACHACHE
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali imesema  kuwa kutokana na kukosekana kwa mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache  ulikuwa  unagharimu  fedha nyingi ikiwa ni pamoja  wakandarasi  kupata changamoto katika kufanya ujenzi wa barabara  hizo.

Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga  wakati wa uzinduzi wa  mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache, amesema  mwongozo huo utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu.

“Ujenzi na ukarabati ya barabara zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu, kama tutatumia mwongozo huu kwani utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini”, amesema Katibu Mkuu.

Amewataka wahandisi na Mafundi ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.
“Hakikisheni wahandisi na Mafundi ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo na kuanzia sasa uwe dira kwenu katika kazi zenu za kila siku”, amesisitiza Eng. Nyamhanga.

Mhandisi Nyamuhanga amesema kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao wa barabara nchini ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na vijijini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo, Mhandisi ,Ven Ndyamukama amesema kuwa mwongozo huo unafananua namna ujenzi wa barabara hizo unavyokuwa ikiwemo kujenga kulingana na idadi ya magari yanayopita.

Ameongeza kuwa Mwongozo huo unaelekeza kutumia rasilimali chache zilizopo na kuhakikisha masuala ya mazingira katika maeneo yanayojengwa barabara hizo yatazingatiwa.

TASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

 Mwanzilishi wa Tasisi ya Humanity  Action For Children Foundation , Rahma Mohamed Abdalah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa ...