Saturday, April 22, 2017

CUF LIPUMBA WAVAMIA CUF MAALIM NA KUZICHAPA MMOJA AKATWA MGUU

 Wanachama wa chama cha Wananchi Cuf wakipambana na wenzao huku wakisaidina na meneja wa hoteli hiyo mara baada ya kuvamia mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika katika Hotel ya Vinna Hotel

wakati mkutano huo unaendelea ndipo kambi nyingine ya Chama cha Wananchi Cuf ilipovamia na kuvuruga mkutano huo na kuzua taharuki kubwa kwa waandishi wa habari na baadhi ya wakazi wa eneo hilo  ambao wapo jirani .

mara baada ya kufanikiwa kuvuruga mkutano huo baadhi ya watu waliokuja kufanya vurugu walikimbia na wengine kubaki ambao wanaonekana pichani kisha kisha kukimbizwa na wanachi wenye hasiara kali na kumjeruhi kwa kumkata maungio ya kisigino ya mguu wake wa kulia .
 Mapambano yanaendelea Mtuhumiwa wa akiwa anapambana

 akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kudhibitiwa na na wananchi kisha kumkata mguu na kushindwa kutembea
 Mtuhumiwa kutoka kambi ya Lipumba amabye amekatwa mguu akiugulia maumivu mara baada ya kujeruhiwa

Friday, April 21, 2017

CHIBU PERFUME YAZINDULIWA DAR

MWAKYEMBE; LOWASA ASAFISHIKIMbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

BODYLINE HEALTH & FITNESS KUFANYA TAMASHA LA MICHEZO KESHO APRILI 22, 2017 JIJINI DAR


Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali  (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017 Mayfair jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.
Kituo cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao.
Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
 Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza watzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
 Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kutunisha misuli wakionyesha umahili wao.

SHIRIKA LA TPDC KUTEKELEZA MIRADI MIKUBWA YA GESI,SOMA HAPO KUJUA


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha wananchi wananufaika na Gesi nchini,Shirika la Maendeleo ya Petrori nchini (TPDC)  kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarajia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya  awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.

“Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.

Aliongeza kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda za usambazaji.

Aidha alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.

Mtandao huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.

Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na mtandao huo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni.


TEMBO ZAIDI YA 20 WAHARIBU EKARI 50 ZA MAZAO

Tembo zaidi ya 20 wamevamia vijiji vya Wenje mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wakitokea nchini Msumbiji ambapo tembo wawili wameuawa na wananchi na kuondolewa meno mawili na kugawana nyama yao huku tembo wengine zaidi ya 30 wakivamia kijiji cha jakika wakitokea Pori la Akiba la Selou na kuharibu zaidi ya ekari 50 za mazao mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa wanyamapori wa wilaya ya Tunduru Bw.Limbega Hassan aliyeongoza kikosi cha askari  wanyamapori waliokuwa wakiangalia usalama wa tembo na wananchi ambapo wananchi wamemng’oa meno mawili tembo mmoja na kuondoka nayo  huku meno mawili ya tembo mwingine yakisalimishwa kituo cha polisi cha Tunduru.

Kaimu Afisa wanyamapori  huyo wa wilaya ya Tunduru anasema kuwa wamewakamata watu watano wanaodaiwa kuhusika na kuwaua tembo wawili na kutoweka na meno huku wekiwatafuta wengine wawili  wawachukulie hatua na pia mikakati ikiwekwa  kuwadhibiti tembo katika vijiji vitano vinavyosumbuliwa na tembo.

Hata hivyo pamoja na makundi makubwa ya  tembo kuingia kwenye vijiji na kuleta taharuki  mkuu wa wilaya Tunduru Bw. Juma Homera amesema kuwa hali ya usalama  iko shwari  askari wanyamapori wamefanikiwa kuwadhibiti tembo hao na hakuna  mwananchi aliyedhurika.

CHANZO: ITV TANZANIA

WATUMISHI SEKTA YA UJENZI WAFUNDWA MOROGORO

 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
 Katibu wa Baraza la Wafanyakazi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ramadhani Msafiri(Wa pili kushoto), akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na Wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
 Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Shukuru Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa Baraza la Wafanyakazi Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani Morogoro.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Wakiimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa  weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa, katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga, ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
"Naliomba baraza hili la wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara kutekeleza majukumu yao  kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano ili kuleta ufanisi", amesema Eng.Nyamhanga.
Aidha, Eng. Nyamhanga amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji kazi wa watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.
Katibu Mkuu Nyamhanga , amelitaka  Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa watumishi ikiwemo kuandaa mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuongeza ujuzi kwa watumishi wa Wizara hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi Bw. Samuel Mticco,  amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote yaliyosemwa katika Baraza hilo  ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi.
Kikao hicho cha siku moja cha Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na mambo mengine kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa.
Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

DKT. GHALIB BILAL KUWA MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA KILL CHALLENGE 2017

MAKAMU wa Rais mstaafu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed  Ghalib Bilal anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni ya Kill Challenge kwa mwaka 2017, kampeni hiyo yenye lengo la kukusanya fedha kwa ajili kusaidia mapambano dhidi ya maambukizi ya vurusi vya Ukimwi.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na virusi vya Ukimwi  nchini (TACAIDS).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo, Makamu wa Rais wa mradi endelevu wa Mgodi (GGM), Simo Shayo amesema uzinduzii huo utafanyika kwenye Hotel ya kimataifa  Kilimanjaro  Hoteli .

‘’Nawakalibisha watu wote kujitokeza katika kuchangia fedha hizi ili zisaidie katika kupambana na maambuzi haya, kwani jukumu la kupambana na ugonjwa huu sio wa serikali peke yake bali hata jamii nzima inahaja ya kujitokeza na kupambana na ugonjwa huu’’Amesema Shayo.

Shayo amebainisha kuwa  katika kampeni hiyo wameshirikiana na wasanii akiwemo Mrisho  Mpoto kwa lengo la kuiamsha jamii ili ijitokeze katika kupambana na vita hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa (TACAIDS)Dkt Leonard Maboko amewasihi Makampuni mengine yaige mfano  wa (GGM) Katika kuhakisha watahakikisha ugonjwa wa Ukimwi unatokomezwa nchini.
Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Mgodi (GGM), Simo Shayo akizungumza na waaandishi wa habari (hawapo pichani) juu uzinduzi wa kampeni ya Kill Challenge kwa mwaka 2017, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko naye akizungumzia Kampeni hiyo katika mkutano ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanamziki maarufu nchini, Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa Kampeni ya Killchalange 2017 amapo amewasihi wasanii wenzake kujitokeza na kuungana naye katika vita ya kupambana dhidi ya maambuki ya virusi vya Ukimwi.leo jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa (TACAIDS) na waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu wa Rais wa miradi endelevu wa Mgodi (GGM) ,Simo Shayo.

RUZUKU YAMPELEKA LIPUMBA MAHAKAMANI

Mgororo wa ruzuku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) unazidi kupamba moto baada ya mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kwenda kuitetea mahakamani.
 
Profesa Lipumba na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Thomas Malima wamefungua maombi Mahakama Kuu wakiomba waunganishwe kwenye kesi iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa CUF, walio upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Katika kesi ya msingi ya ruzuku namba 21 ya mwaka 2017, wadai wanaiomba Mahakama imzuie msajili kutoa ruzuku kwa CUF na imuamuru Sh360 milioni alizozitoa kwa kina Profesa Lipumba zirejeshwe kwenye akaunti rasmi ya chama. 

Wadaiwa katika kesi hiyo ni Msajili wa Vyama vya Siasa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini Profesa Lipumba na Malima wamewasilisha maombi mahakamani nao waunganishwe kwenye kesi hiyo upande wa wadaiwa.
 
Maombi hayo yalitajwa jana na Malima aliieleza mahakama wakiwa viongozi halali wa chama hicho, wanaomba kujumuishwa kwenye shauri hilo kwa kuwa wana masilahi na shauri hilo.
 
Wakili wa CUF upande wa Katibu Mkuu, Juma Nassoro na Wakili wa Serikali, Hang Chang’a waliieleza mahakama kuwa bado hawajapewa hati za maombi hayo.
 
Jaji Wilfred Dyansobela aliamuru waombaji hao (kina Lipumba) kuwapatia nyaraka hizo na amepanga kusikiliza maombi hayo Juni 6, siku ambayo kesi ya msingi itatajwa.

WAANDISHI WA HABARI WA ISLAEL WAHAIDI KUWA MABALOZI WA UTALII WA TANZANIA

 Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachiakiaga na kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Islael ,Ronit Hershkovitz kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao


 kiongozi wa kundi la Waaandishi wa habari na watali kutoka nchini Islael ,Ronit Hershkovitz  akizungumza  na vyombo vya habari vya hapa nchini kabla ya kuondaka kurudi nchini kwao
 Afisa Habari Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Pascal Shelutete akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati akiagana na kundi hilo la Watalii kutoka nchini Islael
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kundi la Waandishi wa habari kumi na Muigizaji mmoja kutoka nchini Islael lililokuja katika utalii wa Maeneo mbalimbali nchini limeondoka leo  mara baada ya kumaliza ziara yao ya siku tano nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kundi hilo ambalo lilitembea sehemu mbalimbali nchini limewasili jijini Dar es Salaam leo kutoka Kigoma na linataraji kuondoka nchini leo majira ya saa tisa kurudi nchini kwao kwa ndege maalumu ya kukodi.

“Waandishi hawa wa Habari waliofika kufanya utalii nchini ni moja ya matunda yaliyotokana na Rais John Pombe Magufuli kurudisha Diplomasia baina ya Islael na Tanzania mara tu walipofungua ubalozi wao hapa nchini hivyo watalii hawa walipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Visiwa vya Zanzibar na Hifadhi ya Sokwe iliyopo Gombe mkoani Kigoma” Amesema Devotha

Kwa upande wake afisa habari wa Shirika la Hifadhi ya Taifa nchini (TANAPA), Pascal Shelutete amesema kuwa watalii hao wamepata kujionea vivutio vingi sana hapa nchini na kusema kuwa kweli nchi hii inahitaji kuitwa nchi ya Asali na Maziwa kama ilivyo kwao.

Amesema kuwa watalii hao wamefuraishwa na jinsi uoto wa asili ulivyo hifadhiwa hapa nchini na kikubwa zaidi kuona sokwe ambao kisayansi inasemekana kuwa wana mahusiano makubwa na wanadamu kwa asilimia 98% .

Kwa uapande wake kiongozi wa kundi hilo la watalii hao, Ronit Hershkovitz, amesema kuwa amefurahishwa sana na vivutio vilivyopo hapa na kwa sasa kundi hilo linakwenda kuwa mabalozi kwa watalii wengine wanaotoka ukanda wa Magharibi hasa nchi za Mashariki ya kati.

TGNP yatoa mafunzo ya Jinsia kwa Club ya Wanafunzi Sekondari ya Makumbusho

[caption id="attachment_78740" align="aligncenter" width="800"] Mwezeshaji wa Mafunzo ya Uraghibishi Shule ya Sekondari Makumbusho, Janet Mawinza (kulia) akitoa mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho yaliyotolewa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) katika shule hiyo.[/caption]   [caption id="attachment_78742" align="aligncenter" width="800"] Mwezeshaji wa Mafunzo ya Uraghibishi Shule ya Sekondari Makumbusho, Janet Mawinza (kulia) akisisitiza jambo katika mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho yaliyotolewa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) katika shule hiyo.[/caption]   [caption id="attachment_78747" align="aligncenter" width="800"] Mwalimu Mlezi wa Kituo cha Shule ya Msingi Mchangani, Goodluck Busago (kulia) akiwasilisha mada katika mafunzo ya Mafunzo ya Siku Tatu ya Masuala ya Kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho yaliyotolewa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) katika shule hiyo.[/caption]   [caption id="attachment_78741" align="aligncenter" width="800"] Mmoja ya wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho akichangia mada katika mafunzo hayo.[/caption]   [caption id="attachment_78743" align="aligncenter" width="800"] Mmoja ya wanafunzi (kushoto) wanaoshiriki mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho akichangia mada katika mafunzo hayo.[/caption]   [caption id="attachment_78745" align="aligncenter" width="800"] Mmoja ya wanafunzi (kushoto) wanaoshiriki mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho akichangia mada katika mafunzo hayo.[/caption]   [caption id="attachment_78746" align="aligncenter" width="800"] Mmoja wa wageni waalikwa kutoka katika vituo vya taarifa na maarifa akichangia jambo kwa washiriki mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho.[/caption]   [caption id="attachment_78748" align="aligncenter" width="800"] Picha ya pamoja kati ya wawezeshaji, wageni waalikwa na wanafunzi wanaoshiriki mafunzo ya kijinsia kwa Club ya Jinsia ya Wanafunzi wa Sekondari ya Makumbusho.[/caption]

ZURICH GROUP, JUBILEE INSURANCEWAZINDUA BIMA MPYA YA GHARAMA NAFUU 'AFYA WOTE'

  Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.

 Na Ripota wa mafoto Blog, Dar
WITO umetolewa kwa  wananchi wa kipato cha chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni  kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali wananchi wa aina zote.

Aidha alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.

Bima hiyo imelenga zaidi kuwafikia wananchi wote haswa wale waso na kipato kikubwa na wa kipato cha kati ili wote wanufaike na huduma za afya.
Mbanga alitoa wito kwa wananchi wengi kutumia fursa hiyo ili kuweza kuwekeza fedha ambazo wanazitumia kwa matibabu kwaajili ya mahitaji mengine ya kiuchumi.

“Pamoja na kwamba kuna sera mbalimbali za afya zinazozungumza juu ya upatikanaji wa huduma za afya kwa njia rahisi, lakini bado bila bima ya afya wagonjwa wengi watapoteza  maisha kwa sababu kuna watanzania  wengi ambao hali za kipato chao sio nzuri.

Ni vyema wananchi wengi wakajiunga na mfuko huu wa bei nafuu ili kile kiasi kilichokuwa kikitumika kufanya matibabu wakiwekeze kwenye shughuli nyingine za uchumi,”alisema.

Aidha alisema asilimia 27 tu, ndio wamejiunga na mfuko hivyo kuna wananchi wengi ambao hawajajiunga na mfuko huo.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Group na Zurich Insurance Brokers (EA) Sudi Simba alisema, huduma hiyo ilianzishwa mwezi Aprili mwaka jana, lengo likiwa ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini na kati, ambapo kwa kila familia ya watu wanne wataweza kukatiwa bima kwa sh.174,000 tu.
“Watu hawa ni baba, mama na wategemezi wao ambao ni watoto chini ya miaka 18 .
Bima hii kama kuna uhitaji wa kuongeza wengine unapaswa kulipia sh. 100,000 kwa mwaka kwa kila atakaeongezeka,”alisema.  
 Khadija Kopa na kundi zima la bendi ya TOT wakitoa burudani na kuimba wimbo maalum uliotungwa nao kuhusu Bima hiyo mpya. 
Mgeni rasmi akihojiwa na waandishi baada ya uzinduzi huo.

TAMASHA LA WASANII WILAYA YA TEMEKE KUPAMBWA NA PATRICIA HILLARY

CHAMA Cha waigizaji Mkoa Temeke  kimeamua kukusanya  waigizaji wote waishio Dar es salaam wilaya ya temeke. Akizungumza n...