Saturday, April 8, 2017

WANAUME SHINYANGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUTAHIRIWA,47,500 WAPATA TOHARA BURE


SeeBait


Huduma za tohara kwa wanaume zimeshamiri mkoani Shinyanga ambapo zaidi ya wanaume 47,500 wamenufaika na huduma hiyo katika kipindi cha Mwezi Oktoba 2016 hadi Machi 2017 kupitia kampeni ya Tohara Kinga ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili kujikinga na maambukizi ya VVU. 

Kampeni hiyo inaendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Intrahealth International kwa ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizi ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia Centre for Diseases prevention and Control (CDC). 
Akizungumza na waandishi wa habari jana,Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya VVU mkoa wa Shinyanga Dkt. Mawazo Amri Saleh amesema serikali imekuwa ikishirikiana na shirika la Intrahealth International katika kuendesha huduma ya tohara kwa vijana na wanaume kuanzia miaka 10 na kuendelea. 
Alisema tangu waanze kampeni hiyo katika halmashauri sita za mkoa wa Shinyanga mwezi Oktoba 2016 mpaka mwezi Machi 2017, zaidi ya wanaume 47,500 wamepatiwa huduma ya tohara bila malipo yoyote. 
Alisema huduma hizo zilitolewa kupitia mfumo wa huduma vituoni na huduma za nje ya vituo zinazotolewa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali zipatazo 50 katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga. 
“Lengo la kampeni hii ni kuwapatia huduma wanaume 95,900 katika kipindi cha mwezi Oktoba 2016 hadi Septemba 2017 lakini mpaka sasa tumefikia asilimia 50 ya lengo lililokusudiwa”,alieleza Dkt. Saleh. 
Alizitaja faida za tohara kwa wanaume kuwa ni pamoja na kujikinga na maambukizi ya VVU kwa asilimia 60,kuwa msafi,kujikinga na magonjwa ya ngono,kujikinga na kansa ya kichwa cha uume na kuwakinga akina mama kansa ya mlango wa kizazi. 
Aliongeza kuwa zoezi la tohara kwa wanaume linazidi kuwa na mwitikio mzuri kwani wanaume wengi wamekuwa wakijitokeza kupata huduma ya tohara. 
“Tunatoa shukrani kwa shirika la IntraHealth kwa ushirikiano mzuri wanaoutoa katika utoaji huduma za tohara mkoani hapa,tunaamini kuwa kutokana na mipango IntraHealth tuliyopanga kwa mkoa na wilaya lengo la mkoa la kufikia asilimia 80 ya tohara kwa wanaume wote mkoani hapa litafanikiwa”,aliongeza Dkt. Saleh. 
Naye Mshauri wa Kiufundi wa masuala ya tohara mkoa wa Shinyanga kutoka shirika la Intrahealth International, Dkt. Innocent Mbughi alisema mbali na mkoa wa Shinyanga hivi sasa shirika hilo linatekeleza pia mradi wa tohara ya mwanaume katika mikoa ya Mwanza, Geita, na Simiyu ambapo katika kipindi cha mwezi Novemba 2016 hadi Machi 2017, zaidi ya wanaume 127,000 wamepatiwa huduma za tohara. 
Dkt. Mbughi alisema wamefikia asilimia 50 kwani lengo ni kuwapatia huduma za tohara wanaume wapatao 256, 529 katika kipindi cha mwezi Oktoba 2016 hadi Septemba 2017 katika mikoa hiyo ambapo pia huduma ya upimaji wa hiari wa VVU inatolewa.
Dkt. Mbughi alibainisha kuwa shirika la Intrahealth International kwa ufadhili wa Mfuko wa rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizi ya UKIMWI (PEPFAR) kupitia Centre for Diseases prevention and Control (CDC) limekuwa likishirikiana na serikali kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, kitengo cha kuzuia kuenea kwa maambukizi ya VVU (NACP), kamati za afya za mkoa na wilaya na wadau wengine wa afya katika kutoa huduma bora za tohara kwa wanaume. 
Serikali ya Tanzania imeandaa mpango wa kitaifa wa kutekeleza huduma za tohara ili kufikia lengo la kitaifa la asilimia 80 kutoka asilimia 72 kwa sasa (THIMS report 2011) ambapo kipaumbele kimeelekezwa kwenye mikoa yenye viwango vya chini vya huduma za tohara na maambukizi ya VVU.
Mikoa hiyo ni Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Katavi, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera, Ruvuma na Mara wilaya ya Rorya.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametembelea baadhi ya vituo vinavyotoa huduma ya tohara katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kahama Mji ametusogezea picha 22 za matukio
Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya VVU mkoa wa Shinyanga Dkt. Mawazo Amri Saleh akielezea namna serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoshirikiana na shirika la Intrahealth International kuendesha kampeni ya tohara bure kwa vijana na wanaume kuanzia miaka 10 na kuendelea. Alisema jamii nyingi nchini Tanzania hufanya tohara ya mwanaume kwa sababu za kijadi na kiimani lakini sasa wanaume wengi wamehamasika kupata huduma hiyo. 
Mshauri wa Kiufundi wa masuala ya tohara mkoa wa Shinyanga kutoka shirika la Intrahealth International, Dkt. Innocent Mbughi akielezea namna wanavyoendesha kampeni ya tohara kwa wanaume katika mfumo wa huduma za nje ya vituo (outreach) katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Kahama Mji lililoanza Machi 15,2017 hadi Aprili 11,2017 ambapo mpaka Aprili 6,2017 zaidi ya wanaume 10,000/= wamepatiwa huduma ya tohara bure.
Dkt. Mbughi alisema takwimu za wanaume 47,500 kufanyiwa tohara kuanzia Oktoba 2016 hadi Machi 2017,zinatokana na huduma iliyotolewa kupitia mfumo wa huduma vituoni na huduma za nje ya vituo ambapo jumla ya hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali zipatazo 50 katika wilaya zote za mkoa wa Shinyanga zimefikiwa. 
Aprili 6,2017-Hapa ni katika zahanati ya Mwabomba iliyopo katika kijiji Mwabomba kata ya Idahina halmashauri ya Ushetu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo huduma ya tohara kwa wanaume katika mfumo wa nje ya huduma za kudumu za tohara imeanza Machi 15 hadi Aprili 11,2017-Pichani ni vijana na wanaume wakisubiri kupata huduma ya tohara
Mhudumu wa Tohara katika zahanati ya Mwabomba Lydia Mabagala akizungumzia huduma ya tohara waliyoanza kuitoa tangu Machi 15,2017 mpaka Aprili 11,2017 ambapo mpaka Aprili 6,2017 jumla ya wanaume 880 walikuwa wamepatiwa huduma ya tohara katika zanahati ya Mwabomba. Katika kufanikisha utoaji wa huduma za tohara,jumla ya watoa huduma wa afya wapatao 166 wa kada mbalimbali za afya waliopata mafunzo juu ya namna bora za utoaji wa huduma za tohara kwa wanaume wameshiriki katika kutoa huduma. 
Mtaalam wa afya akimfanyia tohara mwanamme aliyefika katika zahanati ya Mwabomba kupata huduma ya tohara bure.Umuhimu wa tohara ya mwanaume umeongezeka tangu pale Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilipopitisha matokeo ya kisayansi yaliyoonesha kwamba tohara ya mwanaume ina changia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa wanaume hadi kwa asilimia 60. 
Vijana wakielezea kuhusu namna watakavyofaidika na huduma ya tohara waliyofanyiwa katika zahanati ya Mwabomba .Kulia ni Mhudumu wa tohara katika zahanati ya Mwabomba, Lydia Mabagala 
Bwana James Medard akielezea umuhimu wa mwanamme kufanyiwa tohara 
Bi. Rebeca Daudi akielezea namna alivyohamasika na kuamua kumpeleka mtoto wake katika zahanati ya Mwabomba ili apatiwe huduma ya tohara
Vifaa vinavyotumika kufanyia tohara 
Afisa kutoka Intrahealth International, Andrew Richard akionesha mashine inayotumika kusafishia vifaa vinavyotumika kufanyia huduma ya tohara
Hapa ni katika ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Tumaini kata ya Wendele halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo zoezi la kuwafanyia tohara wanaume linaendelea. Kulia ni Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akitoa elimu ya tohara kwa vijana na wanaume waliofika katika kituo hicho kupata huduma ya tohara 
Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akionesha mfano wa uume ambao haujafanyiwa tohara wakati akitoa elimuya tohara
Huduma ya tohara ikiendelea katika kituo cha Tumaini kata ya Wendele
Uume kabla ya tohara na baada ya tohara
Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akielezea umuhimu wa mwanamme kufanyiwa tohara. Alisema kwa kipindi cha Machi 15 mpaka Aprili 6,2017 jumla ya wanaume 706 wamefanyiwa tohara katika kituo hicho 
Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akionesha mfano wa uume ambao haujafanyiwa tohara na uume ambao umefanyiwa tohara.Kushoto ni Maria Mwakisyala ambaye ni miongoni mwa watoa huduma ya tohara katika kituo hicho cha Tumaini 
Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akionesha mfano wa uume ambao haujafanyiwa tohara 
Zoezi la kuandikisha vijana na wanaume ili wafanyie tohara likiendelea
Mtoa huduma za tohara Nchama Samson akimpima presha mkazi wa kijiji cha Tumaini aliyefika katika kituo hicho 
Ndaki Lucas akielezea faida za tohara kwa mwanamme 
Helena Gabriel aliyemleta mtoto wake kupata huduma ya tohara akielezea faida ya tohara na kulishukuru shirika la Intrahealth International kuendesha zoezi hilo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

MSONGO WA MAWAZO BADO NI TATIZO DUNIANI

Shirika la Afya Duniani Ijumaa limeadhimisha siku ya afya duniani likionya kwamba msongo wa mawazo (depression) ni moja ya sababu kuu za afya mbaya duniani.

Msongo huo ambao unaripotiwa kuwaathiri takriban watu milioni 300 kote duniani. Idara hiyo ya Umoja wa Mataifa imewasihi watu kutafuta tiba kwa msongo wa mawazo, ambao unaweza kupelekea ulemavu na hata kifo.

WHO inasema mzozo, vita na majanga ya asili ndiyo vigezo vikuu kwa mtu kupata msongo wa mawazo.

Idara ya Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa katika kila watu watano kuna mtu mmoja ambaye ameathiriwa na msongo wa mawazo au wasi wasi. Hasa ikizingatiwa kiwango cha tatizo lilivyo, na kusema misaada kwa afya ya akili na kijamii iwe ni sehemu ya misaada ya kibinadamu.

Mbali ya hali hizi, WHO inaripoti kuwa msongo wa mawazo ni sababu inayoongoza katika mtu kupata ulemavu. Mkurugenzi wa WHO katika idara ya afya ya akili na matumizi mabaya ya madawa, Shekhar Saxena anasema msongo wa mawazo ni janga la ulimwengu kwa watu kujiua.

“Duniani kote, watu 800,000 wanafariki kwasababu ya kujiua kila mwaka na hii ni sawa na kifo kimoja kila sekunde 40. Kwahiyo, wakati tunakabiliana na idadi ya vifo, ambavyo kwa hakika ni bahati mbaya katika maeneo yenye mizozo na vita, pia tunahitaji kukumbuka kwamba kuna milipuko ya siri inayoendelea duniani, ambayo huua idadi kubwa ya watu bila ya kutangazwa au kuzungumziwa sawa,” amesema Bwana Saxena.

Saxena ameiambia VOA hakuna tofauti kubwa katika kiwango cha msongo wa mawazo kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Ameelezea kwamba watu wengi wenye msongo wa mawazo wanaishi katika nchi za daraja la chini na kati.

“Msongo wa mawazo ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake, asilimia 5.1 dhidi ya asilimia 3.6 miongoni mwa wanaume. Vigezo vingine ni umaskini, ubaguzi, na hali nyingine zote za maisha – iwe ni masuala sugu au ya hapo kwa hapo, hasa miongoni mwa vijana wadogo,” amesema Saxena.

Anasema matibabu kwa kawaida yanahusisha matibabu ya kisaikolojia, dawa za mfadhaiko na mchanganyiko wa dawa hizo. Anasema si muhimu kuwa a mtaalamu wa kutibu msongo wa mawazo. Anasema kinachojulikana tiba na madaktari wa kawaida, wauguzi au wafanyakazi wa afya inaweza kuwa na ufanisi mkubwa.

WASICHA WATAKIWA KUISMOA HII JE WAJUA: TAULO YA KIKE YAWEZA KUKUSABABISHIA UGUMBA, SOMA HAPA


https://image.shutterstock.com/z/stock-vector-an-image-of-a-menstrual-cycle-chart-74110774.jpg 
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
HEDHI ni mzunguko wa kila mwezi ambao huleta kutokwa na damu ukeni, hali hiyo hutokea pale ambapo yai la mwanamke linakuwa halijakutana na mbegu ya kiume ili kulirubutisha kutengeneza mtoto.
Kila mwanamke ana mzunguko wake wa hedhi, ingawa kwa kawaida hedhi ya kwanza hutokea katika umri wa miaka 12 na 13 hata hivyo wapo ambao huanza kupata hedhi katika umri mdogo wa kati ya miaka tisa hata 10.
Mzunguko wa hedhi hudhibitiwa na homoni zinazozalishwa na mwili wenyewe, hedhi hutokea pale ambapo tishu za ukuta wa mji wa mimba hubomoka na kutoka kama damu ukeni.
Hedhi ni kipindi maalumu katika maisha ya mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa.
Kwa kawaida mzunguko wa hedhi hutokea kila mwezi na kila mwanamke anao mzunguko wake ni hapo ambapo mwili hujiandaa kwa hali ya kupata ujauzito.
Jinsi inavyotokea
Mwanamke ana ovary mbili (vifuko vya mayai) katika mwili wake, moja upande wa kushoto na nyingine kulia ambazo hutengeneza mayai ya uzazi.
Kila mwezi, ovary moja huachilia yai kitendo hicho kitaalamu huitwa ‘ovulation’ yai husafirishwa hadi katika mji wa mimba kupitia mirija ya uzazi.
Wakati huo mabadiliko ya homoni huuandaa mji wa mimba (uterusi) kutengeneza ukuta mpya uitwao ‘endometrium’ kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mapokezi ya mimba inayoweza kutungwa.
Yai linalofika katika mji wa mimba (uterasi) iwapo halitarutubishwa na mbegu ya mwanamume, ukuta huo humeguka na kutoka nje ya mji wa mimba kupitia ukeni ukiwa pamoja na damu.
Kitendo hicho ndicho huitwa hedhi (menstruation) au mzunguko wa hedhi (menstruation cycle). Mara nyingi mwanamke hukoma hedhi anapotimiza umri wa kuanzia miaka 45 hadi 50.
Ingawa ni kipindi muhimu katika maisha ya mwanamke lakini huwa kimejaa changamoto ambazo huzipitia, changamoto hizo hutofautina kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
Wapo ambao hupata hedhi kwa siku tatu na wengine huenda hadi saba na miongoni mwao wapo pia ambao hupata hedhi nyepesi na wengine nzito.
Wapo pia ambao hupata hedhi pasipo kukabiliana na matatizo yoyote lakini wengine hupata hedhi kwa uchungu na masumbufu mengi, kama kuumwa tumbo, mgongo, kichwa, kiuno na mengineyo.
https://www.wellandgood.com/wp-content/uploads/2016/12/lola-pad.jpgUsafi muhimu
Pamoja na yote hayo, suala la usafi ni jambo la muhimu mwanamke anapaswa kuzingatia kipindi chote maishani mwake, hasa kipindi cha mzunguko wa hedhi.
Ili kujiitiri katika kipindi hicho muhimu, mwanamke hulazimika kutumia kifaa maalumu ambacho hukinga damu ya hedhi ili asichafuke.
Inawezekana ikawa ni kitambaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo iwe kwa njia ya asili au kisasa, hujulikana kama pedi au taulo za kike.
Enzi za mabibi zetu njia iliyokuwa ikitumika zaidi ni ile ya asili, walitengeneza vipande vya kanga au kitenge kujisitiri.
Lakini kukua kwa teknolojia kukapelekea kutengenezwa taulo za kisasa za kutumia na kutupa ambazo huuzwa kwa bei tofauti tofauti madukani.
Daktari
Akizungumza hivi karibuni na MTANZANIA, Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Belinda Balandya anasema kipindi cha hedhi ni cha muhimu kwa afya ya mwanamke.
“Mwanamke anapokuwa katika siku zake hulazimika kutumia taulo hizo ambazo kazi yake kuu ni kupokea ile damu inayotoka, kama hatavaa maana yake ni kwamba itapitiliza kuchafua nguo zake.
“Taulo za kutumia na kutupa jinsi zilivyotengenezwa zina ‘layer’ maalumu kwa ndani ambayo hufyonza damu ya hedhi, hulazimu kubadili mara nyingi (kiasi cha kila baada ya saa nne) hasa inapokuwa inatoka kwa wingi,” anasema.
Madhara ya kuvaa taulo muda mrefu
Daktari huyo ambaye pia ni muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (Muhas) anasema kuna athari kubwa iwapo mwanamke hatazingatia usafi akiwa katika kipindi hicho katika via vyake vya uzazi.
“Kwa kuwa inanyonya damu maana yake ni kwamba hufika wakati unakuwa kama vile umevaa kitu kibichi, hivyo ngozi huanza kupata michubuko. Kwa wale ambao ngozi yao ni ngumu kidogo huwa si rahisi kuona michubuko hiyo lakini wanapojisafisha kwa maji na sabuni huhisi maumivu,” anasema.
Bakteria huzaliana
Anaongeza “Damu ni sehemu ambayo bacteria huota kwa urahisi kwa sababu wanakuwa wanapata chakula wanachohitaji kwa urahisi, mtu anaweza kuendelea kuvaa kwa sababu hajui jambo hili lakini ni hatari.
“Kwa sababu bakteria wanakua kwa urahisi husababisha pia muhusika kupata maambukizi katika sehemu zake za siri,” anasema.
Wanaotumia vitambaa
Anasema iwapo mtu anatumia vitambaa alivyovitengeneza kujisitiri navyo vinapaswa kukauka ili bakteria wasipate nafasi ya kuzaliana.
“Kumbuka kwamba nimesema bakteria huzaliana kwa urahisi kwenye damu, kitambaa kisipokauka na kubaki na unyevunyevu maana yake ni kwamba bakteria waliozaliwa watabaki hawajafa kwa hiyo wataendelea kukua hivyo muhusika atakuwa amejiweka kwenye ‘risk’ ya kupata ‘infections,” anasema.
Anaongeza “Kuna pedi  fulani...zimetengenezwa mfano wa unene wa  kidole na imewekwa kamba kidogo. Wapo wanawake wanazitumia, zinauzwa huko madukani, huingizwa ndani ya uke ili kufyonza damu na huitoa kwa kuvuta kamba hiyo inayokuwa imebaki nje ya uke.
“Sasa hizi ni taulo mbaya zaidi, wengine wanapoweka wakati wa hedhi chache, hujisahau kuzitoa na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kupata madhara,” anasema.
http://www.news-medical.net/image.axd?picture=2012%2F11%2Futerus-1.jpg
Mfumo wa uzazi wa mwanamke

Athari yenyewe
Anasema bakteria hao huenda kutengeneza kovu katika mirija ya uzazi na mwisho huziba kabisa na kwamba huweza kupenya na kuingia hadi katika mfumo wa damu na kuleta athari zaidi.
“Kama mwanamke huyu hatawahi hospitalini anakuwa yupo kwenye hatari hata ya kushindwa kushika ujauzito kwa sababu bakteria hao huendelea kushambulia mfumo wake,” anasema.
Kauli za wanawake
Julieth Masinga Mkazi wa Mbezi Luis anasema awali hakuwa anajua iwapo taulo ya kike inaweza kusabisha madhara makubwa namna hiyo.
“Najua suala la usafi ni la msingi lakini sikuwahi kujua nini madhara ambayo yanaweza kujitokeza iwapo mwanamke atakaa muda mrefu akiwa amevaa taulo moja kwa muda mrefu,” anasema.
Anaongeza “Binafsi huwa sipendelei kukaa na taulo moja muda mrefu lakini kuna wakati unashindwa jinsi ya kufanya kwa mfano ukiwa safarini unatumia muda mrefu barabarani, ni changamoto kwa kweli.
“Kuna siku nilikuwa kwenye mizunguko yangu ya kibiashara nilitumia muda mrefu mno, nilikuwa kwenye siku zangu, kusema ukweli nilijihisi vibaya kukaa muda mrefu bila kujisafisha, nililazimika kutafuta bafu la kulipia nikaoga na kubadili pedi nyingine.
“Lakini itabidi tuzingatie ushauri wa daktari ili tuweze kujilinda afya zetu tusipate maambukizi,” anasema.
Mkazi wa Sinza Kijiweni, Pelina Yesaya anasema bado elimu kuhusu hedhi inahitajika hasa kwa kundi la wasichana wadogo.
“Kwa mfano huko vijijini bado kuna maeneo ambayo wasichana wanahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu hedhi, jinsi inavyotokea na namna ya kujisitiri na hata kuepukana na mimba za utotoni,” anasema.
Anaongeza “Kule wengi hawajafikiwa angalau huku mjini watu wanao uwezo wa kutumia taulo ya kutumia na kutupa, kule wengi wanatumia taulo za asili, kwa hiyo kuna ulazima mkubwa wa kuwapelekea elimu kama hii ili wawe salama,” anasema.

WAZAZI WATAKIWA KUWA MAKINI NA KUSOMA HII; PAMPASI, NEPI ZINAVYOWEZA KUSABABISHA UGONJWA WA UTI, FIGOhttp://www.suitcases4kidsmi.org/gty_diaper_baby_thg_110926_wmain.jpgNA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM
BIDHAA pekee ambayo miaka ya nyuma ilikuwa ikitumika kumuhifadhi mtoto pindi anapojisaidia haja ndogo au kubwa ilikuwa nepi na chupi maalumu maarufu chupi ya mkojo.
Lakini kadri siku zinavyosonga mbele kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kitekonolojia leo hii kuna bidhaa mpya inayotumika ambayo imejizolea umaarufu mkubwa (pampasi).
Kwa kawaida pampers hutofautiana bei kulingana na ukubwa, aina na kiwanda ilikotengenezwa lakini huwa ni kati ya Sh 10,000 na zaidi.
Frolence Mussa (si jina lake halisi), mkazi wa Mbezi ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja.
Anasema huwa anatumia bidhaa zote mbili (nepi na pampasi) kumsitiri mtoto wake lakini huwa inategemea na sehemu alipo.
“Kwa mfano nikiwa nyumbani huwa namvalisha nepi na mara nyingi huwa ni kipindi cha usiku tunapokwenda kulala lakini tunapotoka kwenda safari au kanisani huwa namvalisha pampasi,” anasema.
 ..
Florence anasema mchana huwa hamvalishi nepi wala pampers badala yake humvalisha kamputa pekee na kumbadilisha kila anapojisaidia.
“Sipendi kumvalisha nepi wala pampers mchana maana wakati mwingine huwa zinamchubua, hasa pampasi,” anasema.
Anasema hata hivyo wakiwa wamekwenda safari humvalisha pampasi na ikiwa anakuwa hajajisaidia haja kubwa ukaa nayo kwa saa sita.
“Huwa namuacha anakaa nayo hata saa sita, si anakuwa amejisaidia haja ndogo tu lakini inapotokea amejisaidia haja kubwa inabidi nimbadilishe.
“Napenda kutumia pampasi zaidi tukiwa safari maana anakaa nayo muda mrefu kunakuwa hakuna ule usumbufu wa kumbadilisha kila mara, si kama nepi yenyewe unalazimika kumbadilisha mara kwa mara,” anasema.
Shija Mabula ambaye ni baba wa mtoto mmoja anasema huwa anapenda zaidi mtoto wake avae pampasi kuliko nepi.
“Pampasi anakaa nayo muda mrefu hata zaidi ya saa mbili ikiwa hajajisaidia haja ndogo mara nyingi au kubwa. Huwa tunamvalisha zaidi usiku na tukiwa safari,” anasema.
https://1.bp.blogspot.com/-dbv2qSwr5f8/VqOnuTYLCtI/AAAAAAAABt4/BooKR8Tvb1Y/s640/kidneys%2B%2528wwwinteractive-biologycom%2529.jpgJe kuna athari gani
Shija na Florence wote hawajui iwapo hatua yao hiyo inaweza kuwasababishia matatizo watoto wao wapendwa katika maisha yao siku zijazo.
MTANZANIA limefanya mahojiano na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gudila Valentine na hapa anaeleza athari anazoweza kuzipata mtoto kutokana na hatua hiyo.
“Ni hatari kumuacha mtoto muda mrefu akiwa amevaa pampers moja kwani inaweza kumsababishia kupata magonjwa ya UTI na baadae anaweza kupata ugonjwa sugu la figo,” anasema.
Inakuwaje
Dk. Gudila ambaye kwa sasa anasomea ubingwa katika magonjwa ya figo kwenye Chuo Kikuu Kishirikishi cha Sayansi ya Tiba (Muhas) anafafanua,
“Mtoto akikaa na pampasi au nepi muda mrefu ni hatari kwani husababisha mtoto kupata maambukizi, iwapo anakuwa amejisaidia muda mrefu na kukaa na pampasi au nepi yake, kile kinyesi kinakuwa kama kinarudi, kuelekea kwenye njia ya mkojo.
“Bakteria anayesababisha UTI anaishi kwenye sehemu ya haja kubwa, kwa hiyo lazima mtoto naye asafishwe mara kwa mara kama ilivyo kwa watu wazima ili kumkinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu,” anasema.
Anasisitiza “Lazima usafi uwe kitu cha kwanza. Kwa kuwa bakteria yupo kwenye kinyesi, kinapokaa pale kwa muda mrefu hasa akiwa ni mtoto wa kike kinapata nafasi ya kupanda  na kurudi kwenye njia ya mkojo kwa sababu zile njia zimekaa karibu karibu, hivyo inakuwa rahisi kwa yeye kupata UTI.
Anasema ndiyo maana huwa inashauriwa wasafishwe na kubadilishwa nepi au pampasi mara kwa mara kwamba usafi ni suala la msingi na wale watoto wakubwa wasafishwe kutoka mbele kwenda nyuma.
Sababu nyinginezo
Anasema wapo watu ambao hudhani kuwa watoto huwa haugui magonjwa ya figo jambo ambalo si kweli.
“Watoto nao wanaugua magonjwa ya figo kama ilivyo kwa watu wazima, mara nyingi visababishi kwa watoto ni pamoja na hayo magonjwa ya maambukizi kwa mfano ya kuziba kwa njia ya mkojo (UTI) ya kujirudia rudia na kuharisha ambako hutokana na homa ya virusi,” anasema.
Daktari huyo anasema sababu nyingine ni kutapika ambapo husababisha mwili wa mtoto kupoteza maji mengi na kupelekea magonjwa ya figo baadae.
“Kuna magonjwa mengine kama maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), homa ya ini na malaria sugu, yote haya yanaweza kusababisha mtoto kupata magonjwa ya figo,” anasema.
Dk. Gudila anasema mtoto mwenye lishe duni naye huwa kwenye hatari ya kupata tatizo la figo.
“Mtoto akiwa na lishe duni hupata utapiamlo ambao huchochea baadae kupata magonjwa ya figo, matumizi mabaya ya dawa za kutuliza maumivu jamii ya diclofenac na dawa za kienyeji ambazo huwa zinatokewa bila kiwango maalumu, zote hizi zinaweza kusababisha mtoto kupata magonjwa ya figo,” anasema.
Anasema kuna baadhi ya magonjwa ya kuzaliwa nayo kama kuziba njia ya mkojo, na mengine mtoto hurithi toka kwa wazazi wake ambayo yanaweza kumsababishia magonjwa ya figo maishani mwake. https://static.independent.co.uk/s3fs-public/styles/article_small/public/thumbnails/image/2017/01/07/15/cough.jpg
Utajuaje njia ya mkojo imeziba.
Dk. Gudila anasema kitu ambacho mzazi ataweza kukiona mapema ni kwamba atakuta mtoto hapati mkojo vizuri mara tu baada ya kuzaliwa, au akikojoa unakuwa na damu au mtoto.
“Mzazi anapoona mkojo wa mtoto wake unatoka kwa kusita sita au kiwango cha mkojo wa mwanawe kinapungua amuwahishe mapema ili afanyiwe uchunguzi,” anasema.
Anaongeza “Inapokuwa hivyo ajue tayari kuna shida, au mkojo ukitoka vitone vitone ni tatizo, kawaida mtoto akikojoa mkojo ule unatakiwa uruke mbali lakini si kutoka kidogo.
Anasema mtoto anapokuwa amezaliwa ndani ya saa 24 mama anatakiwa awe ameona mwanawe ameanza kujisaidia haja ndogo.
“Sasa unakuta mtoto kakaa hata siku tatu hajakojoa mama hashtuki kama ni tatizo anaendelea kukaa naye nyumbani baadae sasa ndipo anaanza kuvimba mwili,” anasema.
Magonjwa mengineyo
Daktari huyo anasema magonjwa ya saratani nayo huweza kusababisha mtoto kupata magonjwa ya figo.
“Kwa mfano saratani ya mfuko wa mkojo ambayo tunaiita kitaalamu ‘blader cancer”, anaweza pia kuugua magonjwa ya ndani ya figo ambayo mara nyingi shida huwa inatokea pale kwenye chujio la figo,” anasema.
 http://med.stanford.edu/content/dam/sm-news/images/2014/06/kidney-stock.jpg
Jinsi ya kumkinga
Anasema jambo la msingi ni kufuata zile kanuni za afya.
“Tunashauri mtoto anyonyeshwe miezi sita yote ya kwanza baada ya kuzaliwa bila kupewa chakula kingine, inamsaidia kupata lishe bora na ni njia nzuri ya kumkinga na maradhi mbalimbali ikiwamo kuharisha, utapiamlo, maambukizi na mengineyo,” anasema.
Anasema mama ahudhurie kliniki mara kwa mara kwani huko hupewa elimu ya jinsi ya kumkinga mwanawe na magonjwa mbalimbali ukiwamo huo wa figo.
“Kliniki wanapewa chanjo pia ambazo huwakinga na magonjwa mengi, mtoto akiugua mpeleke hospitalini atibiwe na si kununua dawa kiholela,” anasema.
Ushuhuda
Asha Juma (si jina lake halisi) anasema kuna changamoto nyingi katika kulea mtoto mwenye tatizo la figo.
“Mwanangu ana miaka miwili sasa, alianza kuvimba macho, nilipomlaza kifudi fudi akiamka macho yake yalikuwa yamevimba,” anasema.
Anasema alimpeleka katika kituo cha afya ambapo hawakugundua tatizo lake wakarudi nyumbani.
“Kadri siku zilivyoenda mbele ndivyo hali ilivyozidi kuwa mbaya, ukuaji wake ulikuwa si mzuri, nywele zake hazikuota vizuri, miguu na tumbo lake likaanza kuvimba,” anasimulia.
Asha anasema aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo aligundulika kuwa na ugonjwa wa figo.
“Waligundua figo yake ina matundu ambayo yanaruhusu maji kuingia mwilini ndiyo maana anavimba miguu na tumbo,” anasema.
Anasema alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anatibiwa hadi leo.
“Pengine ingegundulika mapema asingekuwa na hali mbaya maana alikuwa akipata malaria mara kwa mara, homa, mafua, na UTI,” anasema kwa huzuni.
Anaongeza “Madaktari walinieleza huenda amerithi kwa sababu kwenye familia ya mume wangu wapo ambao wanaugua ugonjwa huu.
Anasema changamoto kubwa anayoipata ni kukaa muda mwingi akimtunza mtoto wake huyo na kushindwa kufanya shughuli zake za kiuchumi.
“Sitakiwi kumpa maji mengi, tatizo kwa kuwa ameanza kutembea wakati mwingine akiyakuta anakunywa mengi inakuwa tatizo,” anasema.
 
Mnh inapokea 30 hadi 40 kila mwezi
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto na figo Muhimbili, Jacqueline Shoo (pichani) anasema wanapokea watoto 30 hadi 40 kila mwezi kwenye kliniki yao wakisumbuliwa na magonjwa hayo.
“Asilimia kubwa ya watoto tunaowaona wanaugua magonjwa sugu ya figo sawa na asilimia 60, kuliko magonjwa ya figo ya mshtuko,” anasema.
Chanzo
Anasema sababu kubwa waliyogundua kuwa chanzo cha watoto wanapokea kupata magonjwa hayo ni maambukizi, magonjwa ya kuharisha, UTI na malaria sugu.
“Magonjwa ya kuziba kwa njia ya mkojo, matumizi ya madawa lakini saratani zipo kwa kiasi kidogo mno,” anasema.

MVUA YASABABISHA MAJANGA CHALINZE MZEE, KAYA 20 ZAKOSA MAKAZI

 


 
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete (mwenye kanzu) akiwa na wananchi wa jimbo hilo wakikagua `Bwawa la Umwangiliaji la Msoga 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ametembelea eneo la Chalinze Mzee lilokumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jimbo hilo na kusababisha madhara ya nyumba kubomoka na nyumba 9 kusombwa na maji na kusababisha zaidi ya kaya 20 kukosa pakulala.

Akizungumza Ridhiwani,ametaja  maeneo yaliyokumbwa na  mafuriko ni Chalinze Mzee,Bwawa la umwangiliaji la Msoga ambalo limetoboka na shule ya Sekondari ya Imperial.

Aidha,amesema kuwa madhara makubwa yaliosababishwa na mafuriko hayo ni kuharibika kwa mashamba,nyumba za wananchi kuharibika na kusabbishwa wananchi kukosa pa kulala,na ameongeza kuwa kwasasa wananchi hao wanahitaji msaada. 

Ridhiwani ametoa pole kwa wakazi hao na kuwaomba kuwa vumilivu katika kipindi hiki.
 Baadhi ya Nyumba katika eneo la Chalinze Mzee zikiwa zimearibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiangalia madhara yaliosababishwa na mafuriko katika jimbo hilo la Chalinze.
 wakazi wa chalinze wakiangalia nyumba zao zilizobomoka kutokana na mafuriko.
 Sehemu ya bwawa la umwangiliaji la Msoga liloaribiwa na mafuriko na kupasua kingo za bwawa hilo.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
 Moja ya Nyumba iliyobomoka kutoka na mvua zinazoendelea kuonyesha katika eneo la Chalinze.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu katika Ofisi za kijiji cha Msoga.

MWIGULU NCHEMBA AFUTA UKIMYA SAKATA LA KUTEKWA KWA ROMA

Msanii wa hip hop Roma Mkatolikia alikamatwa April 5 usiku ambapo taarifa zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kuwa alikamatwa studio za Tongwe Records  na watu wasiojulikana akiwa na wenzake na wakapelekwa  kusikojulikana.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni.

Waziri Nchemba ameeleza kuwa amewaagiza polisi kufuatilia na kutoa taarifa kwa umma.

“Nimeshtushwa kwa kutokuonekana kwa Msanii Roma na Wenzake mpaka sasa. Nimeshtuka zaidi nilipofuatilia na kuambiwa hakuna kituo chochote cha polisi kinachowashikilia. Nimeelekeza Polisi wafuatilie kwa karibu kujua undani wa tukio hili na hatima yao na kutoa taarifa kwa umma”

SABABU ZA FARU FAUSTA KUTUMIA SH760 MILIONI KWA MWAKA ZATAJWA

Hakuna bosi yeyote serikalini anayelipwa zaidi ya Sh17 milioni baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kutekeleza sera zake za kubana matumizi, lakini yupo kiumbe hai mmoja tu ambaye matumizi yake yalifika Sh64 milioni kwa mwezi; na kuna sababu za kuhalalisha gharama hizo.
Kiumbe huyo ni mnyama mwitu aina ya faru aliyepewa jina la Fausta, ambaye sasa anatumia Sh20.4 milioni.
Fausta ndiye faru kikongwe kuliko wote nchini, akiwa na umri wa miaka 54, na anahitaji matunzo mazuri ili aendelee kuvuta watalii na wanasayansi kutoka kila pembe ya dunia.
Fausta anaishi Hifadhi ya Ngorongoro ambako analindwa kwa saa 24 kumuepusha kushambuliwa na wanyama wengine kama fisi na mbwa mwitu kutokana na uzee, lakini gharama za ulinzi zitapungua baada ya kupata makazi salama ndani ya mwitu jengo lake litakapomalizika.
Hiyo ni sehemu tu ya gharama zinazomfanya Fausta kutumia fedha nyingi zaidi ya mfanyakazi mwandamizi wa serikalini.

Kazi ipo kwenye malisho
Imeelezwa kuwa sababu zinazofanya matunzo ya Faru Fausta kutumia jumla ya Sh768 milioni kila mwaka ni pamoja na ulinzi, chakula chake kuagizwa kutoka nje na miwa anayotakiwa kula.
Sakata la Faru huyo kutumia kiasi hicho cha fedha liliibuliwa juzi na Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul alipoelezea gharama hizo na Serikali kuthibitisha.
Hata hivyo, Serikali imesema gharama hizo ni za kawaida kulingana na thamani na umuhimu wa mnyama huyo ambaye jamii yake iko hatarini kutoweka.
Meneja wa maendeleo ya tafiti na Ikolojia wa Hifadhi ya Ngorongoro, Asantaeli Merita alisema jana kuwa matunzo yake yalianza kugharimu fedha nyingi baada ya kuanza kutunzwa katika eneo maalumu.
Alisema katika eneo hilo ilibidi kujengwa banda lake la kuishi na uzio wa chuma ambao si rahisi faru huyo kuvunja na kutoka nje. Banda hilo limezungushiwa mbao maalumu.
Merita alisema kutokana na faru huyo kuwa katika eneo hilo, kuna askari 15 maalumu ambao wanamlinda kwa zamu kwa saa 24 na kuna gari ambalo ni la mahitaji mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubeba majani ya lishe kila siku.
Alisema ili kudhibiti maradhi ambayo faru huyo amekuwa akiugua, Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikigharamia chakula cha virutubisho aina ya luseni ambacho kinapatikana nchini Kenya na amekuwa akipelekewa chakula hicho mara mbili kwa mwezi.
Alisema luseni anayotumia Fausta ni tofauti na luseni ya ng’ombe wa maziwa ambayo inapatikana hapa nchini.
Alisema faru huyo ‘kikongwe’ pia amekuwa akipewa miwa ambayo inapatikana eneo la Dareda mkoani Manyara. Miwa hiyo humsaidia kuboresha afya yake na imekuwa ikipelekwa mara mbili kwa mwezi.
Merita alisema kuna dawa zake ambazo anapaswa kuzitumia kila baada ya wiki mbili.
“Hiyo gharama ya milioni 64 ni ya mwanzo tu baada ya kuanza kuhifadhiwa, lakini baada ya kupatikana eneo la kumuhifadhi na kujengwa itapungua sana,” alisema.
Alisema baada ya kukamilika ujenzi wa banda maalumu la kumuhifadhi kwa sasa wastani wa gharama kwa mwezi zitakuwa Sh20.8 milioni.
Merita alisema kwa maendeleo ya hifadhi ni muhimu kwa Fausta kuendelea kupatiwa matunzo maalumu kwa kuwa licha ya kuingiza fedha nyingi za kigeni, pia amekuwa akitumika katika tafiti za wataalumu wa hifadhi za asili.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikiingiza zaidi ya Sh70 bilioni kwa mwaka kutokana na watalii ambao wanafika kutembelea eneo hilo. Karibu nusu ya watalii wanaokuja nchini, hutembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
Katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Gekuji alihoji mpango wa Serikali kwa faru huyo kutokana na gharama kubwa za kumtunza.
“Hifadhi ya Ngorongoro inatumia gharama kubwa, ikiwa ni pamoja na kumtunza na kumlisha Faru Fausta. Kiasi cha Sh64 milioni kinatumika kwa mwezi. Je, Serikali ina mpango gani na huyu Faru Fausta,” alihoji Gekul.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema ni kweli mnyama huyo anatunzwa kwa gharama kubwa kwa sababu ni mzee na ananyemelewa na magonjwa mbalimbali.
Waziri alisema wanafanya hivyo kutokana na ukweli kuwa wanyama wa aina hiyo ni wachache katika hifadhi, akasema utafiti unafanyika ili gharama za kumtunza ziwe ndogo kulingana na thamani inayopatikana. Kiwango hicho cha fedha kilisababisha Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka kuomba mwongozo wa Spika.
”Majibu ya waziri anasema Faru Fausta yupo na anatunzwa kwa Sh64 milioni kwa mwezi. Tafsiri yake ni kwamba anatunzwa kwa Sh768 milioni kwa mwaka. Anatoa sifa eti kwa sababu ni mzee sana, naomba mwongozo wako kuhusu hili kwa sababu mnyama huyu hawezi kuingiza faida yoyote,” alisema Mwakajoka.
Akitoa mwongozo wake Spika Job Ndugai alisema suala hilo anaiachia wizara.

Chanzo: Mwananchi

YANGA WAILAZA ALGER BAO 1-0

Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria.

Mchezo huo uliopigwa leo majira ya saa 10 Alasiri katika dimba la Uwanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi kutoka Burundi Louis Hazikumana.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa Kila upande kusaka goli la kuongoza lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Mzambia Obrey Chirwa ilishindwa kutumia nafasi walizozipata.

Mpaka mapumziko timu zinaingia vyumbani, matokeo yalikuwa ni 0-0. Kipindi cha pili kilianza kwa MC Alger kulisakama lango la Yanga lakini umakini wa safu ya ulinzi ilikuwa makini na kuondosha hatari langoni mwao.

Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko ya kwanza na kumtoa Deus Kaseke ambapo mabadiliko hayo yanaleta tija na katoka dakika ya 61 Thaban Kamosoku anaipatia Yanga goli la kwanza.

Yanga walianza kubadilika na kuendelea kulisakama goli la MC Alger lakini Chirwa anakosa umakini na kukosa magoli ya wazi.

Baada ya matokeo hayo, mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa April 15 nchini Algeria ambaoo Yanga inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiongoka na mpira mbele ya Mabeki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga inaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimyani na Thaban Kamusoko.
 Wachezaji wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria wakimdhibiti Mshambuliaji wa pembeni wa Timu Yanga, Hassan Kessy, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 Mchezaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijirabu kuchukua mpira mguuni mwa Beki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...