Saturday, March 25, 2017

MWANAMAMA MTAANI AKIWA ANASUKUMA ROLI KUBWA LA TANKI LA MAFUTA

 Mwanadada akiwa katika usukani wa Roli la Mafuta kama alivyokutwa na Kamera yetu katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam leo
 Mwanadada huyo akiendelea kuchanja mbuaga katika eneo la Manzese Argentina
 Picha kwa nyuma ikionyesha roli hilo aina ya Scania lenye tanki la mafutra nyuma kampuni ya Lke Oil
Mwana dada huyo akiwa makini na kazi yake kama anavyoonekana pichani

TASWIRA YA BARABARANI LEO ASUBUHI JIJINI DAR ES SALAAM

 Askari wa Usalama Barabarani , akiwa anazungumza na mmoja wa Dereva aliyemsimamisha katika kituo cha Daladala cha Kimara Butcher
 Mabasi ya Mwendo kasi yakiwa katika foleni ya Mataa ya Ubungo eneo ambalo linataraji kujengwa barabara za juu hivyo barabara hizo zikijengwa hakutakuwa na haja ya taa za eneo hilo kuendelea kuyasimamisha mabasi hayo hivyo safari zitakuwa zinatumia muda mchache zaidi
 Kikundi cha Askari wa usalama barabarani wakiwa wamesimama katikabarabara ya morogoro neo la Jangwani
Askari wa doria wakiwa wamekamata pikipiki za waendesha bodaboda na kuzipakia kwenye gari kama walivyonaswa katika makutano ya barabara ya kalenga na Morogoro eneo la Fire Jijini Dar es Salaam.

Friday, March 24, 2017

MDAU KUMBILAMOTO ATEMBELEA MICHUZI MEDIA GROUP

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisalimiana na Msimamizi wa Chumba cha Habari , Carthbet  Kajuna wakati alipotembelea ofsi za MMG leo.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, akisalimina na Mhandishi Mwandamizi na Msimamizi wa Habari za Mahakamani Karama Kenyunko wakati alipofanya ziara katika ofisi za MMG.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto Akiwa ndani ya ofisi ya MMG
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto,Akifurahi jambo na Mwandishi Mwandamizi wa Michuzi Blog Chalila Kibuda
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, Akisalimiana na Mkurugenzi wa Michuzi TV , Karim Michuzi wakati alipofanya ziara ya kutembelea chumba cha habri cha Michuzi Media Group

MKUU WA MKOA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KTK MAENEO YAO

 Rc Makalla akizungumza na wananchi WA kata ya mwakibete jijini mbeya

Na Fadhili Atick Globu ya Jamii Mbeya

 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi mtaa wa Shewa kata ya Mwakibete mkoanai Mbeya na kuwataka wananchi kushirikiana na serikali katika kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili.

Makala ambaye ametembelea Shule ya Msingi Shewa na kushuhudia msongamano wa wanafunzi
 amepongeza wananchi kwa kushiriki ujenzi wa madarasa kupunguza msongamano wa wanafunzi, halmashauri ya jiji la Mbeya wachangia shilingi 6.3m kuunga Mkono jitihada za wananchi.

Makala ameahidi kufuatilia kwa Karibu ujenzi wa madarasa mpaka yakamilike kwani wananchi wachukizwa na watu wachache wanapita kushawishi wananchi wasichangie

Makala amewaonya wote wanaoshawishi wananchi kutochangia Maendeleo kuacha tabia hiyo mara moja katika  na kuamua kuonyesha mfano wa kuchangia milioni moja katika ujenzi wa choo cha Shule msingi shewa

Pia ameagiza Tanesco na Mamlaka ya Maji kushughulikia haraka matatizo ya  Umeme na Maji katika mkoa wa Mbeya hili kupunguza kero kwa Wananchi.
Moja kati ya Wakazi WA shewa kata ya mwakibete wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya.


Akishangazwa na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi mwakibete ambapo idadi ilionyesha wanafunzi ni wengi kuliko madarasa

BALOZI WA KOREA AKABIDHI MAKTABA YA KISASA KWA SERIKALI YA TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa , Audax Mabula akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika Makumbusho ya Taifa.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akizungumza kabla ya uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa katika ukumbi wa Makumbusho ya taiafa kwa msaada wa Serikali ya watu wa Korea.
 Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young akizungumza kabla ya uzinduzi wa wa Maktaba ya kisasa ambayo imetolewa na Serikali ya korea


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Serikali ya Korea kupitia mradi wa ''Thank you Small Ribray program'' leo imekabdidhi Vifaa na kuzindua maktaba ndogo ya kisasa katika ofisi za makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana balozi wa Korea nchini Song Geum Young amesema kuwa serikali yake licha ya kusaidia serikali katika miradi mingi lakini kwa sasa wameamua kusaidia katika kuwawezesha watoto kupata elimu inayoendana na wakati.

"sisi kama korea tunahamini kuwa ukimpa mtoto elimu umeweza kumpa maishaya kesho hivyo vifaa hivi vitaweza kuwasaidia katika kukuza taaluma yao " amesema Balozi

balozi ametoa wito kwa wazazi kuwaleta watoto waweze kutumia maktaba hiyo kwa kuwaleta  watoto wao waweze kutumia sehemu hiyo kwa ajili kukuza taaluma yao .


 Baadhi ya wadau walioshiriki tukio hilo
 Viongozi mbalimbali akiwemo na balozi mteule wa korea wakifatia hotuba ya balozi
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakishuhudia tukio hilo
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na  Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa wakikata utepekuashiria uzinduzihuo
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo, akikabidhi vitabu kwa Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah
 Mwenyekiti wa bodi ya Makumbusho ya Taifa , Mama Anna Abdalah akizungumza na waandishi wa habari
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakitumia baadhi ya vifaa vilivyopo katika Maktaba ya Kisasa ndani ya ukumbi huo wa makumbusho ya Taifa
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na  Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young wakipata maelekezo jinsi ya namna vifaa vya kielektronic vinavyofanya kazi katikakutoa elimu kwa watoto ndani ya maktaba hiyo ambayo imefadhiliwa na serikali ya Korea

Picha ya pamoja ya  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Leonard Akwilapo akiwa na  Balozi wa Korea nchini , Song Geum Young na Mama Anna Abdalah  wageni waalikwa wengine waliohudhuria katika hafla hiyo 

Thursday, March 23, 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MRADI WA UJENZI -OFISI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DAR ES SALAAM


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wakwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo  leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WIKI YA UTAMADUNI WA CHINA YAZINDULIWA QUALITY CENTRE

 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akitoa Maelezo kutoka kwa Waandishi wa habari kutoka nchini China
Wageni wakisaini kitabu kabla ya kuingia katika ukumbi wa Quality Centre
 Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Star Times Tanzania ,Juma Sharobaro akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari
 Aliyekuwa Waziri wa habari Sanaa utamaduni na Michezo Nape Nnauye akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Filamu ya Jamhuri ya watu wa China.
 Watu mbalimbali wakifatilia Sinema katika kumbi wa Quality Centre wakati wa uzinduzi wa wiki ya utamaduni wa china
 Baadhi ya wasanii wa filamu hapa nchini wakifatilia tukio hilo
Katibu mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China(CPC),Mh Guo Jinlong

Wednesday, March 22, 2017

KUMBILAMOTO AKABIDHI SARUJI NA MAKOPO YA RANGI SHULE YA MSINGI KOMBO KATA YA VINGUNGUTI

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa Shule ya Msingi Kombo kata ya  Vingunguti  mara kukabidhi mifuko ya Saruji na Rangi kwa ajili ya Shule hiyo.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi Kombo kata ya Vingunguti wakuwa wamekaa Darasani kumsubiri mwalimu
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya Rangi na mifuko ya Saruji kwa Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kombo,Stela Mhando
Wanafunzi wakiwa wameshika makopo ya Rangi wakifurahi kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa makopo ya Rangi na Diwani wa Vingunguti

KUMBILAMOTO AKABIDHI MIFUKO YA SARUJI KWA SHULE YA MSINGI KOMBO

MBEZI LUIS WARIDHIA KUPIMIWA MAENEO YAO.


Image may contain: one or more people and outdoorNA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM
WANANCHI zaidi ya 300 waishio katika mtaa wa Mbezi Luis, uliopo Kata ya Mbezi Luis, Jimbo la Kibamba jijini hapa, wameridhia kupimiwa maeneo yao wakati wowote kuanzia sasa.
Mwenyekiti wa Kata hiyo, James Isdore (Chadema) amesema hayo katika taarifa yake aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa facebook.
Alisema kikao cha maridhiano hayo kilifanyika jumamosi ya Machi 18, mwaka huu ambapo jumla ya wananchi waliohudhuria na kutia saini walikuwa 322, ambao hawakuweka saini walikuwa 49, waliotoa hudhuru walikuwa 18 na kwamba jumla yao walikuwa 389.
“Tulipata wageni watano akiwamo daktari mmoja kutoka kituo cha afya Mbezi, wawakilishi wawili  kutoka kampuni ya Geoid geomatics Consultant enterprises na wawakilishi wawili kutoka TPB Bank,” alisema.
Kuhusu upimaji wa viwanja alisema, mkutano huo uliipitisha kampuni ya GEOID GEOMATICS CONSULTANT ENTERPRISES kufanya upimaji katika mtaa huo.
“Mkutano uliunda kamati ya watu saba kusimamia upimaji na kuipatia hadidu za rejea ikiwemo kufungua akaunti benk yenye jina #UPIMAJI_WA_VIWANJA_LUIS. mapema ili wananchi waanze kuingiza fedha.
“Mkutano ulikubaliana endapo vitapimwa viwanja 1000 na zaidi gharama itakuwa 180,000/- ambayo italipwa kwa awamu tatu, elfu sitini 60 kila awamu. Wenye viwanja zaidi ya kimoja kwenye eneo moja kila kiwanja kinachoongezeka kitalipiwa 100,000 1 pekee badala ya 800,000,” alisema.
Isidore aliongeza “Mkutano uliazimia fedha zitakuwa chini ya kamati na kamati italipa fedha baada ya kuridhika na kazi iliyofanywa na kampuni husika. Sh. 60,000 itapaswa kulipwa ndani ya wiki mbili baada ya kufunguliwa Akaunti na ambaye hatalipa kwa wakati hatapimiwa. Jina na namba ya Akaunti zitatumwa kupitia SMS na kubandikwa Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Luis.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...