Saturday, April 29, 2017

WAWILI WAONDOKA NA PIKIPIKI SHIKA NDINGA BAGAMOYO

 Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo juu Shindano la Shka Ndinga ambalo limeweza kuwazawadia washindi wawili pikipiki aina ya Sunmoto  mara baada ya kufanikiwa kupita katika vipengele vyote katika shindano lililofanyika shule ya Msingi Majengo Bagamoyo
 Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi akikabidhi  Pikipiki kwa mshindi kwa upande wa kina Dada Kawale Halidy  ambaye ameweza kuondoka na pikipiki ya SUNMOTO
 Meneja wa Matukio na Mawasiliano wa Efm Radio, Neema Ukurasi akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa Mshindi wa Shika Ndinga upande wa Wanaume , Valerian Gilbert katika shindano lililofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Majengo Bagamoyo
 Said Magongo akimbusu mkewe Kawale Halidy mara baada ya kufanikiwa kuondoka na pikipiki ya Sunmoto katika shindano la shika ndinga lililofanyika mkoa wa Pwani Wilaya ya Bagamoyo.
 Washiriki upande wa kina Dada wakiwa katika zoezi la mbio za kukimbia na vikombe vya maji
 Mchekeshaji kutoka Efm akitoa burudani kwa wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo
 Washiriki wa shika ndinga upande wa Wanaume wakiwa katika hatua ya kujaza vikombe na kukimbia navyo
 Msanii wa michezo ya Sarakasi za Baiskeli , Junior Talent akiwa amekaa juu ya Baiskeli kwa satili isiyokuwa ya kawaida na kuwashangaza wakazi wengi wa Bagamoyo

 Majaji wakimshusha mmoja wa washiriki katika kipengele cha mwisho cha Shindano la Shika Ndinga
 Washiriki upande wa kiume wakiwa wameshikilia gari kisawa sawa katika hatua ya mwisho ya shindano hilo
Mmoja wa Watangazaiwa EFM radio akizungumza na wakazi wa bagamoyo walifurika katika kiwanja cha Shuleya msingi Majengo

NAIBU SPIKA TULIA AKSON AZINDUA MAFUNZO YA SANAA TASUBA

 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson   akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Vikundi vya ngoma za asili kutoka mkoa mbeya yanayofadhiliwa na Tulia Trust.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson, akiimba wimbo na Msanii wa muziki wa Bongo fleva , Nandy pamoja na Mtendaji mkuu wa chuo Cha Sanaa Bagamoyo,Herbert Makoye .
 Moja ya kazi za Sanaa zilizochorwa katika chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA)
 Mmoja wa Wanafunzi  kitengo cha Sanaa za ufundi na uchoraji wakichora picha ya  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia AksonNa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

 TAASISI ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson imewafadhili wanafunzi 27 kwa ajili ya kupata mafunzo ya sanaa.

Taasisi hiyo imewadhamini wanafunzi hao kutoka Mbeya kusoma kwenye chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Wanafunzi hao watapata fursa ya kujifunza sanaa ya maonyesho ya upigaji ngoma za asili, maigizo na utumiaji jukwaa.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kuwakabidhi wanafunzi hao chuoni hapo, Dkt. Tulia amesema lengo la kuwafadhili vijana hao ni kutokomeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Amesema taasisi yake imedhamilia kukuza sanaa kwa vijana nchini ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza ufanisi kwenye vipaji vyao walivyokuwa navyo awali.

Alisema vijana hao wakipata mafunzo kwenye chuo hicho wataweza kufanya shughuli zao za ngoma za asili kiutaalamu zaidi, hali itakayowaongezea kipato na kuwafungulia fursa nyingi.

Dkt. Tulia alisema zoezi la kuwafadhili vijana kusoma kwenye chuo hicho litakuwa endelevu ili kukuza vipaji vya vijana kwenye sanaa.

Alisema baada ya awamu ya kwanza kumalizika atahakikisha anaongeza idadi ya vijana atakaowadhamini kwa ajili ya kukuza vipaji vya sanaa nchini hususani kwenye mkoa wa Mbeya.

Tulia, alisema atahakikisha kwenye awamu ya pili atachukua wanawake wenye vipaji ili kuendeleza vipaji vyao kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

"Huu hautakuwa mwisho wa kufadhili vijana, nitahakikisha naongeza idadi ya vijana kwenye awamu ya pili. Juhudi hizi zitahakikisha zinasaidia vijana wanaepuka tatizo la ukosefu wa ajira nchini," alisema Tulia.

Aidha, Dkt. Tulia amewataka wadau mbalimbali wa sanaa, Taasisi na Kampuni kuunga mkono juhudi za taasisi yake kwa ajili kukuza sanaa nchini.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dkt.Herbert Makoye, alisematahakikisha chuo chake kinawapa mafunzo mazuri vijana hao ili kuwaongezea ufanisi kwenye vipaji vyao.

Alisema watahakikisha wanawapa mafunzo mazuri ya uchezaji ngoma za asili, ngoma za ubunifu, muziki wa asili ya Tanzania, uigizaji, matumizi ya jukwaa na maleba.

Dkt Makoye, alisema ana imani vijana hao wakihitimu mafunzo hayo watakuwa tofauti na walivyokuwa hapo awali.

Mafunzo hayo yatadumu kwa kipindi cha miezi miwili watakaofuzu wataendelea na kozi ya cheti na diploma kwa ajili ya kukuza vipaji vyao.

 Mtendaji mkuu wa chuo cha Sanaa Bagamoyo(TASUBA) akizungumza kumkaribisha  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson akiwasili katika chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa jili ya ufunguzi wa mafunzo kwa vikundi vya Sanaa mkoa  mbeya.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson,  akicheza ngoma pamoja na Mtendaji mkuu wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo , Dk Herbert Makoye

Friday, April 28, 2017

MISS GRAND TANZANIA 2017 YAZINDULIWA

 Mratibu wa Shindano la Miss Grand  Tanzania , Rasheedah  Jamaldin akizungumza na Waandishi  juu ya uzinduzi shindano la urembo litakalo tambulika kama Miss Grand Tanzania  2017 linalo taraji kuanza mwezi wa sita mwaka huu kwa kuanza mchujo kuanzia ngazi ya vitongoji mpaka Taifa .
 Meneja Matukio wa Miss Garand  Tanzania 2017 ,Abraham Mahimbo akizungumza na waandishi jisni mawakala watakavyohusika katika kuwapata warembo nchi nzima
Waandishi mbalimbali waliofika katika mkutano huo wa uzinduzi wa shindano la Miss Garand 2017 jijini Dar es Salaam leo

Thursday, April 27, 2017

FAHAMU KUHUSU KODI YA PANGO LA ARDHI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Kumekuwa na sitofahamu kubwa sna kwa watu wengi wanaomiliki ardhi na nyumba mijini na vijijini juu ya kodi ya ardhi  inayotakiwa kulipwa Wizarani .

Leo nimefanikiwa kuzungumza na Mmoja wa watendaji kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Denis  Masami na kuzungumzia juu ya hii kodi ya ardhi.
Denis anasema kuwa  Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  ilikasimiwa zoezi la kukusanya kodi na tozo mbalimbali  zinazotokana na sekta ya ardhi   kuanzia mwaka  wa fedha  1996/1997.

Awali kodi hizi zilikuwa zikikusanywa na Serikali Kuu kabla ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Kodi ya ardhi ni tozo/maduhuli  yanayokusanywa na Serikali katika kipande cha ardhi au shamba kwa mjibu wa Sheria ya Ardhi  Na. 4 ya mwaka 1999,Katika fungu la 33 (1) Sheria hiyo inatoa wajibu kwa mmiliki wa  ardhi kulipa kodi ya pango la ardhi  kila mwaka dhana hii inatokana na Sheria ya Ardhi No. 4  ya mwaka 1999 katika fungu la 3 kifungu kidogo cha 1 (a) kinachosema:
 ‘Itambulike kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Umma iliyowekwa chini ya Mheshimiwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi
Denis anasema kuwa hivyo sera ya ardhi ya mwaka 1995 imempa mamlaka Mh. Rais kumiliki ardhi kwa niaba ya wananchi, na wananchi wamepewa haki ya kutumia ardhi kwa masharti ya sheria.

Anataja kuwa mfumo huu wa umiliki wa ardhi unatambulika kama lease hold na sio free hold. Kwa mantiki hii aina hii ya umiliki yani lease hold ni upangaji katika ardhi ambao mpangaji anawajibika kufata masharti ya upangishaji na mojawapo ya masharti hayo ni pamoja na kulipa pango la kipande cha ardhi.

Anasema  hii ni tozo na sio kodi.  Mfano mmiliki na mpangaji wa nyumba. Mmiliki ni Rais kwa niaba ya umma na mpangaji ni mwananchi  kwa mujibu wa fungu la 33 cha Sheria ya Ardhi Na.4  ya Mwaka 1999
Anasema Kodi hii inalipwa katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja kuanzia julai mosi  hadi Desemba bila tozo na kuanzia Januari  ikiwa na riba ya 1% kila mwezi mpaka itakapolipwa (fungu 33 (11).

“Kodi hii hulipwa kwa Kamishna wa Ardhi au Afisa Ardhi Mteule katika  Halmashauri na Manispaa zote nchini kwa mujibu wa fungu la 33 (4) cha Sheria ya Ardhi Na.4  ya Mwaka 1999 vigezo vinavyo zingatiwa ukubwa wa kipande cha ardhi(  The area of land).Matumizi ya  ardhi inayolipiwa (use of the land) thamani ya ardhi (value of the land Kiwango cha malipo ya mbele (premium )”amesema Denisi

Anasema kuwa kwa mujibu wa fungu la 33 (2),(6) cha Sheria ya Ardhi Na.4  ya Mwaka 1999 Kamishna wa ardhi amepewa mamlaka ya kuhuhisha viwango katika kipindi chochote anapoona inafaa lakini isiwe chini ya kipindi cha miaka 3.

Anataja kuwa viwango vinavyotumika vimesha huishwa : 1996, 2006, 2012  na 2015 kwa mujibu wa fungu la 50 la  Sheria ya Ardhi Na.4  ya Mwaka 1999 ikiwa mmiliki wa ardhi atakaidi kulipa kodi kwa wakati basi Kamishna /Afisa Mteule  atachukua hatua zifuatoazo.

1.Kuandaa na kupeleka hati ya madai kumtaka  mdaiwa kulipa kodi hiyo ndani ya siku 14
2.Baada ya siku 14 kupita bila mdaiwa kulipa, Kamishna /Afisa mteule atawasilisha nakala ya hati ya madai katika baraza la Ardhi au Mahakama ya Wilaya.
3.Ikisha pokelewa  na mahakama (filed) sheria  inasema itakuwa hukumu(decree) imepita dhidi ya mdaiwa wa kodi ya pango la ardhi.
4.Kamishna /Afisa Mteule  atawasilisha maombi ya kukazia hukumu (application for  execution ) dhidi ya mdaiwa.
5.  Baada ya kuyasikiliza maombi hayo  mahakama itamteuwa dalali kuendelea na hatua za kukazia hukumu.
6.Dalali atakaye teuliwa lazima awe katika arodha ya madalali waliopata kibali cha udalali wa mabaraza/mahakama husika.

Anasema Baada ya kupokea amri ya kukamata mali dalali atatuma ilani ya siku 14 ya kukamata mali /kiwanja cha mdaiwa wa kodi kama kodi na tozo hazijalipwa dalali  ataomba kibali cha mahakama/baraza kuuza mali/kiwanja alicho kamata.
Anasema kuwa atatangaza katika gazeti lolote la serikali kusudio la  kuuza/mnada akitaja tarehe,mali/kiwanja hivyo taratibu za mnada zitaendelea terehe na mahali husika  na baada ya mauzo hayo  fedha iliyopatikana itawasilishwa katika baraza/mahakama  ili kulipia deni .

Anataja kuwa kiasi kinacho bakia kitalipa gharama za dalali na bakaa atarejeshewa mmilki wa mali iliyonadiwa baadhi ya wamiliki kuchanganya kati ya kodi ya pango la ardhi  na kodi ya Majengo

Anaweka wazi kuwa hatua za kisheria zinachukua muda mrefu sana  hivyo kuchelewesha zoezi zima tatizo la kumbukumbu kuwa baadhi ya wadaiwa wanalipa lakini hawafiki kuhuhisha kumbukumbu hivyo wakati wa kutekeleza zoezi hilo wanajitokeza hatua za mwisho kabisa

Denisi anasema kuwa Kati hali hiyo inapoteza muda na lasilimali fedha nyingi bila ya manufaaa kutokana na Sheria ya Ardhi Namba 4. ya mwaka 1999 inasimamiwa na Kamishna wa Ardhi/Afisa Ardhi Mteule

Anasema fedha hii Inalipwa kwa kila kipande cha ardhi/shamba ilioendelezwa ama isiyoendelezwa na Inalipwa kila Julai mosi. Hii ni tozo na sio kodi

KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WASICHANA 25 KUTOKA SHULE MBALIMBALI NCHINI

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla,amewatunuku vyeti wanafunzi wa kike 25 wa shule mbalimbali za sekondari waliofanya vizuri katika mafunzo ya uchambuzi wa takwimu.

Dk.Kigwangallah ametoa vyeti hivyo leo kwa wanafunzi hao baada ya mafunzo ya siku tatu ya namna ya kutumia takwimu.

Mafunzo hayo yameandaliwa na kufadhiliwa na DataLab-dlab kwa kushirikiana na UDICTII,Apps& Girls and She Code for change na yamelenga kuwajengea uwezo kwenye eneo la kutumia takwimu,  kuzitafsiri na kuziweka kwenye taarifa ambazo zinaweza kutumika na walaji kama vile wanahabari, wabunge, watunga sera na wengine wenye uhitaji.

Dk. Kigwangallah amewapongeza waandaji na kueleza kuwa yatawajenga watoto kwenye utamaduni wa kutumia takwimu.

Mkuu wa Mafunzo wa Mradi wa Takwimu, Tanzania, Mahadia Tunga, ambaye ni Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo ya uchambuzi wa takwimu kwa watoto wa kike sababu mara nyingi mwamko wao huwa ni mdogo tofauti na wanaume.

Amesema kuwa  mafunzo hayo wanayatoa kwa watoto kuanzia umri wa miaka 15 hadi 20 ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto na kuzipatia ufumbuzi.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Tehama kwa wasichana yaliyoandaliwa na tasisi ya Tanzania Data Lab
 Wasichana Walioshiriki katika Mafunzo wakifatilia hotuba ya Naibu waziri
 Mhitimu kutoka Shule ya Sekondari Jangwani , Sheila Juma akizungumza na juu ya programu yake amabyo ameigundua mara baada y kufanya mafunzo kutoka Tanzania data Lab
 Mmoja wa Washiriki katika mafunzo hayo,  Necta Richard akizungumza  juu ya progamua mabyo ameizindua mara baada y kupata mafunzo

Mkuu wa Mafunzo kutoka Tanzania Data Lab , Mahadia Tunga akizungumza na Washiriki waliopata mafunzo hayo

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Zawadi kwa Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa ambaye ni mshindi wa kwanza wa Data Innovation , Asha Abbas
 Caroline Ndosi akizungumza na Washiriki 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya tehema kutoka Tanzania Data Lab

Rais Magufuli mgeni rasmi Siku ya Uhuru wa Habari Duniani

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Makamu Rais wa UTPC, Bi. Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandushi Dar es Salaam akizungumza katika mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanahabari na wageni waalikwa wakiwa katika mkutano na Kamati ya maandalizi ya WPFD-2017 kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 78899" align="alignnone" width="1000"]  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza katika mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.[/caption] RAIS wa Tanzania Mh. Dk John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani(WPFD) inayotarajia kufanyika mkoani Mwanza. Maadhimisho hayo ya siku mbili yaani Mei 2 na 3, 2017 yanatarajia kuwakutanisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari kujadili masuala mbalimbali ya tasnia ya habari. Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari uliyoshirikisha wadau mbalimbali walioshiriki kufanikisha maandalizi hayo, walisema maadhimisho ya WPFD kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza na yatafunguliwa na mgeni rasmi, Rais Dk. John Magufuli pamoja na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii. Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari ambao ni waratibu wa maadhimisho hayo, alisema Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yanayotarajia kufanyika yanabeba maana kubwa kwa wanahabari na wadau wa vyombo vya Habari Duniani kutokana na umuhimu wa tasnia yenyewe. Alisema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwani hakuna taifa linazoweza kuendelea na kuwa na ustawi bila ya uhuru wa vyombo vya habari. Alisema vyombo vya habari ndivyo vinavyotoa mchango wa kuibua uozo na hata kuleta uwajibikaji maeneo mbalimbali ambapo serikali nayo uweza kuchukua hatua.    Katibu wa TEF, Neville Meena akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017. Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano na Kamati ya maandalizi ya WPFD-2017 kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.[/caption]   Alisema wanahabari hawana budu kufanya kazi kwa uhuru huku wakizingatia sheria na kujali usalama wao katika utendaji wa kazi ili kuepuka madhara yanayoweza kuhatarisha usalama wa wanahabari. "Wanahabari waliofanikiwa kupata mafunzo ya usalama kazini wayatumie vizuri ili kuepuka madhara maana yakitumika vizuri yanasaidia," alisema Bi. Kitomari. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga alivitaka vyombo vya habari kubadilika na kuanza kujipangia vipaombele vya kufanya kazi na kuacha utaratibu wa kufanya kazi kwa kufuata mkumbo wa matukio. Alisema umefika wakati vyombo vya habari kujipangia agenda za kuzifanyia kazi na kuacha kuwasubiri wanasia kuvipangia vyombo hivyo. Jumla ya washiriki 250 kutoka ndani na nje ya Tanzania ikiwemo mitandao ya kijamii imealikwa kushiriki katika mkutano huo. Washiriki wengine ambao wamefanikisha WPFD-2017 ni pamoja UNESCO, TMF, UTPC, TEF, TAMWA, MCT, MOAT, Internews, UNIC na UNICEF.   Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano na Kamati ya maandalizi ya WPFD-2017 kutambulisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

UBA YATOA VYETI KWA WANUFAIKA WA RUZUKU

 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akizungumza na wanufaika wa mradi wa Tony Elumelu Foundation kuandika mawazo ya biashara ambao wapo hapa nchini juu ya namna watakvyoweza kushirikiana na Benki ya UBA katika kukuza biashara zao mpaka nje ya mipaka ya Tanzania
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi cheti kwa Hurbert  Mwashiuya juu kama mnufaika wa mradi mara baada ya kupata ruzuku 
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akikabidhi  cheti kwa Bi , Aika Mtei kma mmoja wa wanufaika wa ruzuku mara baada ya kuandika mradi juu ya biashara katika mtandao
 Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwaeleza watendaji wa Benki ya UBA juu ya umuhimu wa kuwasaidia wanufaika hao hili waweze kuwa mfano kwa wengine
Mkurugenzi wa Bank ya UBA Tanzania, Peter Makau akiwa katika picha ya pamoja na wanufaika na baadhi ya watendaji wa beki hiyo

Sunday, April 23, 2017

Harusi ya John Focus na Bi. Bernadetha Munishi ilivyofana


Bwana harusi, John Focus Lyimo akimlisha ndafu mkewe kwenye hafla ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni kabla ya hafla hiyo.

Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akimlisha keki mumewe John Focus Lyimo kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Harusi yao ilifungwa katika Kanisa Katoliki la Mt. Rita wa Kashia, Kimara Temboni.

Bwana harusi, John Focus Lyimo (katikati) akiandaa ndafu maalum kwa ajili ya kumlisha mkewe ikiwa ni ishara ya kumkaribisha nyumbani mara baada ya ndoa yao. Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi pamoja na wapambe wao wakiwa kwenye hafla hiyo.

Bwana harusi, John Focus Lyimo (wa pili kushoto) akimtambulisha mkewe Bi. Bernadetha Munishi (wa pili kulia) kwa wageni waalikwa kwenye hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam. Waliokaa ni wapambe wa maharusi.

Dada na mashemeji wa bwana harusi...

Bwana harusi, John Focus Lyimo (kushoto) akipita meza hadi meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.

Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi (kulia) akipita meza kwa meza kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki hafla kabambe ya harusi yao iliyofanyika Ukumbi wa 'Mwenge Social Hall' jana jijini Dar es Salaam.

Maharusi wakiwaongoza wageni waalikwa kwenye maakuli...

Wanajumuiya wenzake na bwana harusi, John Focus Lyimo kutoka Temboni wakiongozwa na Mr&Mrs Msafiri wakishiriki katika hafla hiyo.

Kulia ni MC Leopold Sondoka (mwenye kipaza sauti) akitoa maelekezo kwa Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi kwenye hafla hiyo.

Wazazi wa Bwana harusi wakiongozwa na mwakilisha wa Baba ndg, Pius Elias (kushoto) wakizungumza machache kwenye hafla hiyo.

Wazazi na ndugu wa bibi harusi wakipata picha ya ukumbusho.

Familia ya bwana harusi ikiongozwa na mwakilisha wa baba ndugu, Pius Elias wakigonganisha glasi kwa furaha

Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi wakionesha furaha yao kwa kugonga chiaz...

Baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya harusi hiyo wakigonga chiaz kwa furaha kubwa baada ya kufanikisha shughuli hiyo. Kutoka kushoto ni Mrs. Machonchoryo na Mrs Oscar Munishi.

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi wakiwalisha vipande vya ndafu 'mades' wao kama ishara ya kuwashukuru.

Wanakamati wakinyanyua keki waliopewa na maharusi kama shukrani kwa kujitoa na kufanikisha hafla hiyo...

Maharusi, John Focus Lyimo na mkewe Bi. Bernadetha Munishi (kushoto) wakimkabidhi keki ya asante Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia).

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Bw. Oscar Munishi (kulia) akiwatambulisha wajumbe mbalimbali wa kamati yake.

Meza ya wazazi wa bibi harusi Bi. Harusi Bernadetha Francis Munishi

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI.

NA MWANDISHI WETU Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo ...