Friday, March 31, 2017

KIONGOZI WA BAPS DUNIANI AKUTANA NA WAUMINI WA DINI HIYO TANZANIA

 Kiongozi mkuu wa dhehebu la dini ya hindu Swaminarayan Duniani MUHANSOMI MUHARAJI akitoa bara kwa moja ya mtoto wa mmoja wa Dhehebu hilo nchini
 Waumini wa Dgehebu la dini ya hindu Swaminarayan wakiwa katika maombi
 Rasi Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi akisalimiana na kiongoiz wa dini ya hindu Swaminarayan Muhanson Muharaji katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 kiongoiz wa dini ya hindu Swaminarayan Muhanson Muharaji akitoa baraka kwa Mwenyekiti wa Baps nchini,Subhashbhai Patel 
  kiongoiz wa dini ya hindu Swaminarayan Muhanson Muharaji akitoa baraka Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam jana
 Vikundi vikitoa burudani wakati wa mkutano huo wa dhehebu la Baps

 watu wakishuka ngazi kutoka katika ukumbi wa Mwalimu nyerere
 Azim Dewji akipokea baraka kutoka kwa kiongozi huyo

Wednesday, March 29, 2017

JAJI WARIOBA AONGOZA WASOMI KUJADILI MAENDELEO YA VIWANDA

 Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akitoa mada katika mdahalo ulioandaliwa na REPOA juu ya mapinduzi ya Viwanda
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Profesa Adolf Mkenda akitoa ufafnuzi juu ya nini kifanyike katika kufikia malengo ya mapinduzi ya Viwanda nchini
 Mzee Butiku akifatilia mjadalahuo ambao ulikuwa wa aina yake
 Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB nchini , Charles Kimei akizungumza namna mabenki yanavyoweza kutoa mchango mkubwa katika mapinduzi ya Viwanda nchini wakati wa mjadala ulioandaliwa na REPOA juu ya nini kifanyike kuelekea mapinduzi ya Viwanda kwa kushirikisha Tasisi
 Waziri wa Fedha Mstaafu wa awamu ya nne ,Bazili Mramba akizungumzia juu ya nini kifanyike katika serikali kuu hili tuweze kufanikiwa katika maendeleo ya Viwanda
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Profesa Adolf Mkenda akiwa na baadhi ya washiriki mara baada ya kumalizika kwa mjadala huo

RC Simiyu amaliza mgogoro wa wanakijiji na wawekezajiMkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Meatu
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo. Mwekezaji huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka, mkataba wa kumiliki ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji hivyo kiasi cha kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao wamekuwa wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji huyo.
Hata hivyo, chanzo halisi cha mgogoro huo kimegundulika kuwa ni viongozi wa baadhi ya vijiji ambao wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi huku wakisambaza taarifa za upotoshaji juu ya mwekezaji huyo na kujenga chuki kwa wananchi. Vijiji vinavyounda WMA ya Makao ni pamoja na Makao, Iramba ndogo, Sapa, Mwangudo, Jinamo, Lukale, Mbushi, Mwabagimu na Sunga.
Baadhi ya viongozi hao wa vijiji pia wamekuwa wakisambaza taarifa potofu kwa wananchi kwamba Mkuu huyo wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Meatu wamehongwa na mwekezaji ili kuwakandamiza wananchi, jambo lililothibitika kuwa si la kweli.
Kutokana na mgogoro huo kuzidi kuota mizizi huku uongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu nao ukichukua upande, Mtaka alilazimika kuitisha kikao cha usuluhishi kilichoshirikisha wadau wote wakiwamo Kamati ya Siasa ya CCM mkoa na wilaya, viongozi na watendaji wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya, viongozi wa vijiji tisa vinavyounda WMA Makao, mwekezaji na wadau wengine akiwamo Mbunge wa Meatu na Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa, Mtaka aliwakemea viongozi wanaoeneza taarifa potofu wilayani humo na kusababisha shughuli za maendeleo kukwama huku akiahidi kuwachukulia hatua zinazostahili viongozi wa namna hiyo.
“Katika masuala ya maendeleo ya wananchi sina mzaha. Nipo tayari kuwa kiongozi unpopular (asiyependwa) ili mradi shughuli za maendeleo za wananchi zinaenda mbele.
“Mgogoro na Mwiba umekuwa kama mkuki mnaojichoma wenyewe kila siku kwa sababu wenyewe ndiyo mlioingia mikataba na mwekezaji wakati sisi hatukuwapo na wala hatuna maslahi yoyote binafsi hivyo acheni maneno maneno, kaeni chini mzungumze tusonge mbele,” alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
“Mmefikisha malalamiko, tena kwa maandishi hadi kwa Waziri Mkuu lakini uhalisia ni kuwa mengi mliyopeleka hayana ukweli, ni hisia na mengine ni fitna tu. Sasa wekeni kila kitu hadharani hapa, tumalize suala hili leo na tujikite zaidi katika mambo ya maendeleo,” alisema.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk Titus Kamani akizungumza katika kikao cha usuluhishi baina ya wananchi wa Meatu na Mwekezaji wa Mwiba Holdings kilichofanyika mjini Mwanhuzi mwishoni mwa wiaki.

Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Kuhusu mgogoro wa mpaka hasa katika kijiji cha Buhongoja ambako alama ya mpaka yenye namba 314 inadaiwa kusogezwa kinyemela kwa umbali wa kilomita 10, Mkuu huyo wa mkoa alizitaka pande zinazohusika kukutana na kutatua tatizo hilo kwa kurejea katika eneo la awali bila ya mikwaruzano yoyote. Aliamuru pia pande zinazohusika katika suala la mkataba wa umiliki wa ardhi,kukaa meza moja na kuacha mambo ya kukimbilia kwa wasuluhishi ambao wamekuwa wakidai fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa maendeleo ya vijiji au wilaya ya Meatu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini aliahidi kupeleka wataalam watatu watakaosaidiana kutatua mgogoro huo wa umiliki wa ardhi watakaosaidiana na wake wa wilaya ili kutatua suala hilo ndani ya wiki mbili.
Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Phillipo alieleza kuwa kijiji kilazimika kupelaka suala hilo kwenye Tume ya Usuluhishi wa Migogoro Dar es Salaam ambako kijiji walishindwa kulipa gharama za usuluhishi huo walizotozwa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk. Titus Kamani alieleza chama hicho tawala kusikitishwa na mgogoro huo unaokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
“Ndugu zangu, sisi tunajiandaa kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kwa hiyo tunawaomba tusikubali kuingizwa katika migogoro kama hii ambayo haina tija kwa wananchi.
“Tunataka wakati wa uchaguzi utakapofika tushinde pila pressure (msukumo) yoyote na tunachotaka ni mshikamano,maelewano mazuri baina ya wadau wote ili tufanye shughuli za maendeleo kwa faida ya mkoa wetu wa Simiyu na wilaya ya Meatu,” alisisitiza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mpina Luhaga ambaye pia ni mbunge wa Kisesa wilayani Meatu alisema katikA kikao hicho kuwa mwekezaji huyo amekuwa akifuata sheria zote za nchi katika utekelezaji wa majukumu yake na ni wazi kwamba wananchi watashindwa katika madai yote wanayofungua katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro.
“Mimi nimefuatilia malalamiko haya ya wananchi serikalini na hasa Wizara ya Maliasili na Utalii na hawa jamaa wamefuata taratibu zote na wanalipa tozo zote wanazostahili kulipa hivyo tunapaswa kuwa waangalifu,” alisema.
Mkurugenzi wa Mwiba Holdings, Abdulkadir Mohamed Luta alisema kuwa Kampuni hiyo ipo tayari kukaa meza moja na kusaidia usuluhishi wa mgogoro wowote ili wajikite zaidi katika shughuli za maendeleo ya wananchi. Aliongeza kwamba kampuni hiyo ilikuwa tayari kugharamia hata suala la mkataba wa umiliki wa ardhi lililofikishwa Tume ya Usuluhishi wa Migogoro ili mradi tu suala hilo liishe na waendelee na mambo ya maendeleo
Alisema watazifanyia kazi hoja zote zilizotolewa na wananchi katika kikao hicho na kwamba sera ya kampuni hiyo ni kushirikiana na wananchi na wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa vitendo.
Mbunge wa Meatu, Salum Khamis maarufu kwa jina la Mbuzi, alisema kuwa hana mgogoro na mwekezaji yoyote lakini hatakaa kimya kutetea maslahi ya wananchi wake ambao ndio waajiri wake kila atakapoona kuna sababu ya kufanya hivyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Pius Machungwa aliahidi kuipatia kiwanja cha kujenga ofisi Kampuni ya Mwiba Holdings katika makao Makuu ya wilaya hiyo ili iwe karibu na wananchi, na kwamba watashirikiana na kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo wilayani humo.

MPANGO AFUNGUA WARSHA YA MAENDELEO YA VIWANDA ILIYOANDALIWA NA REPOA

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya umuhimu wa tasisi katika Maendeeo ya Viwanda nchini kwa watafiti iliyoandaliwa na tasisi ya REPOA
 Mkurugenzi mkuu wa REPOA Tanzania, Dr Donald Mmari akizungumza ju ya tasisi hiiyo na muhudhui ya mkutano kwa watafiti
 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakifatilia kwa makini
 Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa katika mkutano huo
 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo
 Kiongozi wa umoja wa Ulaya  Roeland Van De Geer akizungumza wakati wakati wa mkutano huo
 Profesa Lant Pritchett  kutoka chuo kikuu cha Havard Marekani akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Warsha hiyo Prof Lant ni mmoja wa watoa mada wakuu waliofika katika mkutano huo
 Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakisikiliza mada kutoka kwa Prof Lant
Waziri wa Fedha na Mipango , Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki

Tuesday, March 28, 2017

STAR TIMES YAZINDUA KAPU LA PASAKAMaeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino akizungumza waandishi wa habari

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kampuni ya kuuza Ving’amuzi ya StarTimes Tanzania inatoa pakacha la pasaka  kwa wateja wake ambapo kampuni hiyo imetangaza kuwa kuanzia tarehe 16 Machi 2017  wateja watakaojiunga na kifurushi cha kuanzia Mambo watapata ofa ya wiki moja  ya kifurushi cha Uhuru.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo Maeneja Masoko wa StarTimes Tanzania, Felix Awino amesema kuwa wateja waliolipia  watafurahia maudhui mazuri yatakayokidhi na kuburudisha familia msimu mzima  wa pasaka.Ambapo ndani ya wiki nne (4) wiki moja ya kwanza mteja atafurahia kifurushi cha juu.
“ watazamaji watakaolipia mwezi moja kifurushi cha Mambo (sh.12000) wataweza kufuruhia wiki moja kifurushi cha Uhuru (sh.24,000) ambayo inazaidi ya chaneli kumi na tano (15). Chaneli hizo ni pamoja na Startimes Novella, ,Nat Geo Wild,Startimes World Football,Sport Arena  na Nyingine Nyingi”. Amesema Awino
 “pakacha la pasaka linatoa fursa nzuri kwa watazamaji kujionea maudhui mazuri yanaopatikana kwenye vifurushi vya Uhuru na Super na pia katika  kifurushi chochote  watakacholipia msimu huu  kwenye kingamuzi cha StarTimes” ameongeza  Awino
Startimes inatoa bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya kingamuzi,televisheni ya kidigitali,simu na huduma ya kulipia kifurushi.Tutaendelea kuwapa wateja huduma za kisasa  na nafuu zinazoendana na wakati kulingana na ukuaji wa teknolojia na mahitaji ya wateja ili kufurahia ulimwengu wa kidigitali.

DIWANI VINGUNTI AJUMUIKA KUSAMBAZA KIFUSI

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akisamba za kifusi katika barabara ya Mtakuja mara baada ya eneo hilo kuwa korofi kutokana na kuwepo kwa mashimo mengi ambayo yanajaa maji muda wote pindi mvua zinaponyesha
 Baadhi ya Vijana na Wakazi wa Vingunguti wa mtaa wa mtakuja wakijitolea kuchimba mitaro na kusambaza kifusi katika barabara ya mtaa wa Mtakuja
 Omary Kumbilamoto akisambaza kifusi katika mtaa wa mtakuja  Vingunguti kuziba mashimo akiwa na watoto wadogo kwa lengo la kuwafundisha umuhimu wa  kuwa wazalendo kujitolea katika shughuri za wananchi pindi watakapokuwa wakubwa

WAANDISHI WATAKIWA KKUNDA CHMA KITAKACHO TETEA MASLAHI YAO

 Katibu mkuu wa CHODAWU, Said Wamba akizungumza na waandishi wa habri juu ya warsha ya tafiti kwa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifatilia kwa maini hotuba ya katibu mkuu wa CHODAWU


 Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii

Wito umetolewa kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari  nchini  kuunda chama chao cha Wafanyakazi ambacho kitaweza kutetea maslahi yao katika kazi.

Hayo yamezungumzwa na Katibu mkuu wa CHODAWU, Said Wamba alipokuwa akifungua  Warsha juu ya tafiti kwa wafanyakazi wasio katika sekta isiyo rasmi katika ofsi za CHODAWU Jijini Dar es Salaam


"Waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wafanyakazi wengi hapa nchini lakini cha kushangaza mpaka sasa awana chama chao ambacho kinaweze kuwatetea pindi wanapopata matatizo na wanapohitaji kupanga maslahi yao" Amesema Wamba.

aidha ameongoza watu wengine ambao wamekuwa wakidhalaurika ni wafanyakazi wa ndani ambao wanachama chao ambacho kina watetea lakini wengi wao wamekuwa wazito kujiunga.

ametoa wito kwa wadau wote na watu ambao wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi hili wawezekupata maslahi yao.
Mratibu TUCTA Kanda ya Afrika Vicky Kanyoka  akizungumza na wadau mbalimbali ambao wameshiriki warsha hiyo


Monday, March 27, 2017

BASATA YAKABIDHI VYETI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MITAHANI YA KIDATO CHA NNE

 Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa akizungumza na wadau walifika katika hafla ya ugawaji vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika mtihani wa somo la Sanaa.
 Baadhi ya washiriki waliofika kushuhudia ugawji huo wa vyeti
 Rais wa Shirikisho la Sanaa Maonyesho , William Chitanda akizungumza juu ya umuhimu wa wanafunzi kufanya sanaa pindi wanapokuwa mashuleni
 Baadhi wanafunzi wa Sekondari wakiwa wana fatilia hafla hiyo
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo wakitoa burudani katika sherehe za kukabidhi vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika mtihani ya kidato cha nne
 Afisa wa Basata Bonnah Masenge akizungumza na wadau wa Sanaa walifika katika hafla hiyo
 Mwanamuziki mkongwe John Kitime akitoa somo kwa wanafunzi ju ya ushikaji wa kipaza sauti hili waweze kusikika vizuri
 Mwanafunzi Royola Sekondari , Shadrack Mboya akikabidhiwa  Cheti na psesa Taslim shilingi laki tano baada ya kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne
 Mwanafunzi wa Royola Sekondari , William Mukasa  akikabidhiwa zwadi ya cheti na fedha tslim shilingi laki mbili na amsini
 Mwanafunzi wa Royola Sekondari Josia Sooi akikisitiziwa jambo mara abaada ya kupewa zawadi yake na William Chitanda
 Wanafunzi  Royola Sekondari walifanya vizuri wakiwa katika picha ya pamoja
Mwanafunzi wa Azania Sekondari , Benjamini Kulwa akipokea cheti na fedha kutoka kwa mgeni rasmi William Chatanda

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...