Friday, March 10, 2017

UPELELEZI KESI YA KITILYA WASUBIRI USHAHIDI KUTOKA ULAYA

Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi Miss Tanzania wa Zamani  Shose Sinare  na kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika kizimba cha mahakama ya kimu mkazi kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili
 Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.

Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.
  
Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta liugha za ujanja ujanja.

“Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndaniya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilina inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo ameugiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti  kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.


aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

Maafisa wawili wa TFF waliokuwa wakituhumiwa kwa kuomba rushwa waachiwa huru

 Msaidizi wa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Juma Matandika  akitoka mahakamani Mara baada ya kukutwa hana kesi ya kujibu na kuachiwa huru.
Matandika


 Na Karama Kenyunko

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru watumishi wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandiko  baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu
Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Shahidi amesema kuwa amewaachia huru washtakiwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na kuona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda kosa.

Washtakiwa Matandika na Mecky wanatuhumiwa kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 25.

Awali ilidaiwa kuwa Februari 4 mwaka jana, washtakiwa hao wakiwa wajajiriwa wa TFF walishawishi kuomba rushwa ya kiasi hicho cha pesa kutoka kwa Salum Kulunge na Constatine Morandi ambao ni maofisa kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu Geita.

Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliomba rushwa hiyo kama kishawishi kwa TFF na Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa uamuzi dhidi ya klabu ya Mpira wa Miguu Polisi Tabora ili kuisaidia klabu ya ya Geita kupanda katika ligi kuu ya Tanzania.
  
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Shahidi alisema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka unaonesha hakuna mtu aliyeenda Takukuru kulalamika juu ya washtakiwa kuomba rushwa zaidi ya sauti ya CD kusambaa katika mitandao.

Amesema upande wa mashtaka haukuonesha kama kweli washtakiwa walitoka Geita kuja Dar Saalam.

Kuhusu sauti zilizotambuliwa za Mecky na Matandiko kupitia CD, Hakimu Shaidi amesema watu wana sauti za kufanana na hata kuigizana hivyo hauwezi kujikita kwenye ushauli kuwa ni washtakiwa wenyewe ndio wanaosikika kwenye hiyo CD.

Amesema, ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo kuacha mashakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo.

Hakimu Shahidi ameenda mbali na kueleza kuwa kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa mahakamani hapo, imedaiwa kuwa kanuni za TFF zinaeleza wazi kuwa, mchezaji akibainika kudanganya ndiye anayepaswa kuadhibiwa lakini si timu kunyang'anywa pointi.

"Hawa hawakuwa na mamlaka ya kunyang'anya pointi, hivyo wasingeshtakiwa kwa kuomba rushwa na hata kama walitenda kosa basi wangeshtakiwa na tuhuma zingine, labda utapeli", amesema.

Kutokana na upungufu wa ushahidi, Hakimu Shaidi aliwaachia huru washtakiwa kwa sababu hawana kesi ya kujibu.

Kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai.

Kaimu Mkurugenzi wa mashindano Martin Chacha Mecky akitoka mahakamani Mara baada ya kuachiwa, kwa kukutwa hapana kesi ya kujibu.

JAJI WARIOBA AZINDUA KITABU CHA KIONGOZI MWANAMKE

 Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akionyesha kitabu juu mara baada ya kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanawake ma
 Aisha Bdel na Liliani Lihundi wakifurahi mara baada ya Jaji wa Rioba kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi
 Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Wanawake waliofika katika kongamano la Wanawake na Wasichana  juu ya uongozi ndani ya Tanzania na kuzindua kitabu kinachohusu Mwanamke
 Dkt Mwele Malecela akizungumza juu ya mambo aliyojifunza wakati anagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi na kuwataka wazazi kuwa ndio waangalizi na kuwatoa hofu wasichana pindi wanapohitaji kujaribu jambo lolote lenye manufaa kwa Jamii
 Muendesha Mjadala Liliani Lihundi akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihusisha wasichana na wanawake
 Mbunge Viti Maaalum Chadema , Susan Lymo akichangia jambo juu ya uozefu wake kama mwanamke katika Bunge la Jamhuri wa muungano
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiwa na Mama Anna Abdalah wakiwasalimia wanafunzi wasichana wa chuo kiku cha Dar es Salaam ambao walifika katika kongamano hilo
Baadhi ya washiriki waliokaa Safu ya mbele katika kongamno hilo

MARY MWANJELWA AONGOZA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

 Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwa akipiga makofi wakati wa mahadhimisho ya Siku ya Wanawake mkoa wa Mbeya.
  Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwaakinyoosha mikono juu pamoja na wageni wengine wa meza kuu katika mahadhimisho ya Siku ya Wanawake Mbeya
Mbunge wa Viti Maalum Mbeya akipunga mkono kwa Wanawake wa mkoani mbeya

Thursday, March 9, 2017

CRDB YATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka  (kulia)akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwa tasisi ya Saratani ya Ocean Road.
 Baadhi ya watumishi wa Tasisi ya Saratani ya Ocean Road wakifatlia kitendo hicho cha utoaji wa Msaada kutoka benki ya CRDB
 Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto akizungumza kabla ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka benki ya CRDB
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia)akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto ,vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia)akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto kabati la kuhifadhia vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam

WLAC YATOA ELIMU JUUYA HAKI ZA MTOTO KWA WANAFUNZI WA ANANASIFU SEKONDARI

 Mwanasheria wa WLAC , Wigayi Kisandu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinondoni ananasifu juu ya umuhimu wa mtoto wa kike katika kukuza uchumi wa Tanzania na familia kwa kuweza kutambua haki zake na majukumu yake
 Kaimu Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ananasifu Fatuma Niyopa akizungumza wakati wa mkutano huo ambao umewezesha wanafunzi wa kike kujitambua juu ya haki za mwanamke
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Ananasifu wakiwa katika kikao hicho na tasisi ya Msaada wa Kisheria kwa Wanawake WLAC

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA UWANJA WA UHURUNa Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Tamasha kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama Tamasha la Pasaka sasa kufanyika katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mratibu wa Tamasha hilo Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanaj wa uhuru ndio sehemu maalum ya kuanzia Tamasha hilo jijini Dar es Salaam.

“Malengo ya tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wan chi Dkt John Pombe Magufuli  hili aendelee kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema

Ametaja kuwa tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa albamu mbili

Wednesday, March 8, 2017

JOKATE MWEGELO AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA MANZESE SEKONDARI

JOKATE MWEGELO AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA MANZESE SEKONDARI

KUMBILAMOTO AZIDI KUMWAGA MISAADA VINGUNGUTI

RAY SINA MPANGO WA KUMONYESHA MWANANGU HADHARANI

MSIKILIZE RAY JUU YA HILI

JOKATE AWATAKA WASICHANA KUJIAMINI HILI WAWEZE KUFIKIA MAFANIKIO

 Jokate Mwegelo akipima afya katika zoezi liliondeshwa shule ya sekondari Manzese jijini Dar es Salaam
 Mratibu kutoka tasisi isiyo ya kiserikali ya TAI, Edith James akizungumza na mabinti wa shule ya sekondari Manzese
 Mwanamitindo Jokate Mwegelo akizungumza na Mabinti wa shule ya Sekondari Manzese jijini Dar es Salaam juu ya kujitambua na kujiamini hili kufikia mafanikio


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mwanamitindo maharufu nchini,Jokate Mwegelo amewataka watoto kike kujiamini hili waweze kufikia mafanikio katika maisha hayo kwa kuweka juhudi katika elimu.

Jokate amesema hayo leo katika mahadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam

“nataka niwaambie watoto wa manzese sekondari siri kubwa ya mafanikio ni kujiamini lakini usijiamini katika ujinga hivyo mnapaswa kujiamini katika vitu vya msingi ambavyo viatweza kusaidia jamii yetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema Jokate.

Kwa upande wake program meneja wa TAI, Edith james amesema kuwa umefika wakati wa wanawake kujiamini hasa kwa kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi na usafi wa mwili kwa ujumla hasa wakati wanapokuwa katika siku zao.

Amesema kuwa tasisi ya TAI imekuwa katika kampeni kwa zaidi ya shule kumi za mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike waweze kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi.

 Picha kwa juu ikionyesha namna Jokate alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese
 Jokate akiwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese
 Daktari kutoka tasisi ya TAHMEF, Victoria Joseph  akitoa maelekezo juu ya tasisi yao inavyotoa huduma kwa watoto wa kike mashuleni
 Joakate Mwegelo akikabidhi taulo za kike kwa mmoja wanafunzi wa sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kampuni ya Kays Hygiene product Malik Mtui akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...