Saturday, March 4, 2017

Msaada wakuu --MZEE ALINANOSWE ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE WALIOPOTEZANA MIAKA KUMI ILIYOPITA

 Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake  baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.
Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
 
Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.
Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,
Namba

0713 562954 Augustino Michael
0789682901 Lister Godfrey
0789421644 Frank Michael
0718 528632 Frank Michael
0769 56 2954 Augustino Michael.

VINGUNGUTI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

 Naibu Meya wa Manispaa  ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa mtaa miembeni katika kikao cha kamati ya shule.
 Baadhi ya Wananchi na Wazazi wakiwa wamekaa kwa makini wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala
 Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembeni,Idaya Ndevumbili akizungumza na wazazi wa shiule hiyo
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya rangikwa kamati ya shule ya msingi miembeni


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu.

Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule msingi miembeni kata ya Vingunguti .

“lazima niwambie ukweli hili swala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka hili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto.

Kumbilamoto ametolea uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu amabapo alikuwa mapumzikoni hivi karibuni hivyo anasema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni.

Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza .

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo huo

ZIARA YA KATIBU WA KAMATI MAALUM YA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA,MHANDISI HAMAD MASAUNI VISIWANI ZANZIBAR


Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idaraya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katikaeneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu

Katibu wa Kamati Maalumya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza naMkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma(kushoto), baada ya kutembelea eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo  ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika  ambapo Katibu huyo wa NEC  ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa.


Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ally Kitole, akimuelezaKatibu wa Kamati Maalumya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni baadhi ya hatua walizochukua katika kupambana na uhalifu unaoatokea eneo la Mwanyanya Mikoroshini.Picha na Abubakari Akida

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...