Saturday, May 6, 2017

LUKUVI ; NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHINa Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa nyumba ardhi na Manedeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema ataendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao watakwenda kinyume cha sheria katika umiliki wa ardhi hapa nchini.

Lukuvi  alitoa kauli hiyo Mbele ya Rais Dk .John Pombe Magufuli alipokuwa kaijibu hoja za baadhi ya wajumbe wakati wa uzinduizi wa  baraza la wafanyabiashara nchini  ambao walizungumzia mambo kadhaa ya urasimu uliopo katika ardhi.

“kuna tatizo sana katika umiliki wa ardhi yetu hasa haya mashamba makubwa kuna baadhi ya watu wamechukua mashamba makubwa na kwenda kukopa katika mabenki na ukija katika hayo mashamba hakuna ambacho kimewekwa shambani kulingana na mikopo yao hivyo sasa sitasita kumchukulia hatua mtu yoyote ambaye atakwenda kinyume na na Sheria za ardhi kwa kumnyang’anya hati yake na kuirudisha serikalini” amesema Waziri Lukuvi.

Lukuvi ameweka wazi kuwa yupo radhi kutoa ardhi yenye hati ndani ya siku moja  kwa mtu yoyote anayetaka kuwekeza viwanda hapa nchini na sio wababaishaji ambao wamegeuza ardhi kama mtaji wa kununulia mabasi kwa kukopa kwenye mabenki.

Alimaliza kwa kusema kwa sasa wizara yake imeandaa vitabu ambavyo vinaonyesha watu wote wale ambao wanamiliki ardhi bila ya kufanya shughuli yoyote .


 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania , Beno Ndulu
wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Friday, May 5, 2017

UTAFITI: KAYA 1000 DAR KUPIMWA UKIMWI.


http://www.newsportal.sg/wp-content/uploads/hiv-testing.jpgNa Veronica Kazimoto, NBS-DAR

WITO umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao kaya zao zimechaguliwa kitaalamu kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 kutoa ushirikiano kwa wadadisi wataokusanya taarifa za utafiti huo.

Utafiti huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alitoa rai hiyo hivi karibuni jijini humo alipozungumza kwenye mkutano uliohusisha wadau wa utafiti huo.

Alisema utafiti huo ni wa muhimu kwani husaidia kujua hali halisi ya ugonjwa wa UKIMWI na hivyo kuongeza nguvu zaidi ya kuondokana na ugonjwa huo.
 Image may contain: 2 people, people standing and hat
"Kwa kuwa utatusaidia kujua hali halisi ya maambukizi ya VVU na hatimaye kupata nguvu zaidi za kuondokana na ugonjwa huu, hivyo nawaagiza kusimamia zoezi hili na kuwahimiza wananchi wote ambao kaya zao zimechaguliwa kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaofanya taarifa za utafiti huu",  alisema Mjema (anayezungumza pichani).

Alifafanua kwamba, utafiti huo ni wa kwanza kukusanya taarifa zinazohusiana na maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU na wastani wa maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote pamoja na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count).
 https://afyamd.files.wordpress.com/2016/12/arvs.jpg?w=800
Aidha, utafiti huu utapima uwepo wa viashiria vya usugu wa dawa, kiwango cha maambukizi ya kaswende pamoja na homa ya ini (Hepatitis B).

Akizungumzia kiwango cha maambukizi ya VVU katika tafiti zilizopita, Mkuu wa Wilaya huyo alisema maambukizi yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011 na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizi ya nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo nchi nyingi za ukanda huo zina kiwango cha zaidi ya aslimia 10.Image may contain: 1 person, standing
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Grace Magembe alisema wananchi watakuwa na hiari ya kukubali kupima ambapo kwa wale watakaogundulika kuwa na maambukizi, watapata rufaa ya kwenda kupatiwa matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya.

"Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI hauhusishi watu wote bali ni kaya chache tu ambazo zimechaguliwa kitaalam ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine na kwa hapa Dar es Salaam kaya zilizochaguliwa hazizidi 1000", alisema Dk. Magembe.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Utafiti wa aina hii ni wa mara ya nne (4) kufanyika nchini Tanzania ambapo wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili mwaka 2007 na wa tatu mwaka 2011.

Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 /17 unafanyika nchini, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).

Kanuni uendeshaji mitandao ya kijamii kukamilika mapema- Dk Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na meza kuu kwenye maadhimisho hayo akizinduwa taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi. Anaye msadia kushoto ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya MISA TAN. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi mbalimbali waliopo meza kuu wakionesha baadhi ya nakala za taarifa ya "So This Is Democracy" ya MISA TAN mara baada ya kuzinduliwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza juzi. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Mwakyembe kuzungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi. Mwanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho akizungumza kuwasilisha ujumbe wa TAMWA kwenye kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi. Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akizungumza katika kadamnasi hiyo. Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akizungumza kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.[/caption] WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaharakisha kukamilisha kwa kanuni zitakazo simamia mitandao ya kijamii inayoendesha shughuli zake kama vyombo vya habari vya kieletroniki (Tv na Redio). Waziri Dk. Mwakyembe aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari na wanataaluma wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani zilizofanyika kitaifa mkoani Mwanza. "Hii media nyingine hii ambayo inafanya kazi zilezile kama za vyombo vya habari vya eletroniki, lakini nadhani tulikuwa hatujaamka kutunga kanuni, lakini nauhakika ndani ya muda si mrefu hilo litafanyika...lakini litakuwa zoezi shirikishi kama nilivyo ahidi...," alisema Waziri Dk. Mwakyembe. Hata hivyo aliwataka wananchi kutumia taarifa za kwenye mitandao kwa tahadhari na kama tetesi ili kuondoa mikanganyiko ambayo imekuwa ikitokea kwenye mitandao hiyo. Kwa upande wake Mtaalamu wa Mawasiliano, Innocent Mungy akiwasilisha mada ya 'Mchango wa Mitandao ya Kijamii katika kukuza Uhuru wa Kujieleza' kwenye kongamano hilo ilisema mitandao ya kijamii kupitia intaneti imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano licha ya uwepo wa changamoto zake. Alisema mitandao kama blogu imekuwa ikisambaza taarifa kwa kiasi kikubwa na kutumiwa na idadi kubwa ya watu nchini katika kupata taarifa. "Bloggers wamekuwa sehemu kubwa ya mawasiliano...hadi taasisi mbalimbali zimeona umuhimu wake nazo zimeingia na kuwa zikitumia mitandao hiyo katika kutoa taarifa...," alisema mtaalamu huyo wa mawasiliano nchini. Akifafanua alisema kutokana na wimbi la kukua kwa mitandao hiyo na kusambaza taarifa wakati mwingine imekuwa vyanzo vya taarifa hata katika vyombo rasmi vya habari. Alisema licha ya mafanikio hayo mitandao hiyo imekuwa na changamoto kubwa ikiwepo uwepo wa taarifa za uongo kupitia mitandao hiyo, matumizi mabaya ya mitandao hiyo. Aidha akijibu moja ya swali lililoulizwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii (TBN) juu ya mvutano wa mitandao ya kijamii 'Blogu' na vyombo rasmi vya habari kuchukuliana taarifa basipo utaratibu kwa pande zote, alizitaka pande zote kukaa na kuzungumza kwa pamoja kuangalia namna zinaweza kutatua mvutano huo wa chini chini kwa maendeleo zaidi ya tasnia. "...Nianze kwa kupongeza kuwa kwa sasa bloga wanavyofanya kazi kunamabadiliko makubwa ukilinganisha na hapo nyumba, sasa hivi hadi wao (bloggers) wanaumoja wao unaowaunganisha (TBN). Kaeni chini mzungumze naamini mtayamaliza, mnaweza kuwatumia hata waandishi wa habari wakongwe na hata bloga wazoefu ili kumaliza mgogoro huo wa chini chini na vyumba vya habari," alisema. Hata hivyo alisema kuwa mitandao ya kijamii sio mibala bali watumiaji wake ndio wabaya na kuongeza mitandao hiyo imekuja na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano.   [caption id="attachment_79013" align="alignnone" width="800"] Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.[/caption]   [caption id="attachment_79012" align="alignnone" width="800"] Moja ya kikundi cha burudani kikitoa burudani katika maadhimisho hayo.[/caption]   [caption id="attachment_79025" align="aligncenter" width="763"] Moja ya kikundi cha burudani kikitoa burudani katika maadhimisho hayo.[/caption]   [caption id="attachment_79027" align="alignnone" width="800"] Afisa Habari na Utafiti kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Gasirigwa Sengiyumva, akizungumza kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza juzi.[/caption]   [caption id="attachment_79031" align="alignnone" width="800"] Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.[/caption]   [caption id="attachment_79033" align="alignnone" width="800"] Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.[/caption]   [caption id="attachment_79035" align="alignnone" width="791"] Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga akiwasilisha ujumbe kutoka TEF Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017.[/caption]

UNTOLDY STORY KUCHEZWA MEI 18 MAKUMBUSHO YA TAIFA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MSANII wa Sanaa za Maonyesho Amani Kipimo  anataraji kufanya onesho la  Igizo la Jukwaani linalokwenda kwa jina la Untoldy Story litakalo fanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi  blogu muandaji wa enesho  hilo Amani Kipimo amesema kuwa enesho ambalo litakuwa la bure  hivyo anawaomba kila mtu aliyopo nje na ndani ya Dar es Salaam  kufika katika ukumbi wa makumbusho Mei 18  mwaka huu.

Kipimo  amesema kuwa eneo hilo alina kiingilio  hivyo kuwaomba watu kufika kwa wingi kujionea namna ya wataalamu na manguli wa sanaa za jukwani watakavyokuwa wanatoa burudani na ujumbe kwa jamii

Thursday, May 4, 2017

MAVUNDE-VIJANA WACHANGAMKIE FURSA ZA MAFUNZO KWA VITENDO

WANAFUNZI JIJI LA ARUSHA WAPEWA ELIMU YA MADINIWanafunzi wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka  Taasisi ya  Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth  Bokaba (hayupo pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kuhusu elimu ya madini ya vito yanayopatikana chini, wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.
Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Eric Mpesa akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakati wa mafunzo ya Jemolojia yaliyotolewa na Taasisi ya GIA wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yanayoendelea jijini Arusha.
Mkufunzi kutoka Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA), Elizabeth  Bokaba, akiwafundisha elimu ya Jemolojia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakiangalia madini ya Tanzanite katika Banda la Kampuni Gliters Gems Limited  wakati walipotembelea mabanda ya maonesho baada ya kupata mafunzo ya Jemolojia.
Mfanyabiashara wa Madini wa Kampuni ya Abdulhakim Mulla akiwaonesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madini ya Tanzanite. Mulla alitumia nafasi hiyo kuwafundisha tofauti ya madini yaliyonakishiwa na ambayo bado hayajakatwa.

Na Asteria Muhozya, Arusha
 Jumla ya Wanafunzi 55 kutoka  Shule za Sekondari za Arusha Day, Arusha Sekondari na Wining Sprit wenye  umri kati ya miaka 12- 15 wamepatiwa mafunzo ya Jemolojia katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.
Mafunzo hayo yanayojulikana kama GemKids yametolewa na  Wakufunzi kutoka  Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA) na kuratibiwa na Kituo cha Jimolojia  Tanzania  Cha Arusha, (TGC).
Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, Mratibu wa TGC,  Erick Mpesa amesema kuwa, mafunzo hayo  ya Jemolojia, yanalenga kuwapa ufahamu wanafunzi ili kuwa na uelewa wa madini ya vito, kujua matumizi yake, kuyatumia na baadaye kuwawezesha  kuingia katika biashara ya madini huku wakiwa na uelewa mzuri na rasilimali hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia mahusiano ya TGC na Taasisi ya GIA, Mpesa amesema kuwa, TGC imelenga kuendeleza ushirikiano na Taasisi hiyo kwa siku za baadaye hususani katika masuala ya utafiti na mafunzo na kuongeza kuwa, uhusiano uliopo baina ya taasisi hizo, umewezesha baadhi ya watumishi wa kituo hicho kupata mafunzo katika taasisi hiyo.
Kuhusu mpango wa TGC kutoa mafunzo  kwa Watanzania, alisema kuwa, tayari kupitia Maonesho ya Vito ya Arusha, kituo hicho kuanzia mwaka 2014 kimetoa mafunzo ya ukataji na unga'rishaji wa madini ya vito kwa  jumla wanawake 47 na kueleza kuwa,  hivi sasa jumla ya wanawake 18 wanaendelea na mafunzo hayo na wanatarajiwa kuhitimu ifikapo tarehe 19 ya mwezi huu.
"Kutokana na changamoto ya ajira wahitimu wetu tunawashauri kujiunga katika vikundi ili kuwawezesha kupata ruzuku pale zinapotolewa na Serikali. Hii inawezesha rasilimali inayotumika kuwafundisha kuwawezesha vijana hawa isipotee bure. Lengo letu ni kuwawezesha waweze kujiajiri na kuajiriwa," alisisitiza Mpesa.
Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yalianza  rasmi tarehe 3 Mei na yanataajiwa kufungwa tarehe 5 Mei,2017. 

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA


Frank Mvungi-Maelezo
Serikali  ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa kuimarisha na kuendeleza miundo mbinu ya Afya,uboreshaji huduma kupitia teknolojia  na Usambazaji wa madawa  hadi kwenye vituo vya kutolea huduma.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar  es Salaam na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anna Makinda wakati akifungua Kongomano  la kwanza la bima ya afya na kinga ya jamii .
“’Lazima tuangalie na kuwatambua wale ambao hawawezi kulipia huduma za afya na tuangalie namna gani tutahakikisha wanapata huduma na isitokee wakati wowote wengine wakpoteza maisha kwa kukosa fedha za kujiunga na Bima ya Afya.’’ Alisisitiza Makinda.
Akifafanua Makinda amesema kuwa kuna umuhimu wa kuangalia namna huduma zinavyotolewa katika vituo vya kutolea huduma,upataikanaji wa vifaa tiba na dawa,hali inayochochea upatikanaji wa huduma bora kwakuwa ndiyo dhamira ya Serikali kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kuhusu Afya bora kwa wote Makinda alibainisha kuwa azma hiyo itafikiwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya na na mpango wa CHF iliyoboreshwa katika Halmashauri 50 hapa nchini.
Akizungumzia mkakati wa kutoa huduma bora Makinda amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umejipanga kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na watoa huduma zinaendana na dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma bora za afya .
Aliongeza kuwa watoa huduma watakao toa lugha zisizofaa kwa wagonjwa,kuwanyanyapaa, kuonyesha tabia ya ukatili watafungiwa kutoa huduma kama kituo hicho kimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kwa Upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini Dkt.Baghayo Saqware  amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Sera ya Taifa ya Bima itakayowezesha wananchi huduma bora za Afya.
“Sera ya Taifa ya Bima tasaidiakuondoa tatizo la watoa huduma za Bima wasio waaminifu “ alisisitiza Dkt.Saqware.
Tanzania kama nchi imekuwa na historia ndefu ya kutoa huduma bora za matibabu kupitia bima ya Afya, Kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Bima Binafsi zikiwa ni juhudi za kuboresha huduma hizo hapa nchini.
Kongamano la Bima ya Afya na Kinga limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) na shirika la Pharm Access International.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akiwasili katika ukumbi wa Ledger Hotel Jijini Dar es Salaam kufungua Kongamano la Kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii .
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akizungumza wakati wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii  lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Pharm Access Dkt. Heri Marwa akizungumzia uhuhimu wa Sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za Afya hasa kwa wananchi wasio na uwezo.
 Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa kongamano hilo kuhusu umuhimu wa kuwa na Sera ya Bima hapa nchini ili kuwalinda wananchi .
 Mkurugenzi wa  kuendeleza miradi, Pharm  Access, Ewout  Irrgng akizungumza wakati wa akizungumza wakati wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii  lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akifurahia jambo na Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia Afya toka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Anna Nswilla kabla ya ufunguzi wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
 Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Slvery Mgonza akiwasilisha mada katika kongamano la kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii, lililofanyika Kunduchi katika hoteli ya Ledger plaza Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.​​​​ 

WABUNGE WA CHADEMA WACHIWA HURU PAMOJA NA WAFUASI WAO

 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge watatu wa Ukawa na Makada wao baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu. Wabunge hao na wenzao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kiridhika kwamba ushahidi ulioletwa mahakamani hapo haukuwa unatosha kuwakuta washtakiwa na kesi ya kujibu.


Amesema kuwa katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka  umeshindwa kuthibisha kwani, hata  mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani alimjeruhi. Ameongeza kuwa, ushahidi wake ulielezea tu Jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.

Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema kitendo hicho kingeweza kupelekea mlalamikaji kufungua kesi nyingine lakini siyo kujeruhi.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka uliita mashahidi watatu kutoa ushahidi ambapo hakuna ushahidi ulioweza kuwatia hatiani watuhumiwa hao na kukutwa na kesi ya kujibu.

Wabunge walioachiwa huru ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema , mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma na Diwani wa Kata ya Saranga Kimara, Ephreim Kinyafu.

Ilidaiwa kuwa Februari 27, 2016 katika Ukumbi wa Karimjee wilaya ya Ilala jiji la Dar es Salaam walifanya kosa la kumjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha.

Mmbando katika ushahidi wake alieleza jinsi alivyovamiwa, kujeruhiwa na kupokonywa faili lililokuwa na ajenda na muongozo wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam uliopaswa kufanyika  Februari 27, 2016.

Alidai kuwa siku hiyo ya Februari 27, 2016 alipewa jukumu la kuusimamia uchaguzi huo wa Meya na Naibu Meya ambao ulipaswa kufanyika nyakati za saa 4 asubuhi katika ukumbi wa Karimjee.

Kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam alikuwa ni Mwenyekiti wa uchaguzi huo, wajumbe wote walifika, Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Salehe Yohana ambaye alikuwa Katibu alifungua uchaguzi huo kwa sababu koramu ya wajumbe ilikuwa inajitosheleza.

Baada ya kikao kufunguliwa na Katibu huyo Salehe alisema uchaguzi huo hautaweza kufanyika kwa sababu amepokea zuio la mahakama la kuzuia uchaguzi huo kuendelea na akawaalifu wajumbe.

Baada ya uchaguzi huo kuahirishwa, wajumbe wa CCM walitoka nje lakini wajumbe wa vyama vingine wakiwamo Ukawa walimvamia wakisema aendeshe uchaguzi huo.

“Walinifuata mezani nilipokuwa nimekaa wakitaka niendelee na uchaguzi huo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alilivuta faili lililokuwa na muongozo wa uchaguzi huo na katika tukio hilo niliweza kuwafahamu walionivamia kwa wengine kwa majina, wengine kwa sura.”Alisisitiza kusema Mmbando wakati akitoa ushahidi wake.

Aliongeza kuwa kuna mwanamke mmoja alimkoa konzi kichwani na wengine wakimgonga gonga huku na kule

Aliieleza mahakama watu wengine aliowatambua siku hiyo ya tukio kuwa ni Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akimwambia kuwa yeye ni Kibaraka wa CCM, hawawezi kuendesha serikali kama mali yao, akae aendeshe huo uchaguzi.

Mbunge wa jimbo la Ukonga, Mwita Waitara yeye alikuwa akimsisitiza kuwa hakuna kuondoka hapa kaa uendeshe kikao.

Akiendelea kutoa ushahidi mahakamani hapo, Mmbando alidai kuwa Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema (56) yeye siku hiyo ya tukio alimuona akiwatuliza wenzake ‘muacheni tuweke utaratibu mzuri tutafanya tu kikao’.

Mheshimiwa Hakimu, walinikamata kwa nguvu nisitoke , wengine walinishika maziwa hadi sketi yangu iling’oka zipu na kwamba baada ya tukio hilo aliokolewa na askari wa jeshi la polisi na wafanyakazi wa jiji  kupitia mlango wa nyuma  na hakujua kilichoendelea nyuma yake.

“Katika tukio hili nilipata madhara, utu wangu nilidhalilika na mwili wangu ulivia damu”. Alimaliza kutoa ushahidi wake Mmbando.
Wabunge wa Chadema, na makada wao pamoja na Wakili Wao Peter Kibatala wakifurahi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kiachiwa huru kwa kuonekana hawana kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma iliyokuwa inawakabili ya kumjeruhi Katibu Tarafa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando

Profesa Lipumba Asema Ilikuwa ni MZIGO Mkubwa sana Kumnadi Lowassa

Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na msajili wa Vyama vya Siasa Prof. Ibrahim Lipumba leo May 4, 2017 kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV amesema hakuwa na namba ya Edward Lowassa wakati anajiunga UKAWA.

Aidha, kwenye mahojiano hayo Prof. Lipumba amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaiongoza CUF katika kudai haki za wananchi tofauti na Maalim Seif ambaye mara kadhaa ikitokea suala hilo haonekani akisema:

“Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi Mkuu tuliingia kwenye maandamano Zanzibar, lakini Maalim Seif alikwenda Uingereza nilikuwa mstari wa mbele.

Prof. Lipumba amesema pia kuwa Maalim Seif amekuwa akidai kila anapokosana na mtu kisiasa kuwa mtu huyo anatumiwa na CCM akitolea mfano wa Ahmad Rashid, akisema:

“Ni kawaida ya Maalim Seif, akikosana na mtu kisiasa anasema anatumiwa na CCM. Rejea mgogoro na Ahmad Rashid".

Akizungumzia kuhusu kumpokea na kumtambulisha kwa viongozi wa UKAWA aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa wakati anatoka CCM, Prof. Lipumba alisema:

“Mbatia ndiye aliyeniunganisha na Lowassa. Sikuwa na namba zake, na wakati anakuja, nilisema wazi suala la rushwa ni mfumo siyo mtu.

“Mzigo mzito anapewa Mnyamwezi, lakini huu wa kumnadi Edward Lowassa ulinizidi uzito, nisingeweza kuubeba."

Wakai huo huo Prof. Lipumba amebainisha kuwa hakuwa na nia ya kurejea katika nafasi yake ya Uenyekiti wa CUF baada ya kujiuzulu, lakini aliombwa na wanachama wa chama hicho.

“Sikuwa na nia ya kurudi kuwa Mwenyekiti CUF ila wanachama waliniomba nirudi baada ya uchaguzi kumalizika na hali kutulia”

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AWAPA SHAVU WAKANDARASI WA NDANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi. Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.

Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo. Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.

“Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”

Kuhusu madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha Wakandarasi.

Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.

Waziri Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.

Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.

Nae, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.
 
Msajili huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.

Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Consolata Ngimbwa akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakandarasi Wanawake mara baada ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA SABA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 4, 2017. Mwenyekiti wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge  akiongoza kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Naibu Waziri  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  akiwasilisha randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Naibu Waziri  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia wakifatilia hoja mbalimbali  katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
  Wabunge wa CCM wakijadili  jambo katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Waziri wa Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.Peter Msigwa  katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
 Mbunge wa Konde,Khatib Said Haji(CUF) akiuliza swali katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO UCHINA

Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maharufu kama China International Beauty Expo African Hall,Rex Chan akizungumza na Waanddishi w...