Saturday, February 18, 2017

MSAGA SUMU AONGOZA SINGELI MICHANO MCHIZI WANGU CONCERT

 Umati wa watu waliofurika katika uwanja wa Mwembe yanga katika Tamasha la mchiz wangu Concert
 Msaga sumu akitumbuiza mbele yamashabiki wa Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam Katika Tamasha la Mchizi Wangu Concert
 Majid Migoma akitumbuiza katika Tamashalamchiz wangu Concert


 Msaga sumuakiendelea kuwapa raha wakazi wa Temeke
 Wacheza shoo muziki wasingelei wakifanya yao jukwaani
Dula Makabila akitumbuiza mbele ya wakazi wa Temeke Mwembeyanga

Wednesday, February 15, 2017

TAKUKURU YAWABURUZA MAHAKAMANI WATUMISHI WA WIZARA YA ELIMU MANISPAA YA ILALA

 Watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha wakifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
  
Na Karama Kenyunko
Watumishi  wanne wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi akiwemo Mkurugenzi na Mhasibu wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwana mashtaka saba yakiwemo ya ubadhirifu na ufujaji wa fedha na kuisababishia wizara hasara ya zaidi ya Milioni 41.
Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Emmanuel Jacob aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Mkurugenzi  Bakari Issa, Mhasibu Emmanuel Mayuma, Mkurugenzi  Msaidizi Hellen Lihawa na Mhasibu Msaidizi Mbarouk Dachi.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri ilidaiwa kuwa washtakiwa hao kwa makusudi na kwa nia ya kudanganya walitumia malipo ya tarehe 16 Julai 2014 kwa jina la Emanuel Mayuma ambayo ilikuwa na taarifa ya uongo kuonyesha kuwa zaidi ya sh. Milioni 18.4 zilikuwa ni malipo kwa ajili wanafunzi waliohudhuria  mafunzo ya michezo  yaliyokuwa yamedhaminiwa na  British Council huku wakijua siyo kweli.
Aidha watumishi hao wanadaiwa kufanya ubadhirifu na ufujaji wa fedha kati ya Agosti 30 na Septemba 10 mwaka 2014 na kujipatia kiasi hicho cha milioni 18 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya mpango wa walimu kwa mafunzo ya kadi za michezo  zilizofadhiliwa na British Council.
Mhasibu Mayuma anadaiwa peke yake kuwa, kati ya Agosti 10 na Septemba 2014 wizarani hapo alitumia vibaya kiasi cha shilingi milioni 31.7 alizokuwa amekabidhiwa kwa ajili ya kugaramia mpango wa matumizi ya kadi za michezo.
Katika hatua nyingine watuhumiwa hao wote wanadaiwa kushindwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababisha wizara ya Elimu hasara  zaidi ya shilingi milioni 18.4/- wakati Mhasibu Mayuma aliisababishia wizara hiyo hasara ya shilingi milioni 41.2.
Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka na wako nje baada ya kuweka dhamana ya shilingi milioni 50 kila mmoja na kuleta wadhamini wawili wa uhakika. Aidha washtakiwa hao hawaruhusiwi kusafiri nje ya  Dar es Salaam bila kupata kibali cha mahakama.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 1, upelelezi bado haujakamilika.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI JUU WATANZANIA WALIOFUKUZWA MSUMBIJINa Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wizara ya mambo ye nje na ushirikiano wa kikanda ametoa ufafanuzi juu ya tatizo la watanzania waliopo Msumbiji wanaokabiliwa na changamoto ya kurudishwa nyumbani.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda,Dk Susan Kolimba amesema kuwa amepokea taarifa za kukamatwa na kufukuzwa kwa raia wa Tanzania waliokuwa wakiishi katika mji wa Monte Puez ulio Cabo Delgado, Jamhuri ya Msumbiji.
                                        
Na kuweka wazi kuwa Serikali ya Msumbiji imekiri kuwepo kwa operesheni maalum ya kuwakamata na kuwarudisha raia wa nchi za kigeni wanaoishi katika mji huo bila kufuata Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo. Aidha, Serikali hiyo imetaarifu kwamba, zoezi hilo limeanzia mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

“ Kufuatia hali hiyo, Ubalozi weti nchini Msumbiji upo eneo la tukio ili kufuatilia suala hili na kujionea hali halisi. Aidha, unaendelea kufanya mawasiliano ya Kidiplomasia na Serikali ya Msumbiji ili kuhakikisha usalama wa Watanzania na mali zao. Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Kuanzia zoezi hilo lilipoanza, Raia wa Tanzania wapatao 132 wamesharudishwa nchini. Tarehe 11/02/2017 walirejeshwa raia 58. Tarehe 14/02/2017 wamerejeshwa raia 24 na leo tarehe 15/02/2017 wamesharejeshwa raia 50 ”amesema Naibu Waziri.

Ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahakikishia Watanzania kuwa uhusiano kati ya Tanzania na jirani yetu Msumbiji ni mzuri. Hivi karibuni mwezi wa Desemba 2016, Tanzania na Msumbiji zilifanya mkutano wa ujirani mwema uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa Pemba ulio Cabo Delgado uliainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo masuala ya biashara na uhamiaji.

NAPE KUONGOZA BONANZA LA WANHABARI FEB18

 Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akizungumza juu ya Bonanza hilo
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hiloNa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa habari Sanaa ,utamaduni na Michezo , Nape Nnauye anataraji kuongoza  Bonanza la mazoezi na upimaji afya February 18 mwaka huu ulionadaliwa na Chama cha maofisa mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na jukwaa la wahariri Tanzania na Dar es Salaam City Press Club.

  

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msemaji wa chama TAGCO, Abel Ngapemba ametaja kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya kama ilivyozoeleka kwa kuunga mkono kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rias Mama Samia Suluhu Hassan.
“washiriki wa bonanza hili ni pamoja na maofisa mawasiliano wa Serikali na wasekta binafsi ,Wahariri , Wahandishi wa habari na Bloggers na wananchi kwa ujumla kwa kuongozwa na Waziri Nape Nnauye na kuhudhuliwa na viongozi wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto” amesema  Abel.

Ametaja kuwa mbali ya mazoezi tasisi zitakazo shiriki kutoa huduma siku hiyo ni pamoja na Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road,Hospitali ya Sanitas,CCP Medicine Kinyerezi na Mfuko w Bima ya Afya (NHIF), Chama cha madaktari wa meno Tanzaniana tasisi ya wagonjwa wa mifupa MOI.

Abel ametoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habar, waandishi wa habari , Bloggersna maofisa mawasiliano Serikalini, mashirika binafsi na tasisi za kimataifa kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo.

Tuesday, February 14, 2017

STARTIMES YASHEHEREKEA VALENTINE NA WATEJA

 Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
 Bwana na Bibi Alex wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi kampuni ya Star Times Tanzania
 Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick
 Wafanyakazi wa Star Times Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  wakiwa wameshika maua
 Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni Valentine's na Star Times


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa zawadi kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi hizo Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix Awino amesema Star Time inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi kupata chakula cha jioni na malazi ya Hotel ya kisasa.

“tunafurahi kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama sehemu ya upendo wetu kwao kwa kuwapa promotion na maudhui yanayoendana na wakati hivyo kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata malazi SeaScape,  Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika , Meya wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata kupumzika katika Hotel ya Morena”amesema Awino.

Kwa upande wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na Startimes, Nuezy Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja wa Star Times kupata nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama hiyo hili waweze kufurahi na wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi cha Star Times.

Amesema kuwa star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na kufurahia vipindi bomba vya kila siku.

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...