Saturday, February 25, 2017

MAWAZIRI WA ZANZIBAR WATEMBELEA WIZARA YA ARDHI KUBADILISHANA UZOEFU

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na ujumbe wa  Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
Wananchi wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.                                                                                                                                        Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MWAMBUSI AKIRI UKABAJI UMEIGHARIMU YANGAKocha msaidizi  wa yanga Juma Mwambusi akiwa na kocha mkuu wa timu hiyo George Rwandamina wakipanga jambo katika mchezo wa dhidi ya Simba.

 Na Humphrey Shao, Globu Ya Jamii
Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amekiri kuwa timu yake ilikuwa na tatizo katika eneo la ukabaji na kupelekea kuchapwa bao 2-1.

Mwambusi amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kutaja ubovu wa timu yake.
“tulianza mchezo huu vizuri lakini tatizo la ukabaji katika timu yetu ndio limetugharimu na kuwapa wapinzani wetu ushindi wa wazi ambao kila mtu ameuona” amesema Mwambusi.

Mwambusi ametaja kuwa kulikuwa hakuna sababu ya timu yao kupoteza mchezo huo kwani tayari walikuwa washatangulia kwa bao moja hivyo walikuwa na nafasi nzuri ya kupata ushndi lakini uzembe wa wachezaji wachache umeigharimu timu.
Ametaja kuwa tatizo lililowakuwa wapinzani wao la kupewa kadi Nyekundu lilikuwa zawadi tosha ya kuondoka na ushindi lakini bado wachazaji walishindwa kukaba.

MASHABIKI WAWAJAZA MANOTI MAVUGO NA KICHUYA


Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akipokea pesa kutoka kwa mashabikiw a Simba 

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Ushindi wa bao 2-1 wa klabu ya Simba dhidi ya mahasimu wao Dar es Salaam Young Africa umeweza kuwaneemesha wafungaji wa Simba, Laudit Mavugo na Shiza kichuya.

Wachezaji hao ambao waliweza kung’ara katika mchezo huo waliweza kujipatia fedha za kutosha kutoka kwa mashabiki wa mchezo huo ambao waliweza kuwatunza fedha mara baada ya mchezo huo kuisha.

Ushindi wa mchezo huo amabo umeweza kuleta furaha kubwa sana kwa washabiki na  kuamua kuwajaza manoti wachezaji hao.
Mshambuliaji wa Simba , Shiza Kichuya akiokota fedha ambazo amepewa na mashabiki

SIMBA YAILZA YANGA BAO 2-1 TAIFA

 Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni , Nape Nnauye akisalimiana na Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima.
 Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni , Nape Nnauye akisalimiana na Nahodha wa Simba Abdi Banda
 Kiungo wa kati wa Yanya Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka beki wa SimbaJanvier Bukungu
 Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka sawa mpira mbele ya beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondan
 Golkipa wa Yanga Deogratius Munishi akiokoampira uliopigwa na mshambualiaji wa Simba Laudit Mavugo
 Kiungo wa Simba Said Ndemla akiwania mpira na kiuongo wa kati wa Yanga,Justin Zulu (Mkata umeme)
 Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib akimtoka beki wa Yanga Mwinyi Haji katika mchezo huo ambao Simba imeshinda bao 2-1
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kusawadhisha liliwekwa kimyani na mshambuliaji Laudit Mavugo
 Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akipiga mpira mbele ya beki wa Yanga , Andrew Vicent katika mchezo ambao Simba waliweza kutoka na ushindi wa bao 2-1
 Mshambuliaji wa Yanga , Obrey Chirwa akiwania mpira mbele ya kiungo wa Simba Said Ndemla
 Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka swa mpira mbele ya beki wa Yanga Mwinyi haji
 Wachezaji wa Simba wakiwa wamembeba winga wa kulia wa timu hiyo Shiza Kichuya mara baada ya kuipatia Simba bao la ushindi katika mchezo wake wa ligi kuu ya Viodacom Tanzania
 Mameneja wa timu ya Simba wakiwa wamembeba mchezaji Shiza kichuya mara baada ya kuipatia timu hiyo bao la kuongoza katika mchezo wake dhidi ya Yanga
 Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekaa kwa huzuni mara baada ya timu yao kupigwa bao 2-1 na timu ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
 Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania
 Askari wa jeshi la Zimamoto wakiwa wamembeba mtu mabaye amezimia kwa furaha mara baada ya Simba kushinda
 Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akimtoka beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondani
Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kuichapa Yanga bao 2-1 katika mchezo waligi kuu ya vodacom

Friday, February 24, 2017

14+ YAFANYA ONESHO LA WAZI VIWANJA KABURI MOJA POSTA

 Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi
 Msemaji wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
 Mchoraji Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
 Mchoraji Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
 Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo


Na  Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba tasisi za Serikali na mashirika mbalimbali  kuweza kununua kazi za Sanaa za uchoraji za  wasanii watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo aina ubora.
Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na kundi la 14 + la hapa nchini.
“Sanaa za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa hali ya juu ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa tasisi zetu za umma na ofisi za serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.
Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.

 Mchoraji Mins Mims akionyesha ufundi wake wa kuchora katika maonyesho hayo
 Mchoraji Caludia Chatanda akitoa maelezo kwa watu waliofika katika maonyesho hayo
 Mchoraji wa vibonzo Nathan Mpangala akichora mchoro wake mbele ya wadau katika maonyesho hayo ya wazi
 Nathan Mpangala akitoa somo kwa wadau wakifika katika maonyesho hayo
 Mchoraji kutoka Vipaji House akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo
wanafunzi wakitazama kwa makini moja ya michoro iliyochorwa na wasanii wa kundi la 14+

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AENDESHA KIKAO CHA IDARA ZA WIZARA HIYO JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiongoza kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam

Kamishna wa Jeshi la Magereza Divisheni ya Utawala na Fedha,Gaston Sanga, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa  kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna  wa Fedha Jeshi la Polisi  Albert Nyamuhanga.

Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Afisa Tawala wa Idara hiyo,Jenita  Ndone(Kulia), wakifuatilia kwa makini kikao cha ndani cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Regasira (hayupo pichani) .Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.


Maafisa kutoka idara ya Uhamiaji wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa  kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara. Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...