Thursday, March 16, 2017

MARAIS WASTAAFU WAONGOZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU SIR GEORGE KAHAMA

 Mke wa Marehemu Sir Georeg Kahma, Janeth Kahama akiaga mwili wa Mumewe katika ukumbi Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu , Benjamini Mkapa  akitoa pole kwa watoto wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri wa Habari Sanaa  Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Spika Mstaafu wa Bunge , Anna Makinda akitoa pole kwa wanafamilia ya Marehemu Sir George Kahama.
 Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni , Freeman Mbowe  akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Mtoto wa Marehemu Sir George Kahama  akiaga mwili wa babake
 Sehemu ya ndugu wa familia wakiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa akitoa pole kwa watoto Marehemu Sir George Kahamakatika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Mawaziri wakuu wa Staafu pamoja na wake zao wakiwa katika msiba huo kwa uhuzuni
 Marais Wastaafu na wake zao wakiwa wanatafakari  kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
Mawaziri wakuu wastaafu wakitafakari jambo kabla ya kuaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama  katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Wednesday, March 15, 2017

TEMEKE STERIO SASA KUPEWA MZABUNI

 Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Faysal Salum akitoa maagizo ya sokol Sterio kupewa mzabuni mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mafunzo kutoka kwa watendaji wa Manispaa ya Ilala
 Baadhi ya Madiwani na Watendaji kutoka Temeke  wakisikiliza kwa makini  maelekezo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke.
 Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika kikao hicho cha madiwani na maofisa masoko kutoka Temeke na Ilala.


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
 Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, ameagiza kuanzia sasa Soko la Matunda la Temeke Sterio kupewa mzabuni wa ukusanyaji mapato hili kuongeza ufanisi katika mapato ya Halmashauri.
Salum ametoa agizo hilo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujifunza kazi kwa maofisa masoko wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na Madiwani ambao walikwenda kujifunza namna jinsi gani halmashauri ya Ilala imeweza kufanikiwa kupata mapato kupitia masoko kupewa wazabuni kukusanya masoko.
“lazima niwaambie ukweli kuwa soko hili tunalipeleka kwa wazabuni hili tuweze kupata mapato, aiwezekani kukusanya mapato milioni 50 kwa mwezi na gaharama za uzalishaji kuwa juu ya hiyo pesa hivyo hapa akuna namna lazima tuligawe hili soko hili tuweze kupata faida” amesema Salum.
Amesema kuwa kwa ziadi ya miaka mitano soko hilo lilikuwa likiendeshwa kwa hasara kwa fedha kutoka Halmashauri hivyo kuanzia sasa imefikia tamati .
Kwa upande wake Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wanasiasa kuacha kukumbatia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwaletea jeuri maofisa masoko na wakusanya ushuru kwa sababu wanafahamiana na viongozi.
Ametaja kuwa kama viongozi wa juu watakuwa mstari wa mbele kusimamia makusanyo bila ya kumwangalia mtu wataweza kufanikiwa katika mfumo huo wa ukusanyaji kupitia mzabuni ambao una manufaa makubwa sana kwa Halmashauri.

Tuesday, March 14, 2017

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWAOMBA VIONGOZI WA DINI NA MILA KUWAEPUSHA WANANCHI NA IMANI ZA KISHIRIKINA NA KUFUFUA WATU

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na viongozi wa Dni, wa mitaa na wa mila katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mkapa leo jijini mbeya
 Baadhi ya viongozi wa dini na serikali za mitaa na mila wakiwa katika ukumbi wa mkapa kumsikiliza mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makalla watatu kutoka shoto pamoja na mkuu wa wilaya ya mbeya mh.William Ntinika wa kwanza kushoto katika picha ya Pamoja na viongozi wa Dini mkoa wa Mbeya.Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala  aitisha kikao na viongozi Dini na mila kwaomba msaada wa kukemea vitendo vya kishirikina katika mkoa huo.
Makala amesema hayo katika kikao chake na Viongozi wa Dini Mila na wenyeviti wa mitaa na vijiji katika mkoa wa Mbeya.

" matukio ya watu kufukua maiti au kutozika kwa imani ya kuwafuafua  hayapaswi kuachwa yaendelee , bibilia na Quruan imeandikwa kuna kufufuliwa, kuna kiama ,kuna pepo ni baada ya kufa nawaomba  mnisaidie   kutoa Elimu na mafundisho yenye kuondosha matukio hayo" Aamesema Makala.

 Makala awaomba pia kusaidia serikali katika mapambano ya Dawa ya Kulevya kwa kutoa Elimu na hamasa ya kuelimisha madhara ya dawa ya kulevya.

Amesema Mbeya itangazwe kwa sifa nzuri kama Mkoa unaotegemewa kwa uzalishali wa Chakula, Mkoa wa tatu kitaifa kuchangia pato la Taifa na ni Mkoa unapiga hatua kubwa kimaendeleo

MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua ilinyosha jana
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mt Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivuka moja ya sehemu ambazo zina maji katika bonde la mto Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha Dar es Salaam na kuleta madhara kwa wakazi hao
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza katika maeneo ya bonde la Mto Msimbazi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuza maembe.
Na Ripota wa globu ya jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Makonda amesema ahayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa kaitembelea maeneo hayo.

"la kwanza katika ngazi ya mkoa kulingana na utabiri wa hali mvua zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50 maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili usema kinga ni bora kuliko tiba "Aamesema Makonda

amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia hili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi hili kupunguza Madhara.

amesema hayo yanayo onekana leo ni tabia mabaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunavyoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi la pili tunaambiwa tuhakikishe kuwa atuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga

ametaja kuwa maji hayo mengi utokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo mkoa wa pwani hasa katika eneo la kisarawe na kuhitaji kupita katika mto huu hivyo ukijengwa ndipo madhara haya ayataonekana.

Monday, March 13, 2017

KUMBILAMOTO AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI NA GETI KWA AJILI YA KISIMA CHA MAJI

 J.tatu ya leo nimeituma ktk shule ya secondary vingunguti nitoe shukrani za dhati kwa ubalozi wa Kuwait Wametuchimbia kisima ilikuwa ni changamoto kubwa ktk shule hii wanafunzi walikuwa wanakwenda mitaani kutafuta maji jukumu walilonipa ni kumalizia geti lijengwe ktk chumba kinachokaa pump ya kisima kwa usalama ahadi hiyo nimetimiza leo na mafundi wanaendelea na ujenzi tunajiandaa kwa uzinduzi dua zenu.tunaelekea ktk "nchi ya ahadi"


Mifuko ya saruji ilitolewa na Mh Omary Kumbilamoto

RC MAKONDA AKABIDHIWA BARABARA KURASINI LEO JIJINI


Na Chalila Kibuda, Globu ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika  katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa.
 Makonda ameyasema hayo leo wakati wa akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja ,amesema  barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.
Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.
"Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sta haijapita" amesema Makonda .


Amesema barabara imejengwa na kampuni ya kizalendo ya Grant Tech Company ya jijini Dar es Salaam na maombi ya barabara ni miwili miezi miwili iliyopita lakini imekamilika kwa muda mwafaka .
Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile.
Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza bugudha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta haza hata kwa vyombo vyao vya usafiri.
Amesema amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni  ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia
Mkandarasi huyo (Grant tech), Masito Mwasingo amesema kuwa wamefanya ujenzi kwa muda mwafaka kutokana umuhimu na kuunga kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.
mwisho

Sunday, March 12, 2017

WANANCHI WA MKURANGA WAPATA HUDUMA ZA VIPIMO VYA AFYA ZAO BURE

Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa upimaji wa afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga leo.
  Muuguzi Mariam Adamu akipima kipimo cha Sukari na Msukumo wa Damu
 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Wananchi wa Mkuranga wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapokutwa kuweza kutibu kwa wakati mwafaka.

Akizungumza katika upimaji wa Afya huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo amesema kuwa katika dunia ya sasa jamii inawajibu wa kupima afya kujua ana tatizo au hana ili kuweza kuchukua hatua pamoja na kujinga na magonjwa mbalimbali yanatokana na mfumo wa maisha.

Othman amesema kuwa huduma hiyo itatolewa  kwa wa wananchi wa Mkuranga, Vikindu, Mwanambaya, Mbagala na maeneo  mengine yaliyo karibu.

Amesema wamechagua Wilaya hiyo kutokana watu wengi wanashindwa kuifikia na kuona kwa taasisi hiyo inawajibu wa kupima afya za wananchi ha.

Aidha amesema kuwa watu wengine ambao wanauwezo wajitokeze katika kutoa huduma ya upimaji ili waweze kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na mfumo wa maisha.

Amesema tangu jana walipoanza kupima watu zaidi ya 500 wamwjitokeza kupima na mwitikio umekuwa  mkubwa wa kuweza kuvuka malengo ya upimaji huo.

Huduma ya vipimo walivyotoa ni Msukumo wa Damu (BP), Sukari , Unene na Urefu kuendana sawa na mwili (BMI) Ushauri Nasaha  na Upimaji wa VVU,Utafiti wa Saratani ya matiti pamoja na utafiti wa Saratani ya Kizazi.
 Wananchi wakisubiri huduma ya vipimo vinavyotolewa na Taasisi ya Ibun Jazar leo.
WATANGAZAJI WA MICHEZO WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI

 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo na Warsha ya Wanahabari za michezo  juu ya maadili ya utangazaji kwenye radio na Televisheni na kuzingatia taaluma
 Mwandishi wa habari mkongwe kutoka kituo cha Azam Televisheni , Baruani Muhuza akitoa somo kwa wanahabari hao walifika katika mkutano huo juu ya umuhumu wa weledi wa taaluma
 Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Superdoll, Jamal Baiser akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watangazaji wa waandishi wa habari za michezo
 Evance Mhando akichangia mada katika mkutano huo ambao uliweza kuwajenga watangazaji kufuata weledi
 Mwalimu Alex Kashasha akitoa mada juu ya kuwaleta wasikilizaji na watazamaji kuwa sehemu ya watu waliopo uwanjani pasipo kusababisha mfarakano wa moyo na kulaumu marefa na wachezaji kutokana na aina ya utangazaji tulionao sasa
 Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo

 Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo
 Msemaji wa shirikisho la Soka nchini ,Alfred Lucas Mapunda akizungumza na juu ya watangazaji kusomana kufuata kanuni za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na mashindano mengine hili kuweza kuwa na majibu sahii pindi wanapokuwa wanatangaza mpira
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Superdol , Jamal Baiser akikabidhi zawadi kwa  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari ambaye alimwakilisha waziri wa haabri Vijana utamaduni na Michezo Nape Nnauye

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...