Friday, February 10, 2017

KUMBILAMOTO ATETA NA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA ILALA

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akizungumza na wafanyabishara wa soko la Ilala
 Wafanyabiahsra wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto katika mkutano wa halmashauri ya Ilala na wadau wa soko hilo.

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa ameongozana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.

Thursday, February 9, 2017

WEMA ACHIWA KWA DHAMA ARUDI USWAHILI KWA MBWEMBWE

 Wema Sepetu akishuka katika gari ya Polisi huku pembeni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akipunga mkono akitokea katika gari hiyo kwa mbele

 Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii
Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana msanii maarufu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambaye kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni tano.

Baada ya kutimiza masharti hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Thomas Simba aliwataka washitakiwa kuhakikisha hawaruki dhamana waliyotakiwa na kuhakikisha wanafika mahakamani hapo kila wanapohitajika.

Hata hivyo, aliwataka  mawakili wa serikali  kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo ifike mwisho.

Mbali na wema washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa ambaye ni mfanyakazi wa ndani na Matrida selemani Abas ambaye ni Mkulima.

Wote watatu wanashtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba  17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, iwapo Wema na wenzake watapatikana na hatia basi watatakiwa kulipa faini isiyozidi sh.laki tano au kwenda jela.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili Pamela Shinyambala walidai kuwa Wema na wenzake watatu walitenda kosa hilo tarehe 4 February mwaka huu, huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio.

Ilidaiwa kuwa, siku hiyo walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi viwili vya banfi vyenye gramu 1.80.

Hata hivyo washtakiwa wote wamekana mashtaka.

Akielezea hali ya upelelezi wakili Katuga alidai "mheshimiwa Hakimu, upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika tunasubiri taarifa kutoka kwa Mkemia Mkuu ambayo tunategemea kuipata hivi karibuni".

Hakimu Simba aliwapa washtakiwa masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao weka dhamana na milioni tano.

mshtakiwa Wema na Wenzake walitimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo February 22 mwaka huu.

Nje ya Mahakama
Umati wa watu na wasanii mbali mbali walijaa nje ya mahakamaj kumlaki Wema akitoka mahakamani baada ya kutimiza masharti ya dhamana.


 Wema Sepetu akitolewa kutoka mahabusu ya Hakimu Mkazi Kisutu
 Wema Sepetu akishuka katika ngazi za Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuamuriwa apte dhamana ya mahakama.
 Weme sepetu akipanda kwenda kusaini hati ya Dhamana kwa hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu
Wema akishuka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Wema Sepetu akiwa nje na kwa dhama akiwa ameongozana na wakili
 Wema akirudi mahabusu ya hakimu mkazi kisutu akiwa chini ya ulinzi
 aliyekuwa meneja wa wwema  akitoka mahakamani
 Baadhi ya wasanii waliofika mahakamani hapo
Mama wema akiwa naingia mahakamani

KIAPO KIBOVU CHAMPA DHAMANA TUNDU LISU

 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akipelekwa mahabusu kwa jili ya kusubiri kupandishwa kizimbani


Na Karama Kenyunko
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali hati ya kiapo ya mkuu wa upelelezi Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Denis Mujumba na kumuachia Tundu lissu kwa dhamana.
Lissu yuko nje kwa dhamana ya shilingi milioni ishirini na mdhamini mmoja.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kumsomea Lissu ambaye ni Mbunge na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani mashtaka yake na kuwasilisha hati ya kiapo kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo alisema kuwa kiapo kilichowasilishwa mahakamai hapo na upande wa mashtaka kina mapungufu makubwa sana.

Amesema kuwa kukosekana kwa namba ya kesi na mahali ambapo inaonyesha muapaji wa kiapo hicho aliapa ni mapungufu makubwa. 

Ameongeza kuwa mshtakiwa Lissu anahaki ya kupata dhamana kwa kuwa shtaka analikabiliwa nalo linadhaminika licha ya kuwa na kesi tatu tofauti mahakamani hapo kama ambapo kiapo kilivyosema.
Amesema kuwa, licha ya kuwa Lissu kweli anamashtaka mahakamani hapo lakini hakuna shtaka hata moja ambalo amekutwa na hatia na alilokutwa nalo na hatia Kabla ya kiapo hicho jopo la mawakili wanne likiongozwa na wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kishenyi aliyekuwa akisaidiana na Wakili Easter Martin, Jackline Nyantori na Clementina Masawe walimsomea mshtakiwa mashtaka yake manne yanayomkabili ya kutoa lugha ya uchochezi.
Lissu ambaye amefikishwa katika viwanja vya mahakama hiyo leo majira ya saa 11.42 asubuhi akiwa ndani ya land lover ya polisi pamoja na msanii maarufu wa uigizaji nchini Wema Sepetu na watuhumiwa wengine alikamatwa juzi mara baada ya kutoka kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Saa 12:24 mchana, Lissu alipandishwa kizimbani Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa manne ya kutoa lugha ya uchochezi.
Katika kesi hiyo namba 48 ya mwaka 2017, Lissu anatetewa na mawakili watano, Peter Kibatala, Omary Msemo, John Mallya na Fredrick Kihwelo.Jeremiah Ntobesya.

Wakili Kishenyi alidai kuwa Januari 11, mwaka huu maeneo ya Kibunju Maungoni maeneo ya Magharibi B wilaya ya Mjini Magharibi mkoa wa Zanzibar Lissu alitoa matamko mbalimbali ya uchochezi
Moja kati ya mashtaka hayo ni kwamba mshtakiwa Lissu akiwa kama Mtanzania kutoka Bara, kabla ya uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, ambapo akiwa kwenye Kampeni alisema kuwa “…Tangu mwaka 1964 Tanganyika ndiyo inayoamua nani atawale Zanzibar…”. Kishenyi alidai kuwa maneno hayo yangesababisha uvunjifu wa amani.
Mshtakiwa Lissu alipoulizwa kama ni kweli ametenda makosa hayo, alikubaliana na makosa yote na kudai kuwa ni kweli alisema hayo maneno lakini kusema ukweli sio kosa la jinai, hivyo jibu lake ni hapana.


Matamko mengine anayodaiwa kutamka Lissu ni kuwa,  “…Tangu mwaka 1964 Zanzibar inakaliwa Kijeshi na Tanganyika, nane anaye bisha…Tangu mwaka 1995 ikifika uchaguzi askari wa Tanganyika wanahamia Zanzibar ili kuja kuhakikisha vibaraka wao wa Zanzibar hawaondolewi madarakani na wananchi wa Zanzibar mnapigwa,
Mnateswa, mnauawa kwa sababu ya ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar….,Marehemu Karume alipoanza kushtakiwa mwaka 71, 72 akauawa…itakapofika tarehe 15 mwezi wa kwanza muadhimishe miaka 53 ya kukaliwa kijeshi na Tanganyika…,”.
Aidha inadaiwa kuwa, siku na mahali hapo Lissu akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani alisema kuwa “…Jumbe aliondolewa Dodoma, na Ally Hassan Mwinyi alipewa urais wa Zanzibar Dodoma, na aliyempa ni Nyerere na si Wazanzibar…, marais wa Zanzibar wote ni made in Tanganyika…, wametengenezwa Tanganyika, wako madarakani kwa sababu ya Tanganyika,”.
Katika shtaka la mwisho la kutoa lugha ya uchochezi kwa kutamka kuwa
“…Zanzibar wanatawaliwa na Tanganyika kwa kivuli cha Tanzania, Tanzania ni Tanganyika…, Tanzania ni kivuli tu cha kuikalia Zanzibar, cha kuigeuza Zanzibar koloni, na makoloni uwa yananyonywa,
Yananyonywa kisiasa, kiuchumi na yanakandamizwa kijeshi…Metawaliwa na Tanganyika kisiasa miaka yote hii…, Mohamed Shein hana lolote ni kibaraka tu siku watawala wakisema hatufai ataondolewa tu kama alivyo ondolewa Aboud Jumbe…,”.
Kishenyi alidai kuwa maneno hayo ya Lissu yangesababisha uvunjifu wa amani.
Baada ya kusoma mashtaka hayo upande wa serikali ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba kesi hiyo iahirishwe.
Aidha aliomba mahakama kuzuia dhamana kwa mshtakiwa, maombi ambayo yanaungwa mkono na kiapo kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Ilala, ASP  Mujumba.
Kiapo hicho kimewasilishwa kikiwa na hoja kadhaa ya kutaka Lissu akose dhamana ikiwemo ya kukabiliwa na kesi tatu katika mahakama hiyo ikiwemo namba 279/2016, 218/2016 na 233/2016.
Hata hivyo Hakimu Shahidi baada ya kupitia hoja zote zilizotolewa na upande wa utetezi na ule wa serikali alifikia uamuzi kuwa,mshtakiwa anahaki ya kupata dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili inadhaminika na kwamba hati hiyo ya kiapo inamapungufu sana.

Tundulisu akishuka kwenye gari akiwa amebeba suti yake
Tundu Lisu akielekea Rumande kwa ajili ya kusubiri kupandishwa kizimbani

MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN YAFANA

 Wahitimu wa Chuo kikuu cha Aga khan wakiingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Wahitimu wa chuo kikuuucha Aga Khan miaka wakingia katika mahafali ya chuo hiyo
 Wazazi na wageni waalikwa waliofika katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Aga Khan jijini Dar es Salaam
 Naibu Gavana wa Benki Kuu nchini Tanzania, Lila Mkila akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Aga Khan


 Rais wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Firoz Rasul akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa chuo hichi
 Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha Aga Khan wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa chuo hicho

MANJI ATINGA POLISI KUITIKIA WITO WA MAKONDA


 Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye
 Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho
 Manji akisalimiana  na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati
 Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi KatiWednesday, February 8, 2017

MBOWE, IDD AZAN WATAKIWA KURIPOTI POLISI

NEWSSSSSSS
Awamu ya pili ya ya listi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aawanika vigogo wakuu nchini wakiwemo wanasiasa.
Makonda amtaja Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe,Mchungaji Josephat Gwajima, Mbunge Mstaafu wa Kinondoni , Iddi Azzan na Mfanyabiashara  maharufu na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufu Manji.

Makonda ambaye amekiri kukamtwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM mara baada ya kusambaa kwa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuwa yumo ndani.
Pamojana matajiri wanaomiliki meli za mafuta na mduka makubwa ya nguo nchini

SIMU NA MANGE KIMAMBI KUMSOTESHA WEMA SEPETU RUMANDE
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Matumizi ya simu ya mkononi huku akiwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi ni moja ya mambo yalitojwa kumfanya mtuhumiwa wa kesi ya Dawa za kulevya Wema Sepetu kuendelea kusota rumande.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa moja ya makosa katika nchii hii ni mtu akiwa yupo chini ya ulinzi alafu kuendelea kutumia simu ya mkononi.
Amesema kuwa mrembo huyo ambaye alikuwa akituma Video na sauti mbalimbali kuhusu hali ya maisha akiwa mahabusu ya kituo cha kati huku akimkejeli mkuu wa mkoa uenda akaendelea kuwa katika wakati mgumu zaidi kutokana na kitendo hicho cha kutumia simu akiwa mahabusu.

Makonda ametaja kuwa amezungumza na wakuu wa magereza yote yaliyopo Dar es Salaam na wakuu wa mikoa juu ya vitendo vya watu kuingia na simu katika vituo vya Polisi.
Pia amesema kuwa matumizi ya simu hizo watu wakiwa gerezani yamekuwa yakitumika kuendeleza biashara zao za dawa za kulevya kwa njia ya mawasiliano hata kama wakiwa ndani.


WAZIRI WA ARDHI AKABIDHI HATI 1,361 MKOANI MOROGORO


Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekabidhi hati miliki za ardhi 1,361 kwa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Waziri Lukuvi amegawa hati hizo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mvomero kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji kote nchini kuhakikisha wanakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea katika maeneo yao.

Pia amesema ili mwananchi aweze kujikimu kimaisha ahakikishe anazitumia hati miliki hizo za kimila kujiletea maendeleo na anaweza kuomba mkopo benki kwa kutumia hati hiyo ili kuendesha shughuli zake za kujipatia kipato kupitia eneo analomiliki kisheria.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amewataka wananchi kuzitunza hati hizo walizokabidhiwa na kuyatumia mashamba yao waliyomilikishwa kwa kuyalima na sio kuyauza au kukodisha kwa watu wengine na wao kubaki masikini.

Waziri Lukuvi pia alimtaka Mkuu wa mkoa wa Morogoro ayaainishe mashamba mengine makubwa yasiyoendelezwa na kugeuka kuwa mashamba pori ili amshauri Rais kuyafutia umiliki wa mashamba hayo na kurudishwa kwao ili kuweza kuwapa kaya maskini ambazo zinaishi katika maeneo ya hayo.

Kazi hii ya upimaji wa maeneo na kutoa hati kwa wananchi ni katika mpango wa nchi wa matumizi bora ya ardhi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa Morogoro kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi na utahusisha nchi nzima kwa wapimaji wa ardhi kutumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo kwa kiasi kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila mtu kumiliki kipande cha eneo lake.

Lukuvi alisema kuwa wakati wa kampeni mwaka 2015,Rais Dkt. John Magufuli alihaidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa, na kwa miaka mitano takribani vijiji 7,500  vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo na kila mwaka vitapimwa vijiji 1,500 na kutoa hati. Alisema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza.
    Mzee Ali Juma mkazi wa kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kumuwezesha kupata hati ya kumuliki ardhi yake ambayo amekuwa nayo kwa miaka mingi bila kupewa hati hiyo, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Dkt. Stephen Nindi anayemsaidia kwa kumshika mkono.
  Bi. Zaina Hussein mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
  Bibi. Magret Hamis mkazi wa kijiji cha Hembeti akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
  Baadhi wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakiwa hati zao za kumuliki ardhi mbele Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo  na kuwataka wahakikishe wanazitumia hati miliki hizo za kimila kwa kujiletea maendeleo.
 Baadhi wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro Bwana Limbena Madela akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwezesha wakazi wa kijiji chake kupata hati miliki hizo za kimila.

Monday, February 6, 2017

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA WAKIMBIZIWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya(kushoto), alipofika ofisini kwake  kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa  katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala  ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo  jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) ,baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala  ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka wizarani hapo, Harrison Mseke.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...