Saturday, April 15, 2017

DUKA LA MTOTO WA DIAMOND LAUNGUA NI LILE LA DUKA LA KISASA LA GSM MALL


 Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
 Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo

 Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto


Na Richard Mwaikenda 

DUKA kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam, linateketea kwa moto hivi sasa.

Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba duka hilo lilianza kuungua majira ya 8;30,Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. 

Magari ya zimamoto na uokoaji yamejazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.

Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana kutoka mkuku kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.

Duka hilo kubwa la kisasa lenye maduka yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na ndani ya jengo hilo kuwa na giza nene lililotawaliwa na wingu la moshi uliosababishwa na moto huo.

Wamejitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini ilishindikana.

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na muwakilishi wa wananchi wakifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo. Wengine ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliani, Profesa Makame Mbarawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa kwa furaha na wasanii mbalimbali wa filamu na wananchi wakati akikagua eneo la ujenzi wa nyumba za makazi baada ya kuweka jiwe la msingi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba wakati bendi ya Msondo Ngoma ikitumbuiza wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

EFM YAKABIDHI PIKIPIKI MBILI SHIKA NDINGA TABATA

 Mshindi wa Pikipiki ya Sanmoto katika shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na Efm Radio kwa Wilaya ya Ilala, Jane Honga akinyosha mkono juu kuonyesha furaha yake mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika shindano hilo katika uwanja wa Tabata Shule.
  Mshindi wa Pikipiki ya Sanmoto katika shindano la Shika Ndinga lililoandaliwa na Efm Radio kwa Wilaya ya Ilala, Jane Honga akitokwa na Machozi
 Mshindi wa Shindano la Shika ndinga ambaye ameweza kujinyakulia pikipiki ya Sanmoto , Amani Juma akishangilia kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo katika Wilaya ya Ilala lililofanyika katika uwanaj wa Tabata shule.
 Mkuu wa Vipindi wa Redio ya Efm 93.7, Dikson Ponela 'Dizo' akikabidhi mkataba wa pikipiki kwa mshindi wa shindano la shika ndinga Wilaya ya Ilala, Jane Honga
 Mtangazaji wa kipindi cha ubaoni Mujuni Silvery 'Mpoki' akiwa na Mtangazaji mwenzie bikira wa Kisukuma katika shoo ya Shika ndinga Tabata Shule
 Wahindi wa shindano la Shika Ndinga  wakiwa wamekalia pikipiki za Sanmoto mara baada ya kukabidhiwa
 Wanawake wakiwa katika hatua ya shindano la kujaza maji hili kwenda hatu ya pili

 Afisa Uhusiano wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ),Aisha Mohamed  akizungumza na Swebe juu ya huduma za benki hiyo
 Maofisa habari wa Efm na waratibu wa shindano la Shika Ndinga , Jesca na Anet wakipanga jambo katika shinadano katika uwanja wa Tabata shule
 Afisa Masoko wa Kampuni ya Property International ,Leila Mahingu akizungumza na wakazi wa Tabata juu ya huduma zinazotolewa na kampuni yake
 Mmoja wa washiriki akibebwa na walinzi mara baada ya kushindw akuendelea na shindano la shika ndinga katika Viwanja vya Taba Shule
 Mzee wa Kizingiti kutoka E.TV  Akitoa burudani kwa wakazi wa Tabata Shule
Washiriki wakiwa wameshika gari wakati shindano likiendelea

Thursday, April 13, 2017

CHUO CHA SHENYANG CHA CHINA YATOA UFADHILI KWA AIR TANZANIA NA NIT

 Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akimkabidhi hati ya ufadhili wa masomo  Mkurugenzi wa shirika la ndege nchini Air Tanzania,Ladislaus Matindi  kwa  ajili ya wafanyakazi wa shirika hilo watakotakiwa kwenda kusoma China
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Chuo kikuu cha shenyang kutoka nchini China kimeahidi kutoa ushirikiano na Shirika la ndege la Aira Tanzania kwa kutoa msaada wa kuwasomesha wafanyakazi wa kampuni hiyohili waweze kumudu ushindani wa soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa malezi wa chuo cha Shenyang, Shi Guangda katika mkutano ulioandaliwa na Tasisi ya Global Education Link kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma urubani  na Masuala ya anga katika chuo hicho.

“tangu Rais wetu wa China alipofika hapa tumekuwa na mahusiano makubwa na na nchi hizi mbili hivyo kwa kuanza kama chuo chetu tutatoa ufadhili kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Air Tanzania na kubadilishana  mafunzo katika chuo cha uasafirishaji cha NIT na Shenyang” Amesema Guangda .

Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Tanzania,Ladislaus Matindi ameishukuru tasisi ya Global Education Link kwa kuweza kuwaunganisha na chuo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa msaada mkubwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa shirika hilo.

Matindi ametaja kuwa upatikanaji wa nafasi hiyo itasaidia kutoa motisha kwa vijana wetu ambao wanafanya kazi katika shirika hilo na wengine ambao wako nje kuwa na hamu ya kusoma masuala ya usafirishaji .

Kwa upande wake mkurugenzi wa Global Education link , AbduMalik Molell alitumia fursa hiyo kuzungumza na wazazi hao juu ya swala la bima ya wanafunzi amabo wanasoma chuo hicho katika swala zima la matibabu na majanga mengine ambayo yatawakuta wanafunzi Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Air Tanzania Ladislaus Matindi akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasoma masuala ya Anga nchini China
 Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akifafanua jambo kuhusu masuala ya bima ya matibabu kwa wazazi ambao wamefika katika mkutano huo
 Mlezi wa wanafunzi kutoka chuo Shenyang, akizungumza juu ya mazingira na ufadhili walio utoa nchini kwa shirika la ndege

 Afisa Biashara mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara upande wa Tantrade, Stephene Kobelo akizungumza na wazazi juu ya namna watoto wanavyotakiwa kuitangaza nchi
 Baadhi ya Wazazi ambao wamefika katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini juu ya swala zima la bima ya matibabu kwa wanafunzi
 Baadhi ya wakurugenzi wa wenza wa Tasisi ya Global Education Link wakisikiliza
 Mmoja wa wazazi akichangia jambo juu ya kuboresha bima ya wanafunzi wanaosoma China
Wazazi na baadhi ya ndugu ambao watoto wao wanasoma nchini China wakifatilia mkutano

KIPINDI CHA 360 KURUSHWA MUBASHARA KUTOKA KATIKA HIFADHI ZA SERENGETI NA NGORONGORO

 Afisa uhusiano wa Tanapa Pascal Shelutete akizungumza na watangazaji wa kipindi cha 360 cha Clouds Tv ambao wamewasili mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya kipindi katika mbuga za Ngorongoro na Serengeti
 Watangazaji wa kipindi cha 360 cha Clouds Tv wakijadili jambo kabla ya kupanda kwenye magari kwa ajili ya kuelekea mbugani
 Watangazaji wa kipindi cha Clouds 360 wakiongozwa na Sam Sasari wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Arusha


Watangazaji wa kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Tv wamewasili mikoani Arusha jioni hii kwa ajili ya ziara katika hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.

Kipindi kilichoendelea kujizolea umaarufu cha 360 kinataraji kurushwa moja kwa moja kutoka katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro na Serengeti kikiongozwa na watangazaji wake Baby Kabaye, Sam Sasali, Hassan Ngoma na James Tupa tupa.


Couple ya washindi ambao wamewasili kwa ajili ya safari katika mbuga hizo za Wanyamapamoja na timu nzima ya 360

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZAIARA KATA YA MASANGA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI, APIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULAMkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku wananchi kuuza mazao ya chakula wanayovuna hususan mtama na badala yake waweke akiba. 
Taraba alipiga marufuku hiyo jana wakati akifanya ziara katika kata za Lagana, Mwamashele, Mwakipoya na Masanga baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kufanya biashara hiyo. 
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masanga alisema kuna baadhi ya watu huwahadaa na kununua mtama kwa bei ya juu hali inayowafanya wananchi wabaki bila chakula. 
“Nasikia hapa kuna baadhi watu wanapita kwenu wananchi na kununua debe moja la mtama kwa shilingi elfu ishirini na tano msidanganyie na kuuza wewkeni akiba,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya. 
Aidha alionya tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yakiwa shambani baada ya kukadiriwa kiasi cha mazao yao kabla ya kuyavuna aliwataka wananchi wakatae kufanya hivyo. 
Kwa upande mwingine aliwataka kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayohimili ukame yakiwemo mtama ili yaweze kustawi na kuwapa chakula. 
Taraba aliwataka wananchi hao kuwatumia wataalamu wa kilimo kwenye kata zao ili kupata ushauri wa kutumia mbegu zilizo bora ambazo zinaweza kuota na kukua kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. Wengine pichani kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe aliowakuta wakifanya kikao cha kujadili maendeleo ya kata, Mwamashele alipokuwa katika ziara ya kutembelea kata tatu. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele.

TFS NA WADAU WAANZA SAFARI YA KUELEKEA MISITU YA AMANI

 Meneja Masoko na Uwekezaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS),Mariam Kobelo akigawa Vipeperushi kwa Wakazi wa Dar es Salaam amb...