Thursday, May 11, 2017

LG YAZINDUA BIDHAA YA MPYA YA KIYOYOZI INAYOTUMIA UMEME MDOGO NA RAFIKI KWA MAZINGIRA


KAMPUNI ya vifaa vya Umeme ya Life Good (LG) imezindua  viyoyozi  ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa gharama za kuweza kumuda kwa kila mtanzania.
Akizungumza na katika  hafla ya uzinduzi wa viyoyozi  hivyo , Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma amesema vifaa vya LG vina ubora katika matumizi ya nishati ya umeme.
Amesema kuwa  kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ni muhimu  kutumia vifaa vya umeme ambavyo ni rafiki wa mazingira bila kufanya hivyo  itakuwa tunaharibu mazingira kwa vizazi vijavyo.
Amesema kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hakuna mtu anayeweza kukwepa katika kutumia vifaa ambavyo vinakuwa ni rafiki wa mazingira.
Nae Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung,  amesema kuwa wamefanya utafiti na kuona kuna mahitaji ya viyoyozi ambavyo vitakuwa ni rafiki wa mazingira na kutaka  watu watumie bidhaa hiyo.
Amesema viyoyozi hivyo vinatumia nishati ndogo hali ambayo inafanya kila mtu kuweza kumudu matumizi ya viyoyozi pamoja na kulinda mazingira .

Aidha amesema kuwa watu wanatakiwa kutumia vifaa ambavyo vinakuwa rafiki wa mazingira ambapo LG wameweza kuzalisha bidhaa kutokana na mahitaji ya sasa yaliyopo.

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara Ushauri wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Mhandisi Mtapuli Juma akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa viyoyozi iliyofanyika leo  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa viyoyozi vya LG iliyofanyika leo  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji  akizungumza wakati wa  uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG 
Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana  akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira .
 Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu  iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania , Ramachandran  Veeraman
 Watumbuizaji wa bendi ya Borabora wakiwa wanatoa burudani jukwaani
 Afrika Mashariki Bendi ya muziki ya Borabora ikitoa burudani kwa watu waliofika katika mkutano huo
sehemu ya wafanyakazi wa LG wakiwa katika picha ya pamoja

MISS TANZANIA AKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA GARI

 Ofisa wa Basata akikabidhi funguokwa Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai  kama ishara ya kumkabidhi mrembo  gari yake aina ya Suzuki Swift pembeni yake Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili.
 Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akiingia ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa
 Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai akifurahi mara baada ya kuingia ndani ya gari yake
 Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania , Arbart Makoye akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi gari
 Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili na Mumewe  wakikabidhi kadi ya gari kwa Miss Tanzania 2016/217 Diana Lukumai
 Mkurugenzi wa Grace Products Ltd Elizabeth Kilili. akizungumza na Miss Tanzania 2016/2017 Diana Lukumai katika duka la ke lililopo City Mall jijini Dar es Salaam.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Grace Product na Gift Jewelers wamekabidhi gari kwa Mrembo wa Shindano hilo Diana Edward Lukumai  ambaye alishinda taji la Miss Tanzania 2016/2017.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa zawadi hiyo Miss Diana amesema kuwa  anaishukuru sana kamati hiyo kwa kuweza kumsaidia kupata zawadi hiyo ambayo ameisubiri kwa hamu .

“Wasichana wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujiandaa kisaikolojia kwani kushinda taji la urembo la Miss Tanzania sio kitu kidogo, watu wengi watakufatilia hivyo lazima ujitambue kuwa ukiwa Miss Tanzania ni mtu ambaye anatakiwa kuwa msiri  hivyo wasichana wajiandae sana kisaikolojia katika hili.” Amesema Miss Diana.

Amesema kuwa gari hiyo itaweza kumsaidia katika matumizi yake binafsi hasa katika kipindi hiki ambacho anaendelea na kampeni yake ya Dondosha wembe ambayo ina lengo la kumkomboa  mtoto wa kike juu ya mila potofu za kuozeshwa mapema na ukeketaji.

Kwa upande wake mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albart Makoye amesema mara baada ya kukabidhi kwa zawadi hiyo kunafungua pazia la shindano jipya la mwaka 2017/2018 .


Amesema kuwa warembo wanatakiwa kujiweka sawa hili waweze kunyakuwa taji hilo ambalo mashindano yake yataanza kuanzia ngazi ya votongoji mpaka taifa.


Wednesday, May 10, 2017

PICHA KADHAA ZA WAZIRI MKUU BUNGENI LEO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 10, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Kange Lugora wa Mwibara (kushoto)  na Katani Ahmed Katani wa Tandahimba (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10,2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Salum Mwalimu kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma (katikati) na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mwanne Mchemba (kushoto) na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. 

POLISI INAWASHIKILIA WATUHUMIWA WA MENO YA TEMBO


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Watu wawili wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na nyaraza serikali za Meno ya Tembo vipande sita ambavyo vilivyokamatwa Chanika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Somon Sirro amesema kuwa  vipande hivyo vilikamatwa wakati polisi wakifanya operesheni kupata taarifa ya watu wanataka kufanyabiashara ya kuuza vipande sita vya meno ya tembo na kwenda kuwatia hatiani nje ya nyumba ya moja ya watuhumiwa hao.
Watuhumiwa hao ni Mfanyabiashara Senei Abbas (36) pamoja na  Juma Mkong’wa (33) Fundi Ujenzi Mkazi wa Gongolamboto  jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa Chuo cha St. Joseph, Lewis Mbise (23) kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Luger CZ yenye namba za usajili C 4122 ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine .
Mwanafunzi huyo alipohojiwa alivyopata silaha na kukiri kuwa aliiba kwa baba yake pamoja na fedha Tasilimu sh.800,000.
Jeshi polisi limeagiza kukamatwa kwa baba wa manafunzi kwa kukosa kutunza silaha mpaka mwanae anapata nafasi ya kwenda kuiiba.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi inawashilikilia watu watatu kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa kidato cha Sita ambao unafanyika hivi sasa.
Watuhumiwa hao ni Mwalimu  Mussa Elius , Mwalimu Innocent Mrutu pamoja na mwanafunzi wa Kidato  cha Sita, Ritha Mosha .
Kamanda Sirro amesema wanaaendelea na mahojiano kuhusiana na mtihani  wa kidato cha sita unaoendelea kufanyika.
Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa watatu ambao ni walinzi kituo cha Mafuta cha Camel Kurasini kwa kula njama za wizi wa mauta lita 36000 zenye thamani ya sh. Milioni 72.
Walinzi hao Hamis Peter (49) mkazi wa Charambe, Jumanne Hamis (35) pamoja na Huruka Ramadhan (37).
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam  leo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha vipande vya meno ya tembo vilivyokamtwa na jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha silaha waliokamata kwa mwanafunzi ambayo aliiba kwa baba yake  leo jijini Dar es Salaam.

RAIS WA ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA DJIBOUTI.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Moahammed Mahmoud mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya SMZ mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein wa kwanza kulia akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

HOFU ILIYOPITILIZA NI UGONJWA, HUATHIRI KIBOFU CHA MKOJO


https://www.womenshealth.gov/files/styles/masthead/public/images/mh_woman-crossing-legs.jpg?itok=2mDGfY9_&c=fb0bb35101799fc7b9ace6dcd4defc95Na Veronica Romwald – Dar es Salaam

KUNA mtu leo hii akiambiwa asimame, azungumze mbele ya umati wa watu, anashindwa kabisa na iwapo atajitahidi kusimama anaweza kutokwa jasho jingi au kutetemeka kabisa na hata kusahau baadhi ya maneno aliyokusudia kuyazungumza.

Lakini wapo watu ambao wanao uwezo wa kusimama na kuzungumza kwa ufasaha pasipo kuwa na shaka yoyote ile.
Kuna mtu mwingine akiona kwa mfano mdudu mdogo kama mende ameingia ndani ya chumba chake basi yupo radhi kuhama kwa muda chumba hicho na kutafuta watu wa kumsaidia kumtoa mende huyo.

Simulizi ya John

John Simon mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam anasema hawezi kabisa kusimama mbele ya umati wa watu na kuzungumza.

“Natamani mno kusimama na kuzungumza mbele za watu, lakini sijui kwanini huwa nakosa kabisa ule ujasiri, hofu kuu huwa inaniingia ndani ya moyo wangu,” anasema.

Simon anasema hata alipofanikiwa kuendelea na masomo yake ya sekondari alikuwa anachelewa kufika shuleni ili asichaguliwe kuzungumza kwenye gwaride.

“Shule niliyosoma, viranja waliweka utaratibu wa kuita wanafunzi mbele kuzungumza jambo, hasa siku ya jumatatu, basi nilikuwa nachelewa makusudi ili nisichaguliwe,” anasema.

Anasema hali hiyo anayo hadi leo na hajui kama anaweza kuondokana nayo.

“Jambo ninaloshukuru mimi sina nafasi yoyote ya uongozi kazini, nadhani wanajua nina udhaifu huu maana hawajawahi kunichagua kuzungumza, sijui lini nitaweza kupata ule ujasiri walio nao watu wengine,” anasema.
http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/07/cockroach.jpg?resize=720%2C302
Wapo watu wakimuona mende 'hutimua' mbio

Mariam

Mariam Eliud, Mkazi wa Magomeni anasema yeye akimuona mende ameingia ndani ya nyumba yake anakosa amani kabisa.

“Yaani bora nimuone nyoka simuogopi hata kidogo, nitampiga mwenyewe hadi nimuue lakini si mende, nikiona yupo ndani nakosa amani kabisa.

“Nyumba yangu ina vyumba viwili vya kulala, nipo radhi nihame chumba changu kwenda kingine, nitatafuta na mtu aje kunisaidia kumuua mende huyo kwa kutumia dawa maalumu ya kuua wadudu,” anasema.

Wazazi wanavyochangia

Msaikolojia Tiba wa Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Isack Lema anasema wengi wanakumbwa na hali hiyo ukubwani lakini msingi wake ulianzia walipokuwa utotoni.

“Wazazi wengi hawajui, ni kosa kubwa kumtamkia maneno yanayomvunja moyo mtoto au kumshusha thamani.

“Unakuta mtoto anajitahidi kuonesha kipaji chake lakini mzazi anamvunja moyo na kumwambia hawezi kufika popote, au kwa mfano mwanafunzi ananyoosha mkono darasani kujibu swali akakosea, wenzake wakamcheka.

“Mwalimu anatakiwa amsaidie mwanafunzi husika, kumjenga, ili asiogope tena wakati mwingine kujibu, amsaidie kujenga ule ujasiri, wengi wanaoshindwa hata kusimama mbele ya watu ukubwani, walichekwa au kukatishwa tama walipokuwa utotoni,” anasema.
Nini hutokea

Lema (pichani) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya Akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasema wasiwasi uliopitiliza ni tatizo la akili lakini wengi hudhani ni hali ya kawaida.

“Kila mmoja anaugua ugonjwa wa wasiwasi lakini si rahisi kuona watu wakija hospitalini kupata matibabu kwa sababu wengi hudhani ni hali ya kawaida, kwa sababu mara nyingi huwa si rahisi kusababisha athari za moja kwa moja, na utaona wengi huendelea kufanya shughuli zao za kila siku kama kawaida,” anasema.

Dk. Lema anasema kawaida magonjwa ya akili huanza na vitu ambavyo ni vya kawaida kabisa.

“Kwa mfano mtu alikuwa analala kwa saa nane inafika hatua hawezi tena kulala analala kwa saa mbili, hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya miezi mitatu tayari ni tatizo, inakuwa si hali ya kawaida tena bali ugonjwa,” anasema.

Kila mwanadamu ameumbwa na hofu

Daktari huyo anasema jinsi Mwenyezi Mungu alivyoumba mwili amemuwekea kila mtu hofu ndani yake.

“Ni hali tuliyoumbwa nayo katika mfumo wa akili, hofu ni sawa sawa na ‘alarm’ ya gari, kwa mfano  nikiigusa gari yangu vibaya ‘alarm’ itatoa mlio, kuashiria gari haikuguswa vizuri.

“Hofu katika maisha ya binadamu ni hali ambayo ipo na inatusaidia kuishi maisha yetu ya kila siku hasa tunapokabiliwa na hali za hatari,” anasema.
https://i.ytimg.com/vi/DVXtnWQ1LVw/hqdefault.jpg
Mwanamume akipambana na simba porini

Anaongeza “Kwa mfano tunajua kwamba simba ni mnyama hatari, ikitokea mtu akakutana naye porini, macho yake humsaidia kuona, hofu iliyopo ndani yake hutoa ishara na ubongo hupokea taarifa na kwamba kilichopo mbele yake ni kitu cha hatari.

Anasema kwa sababu hiyo, mwili nao ambao umeumbwa ukiwa na mfumo wa kumsaidia mtu kupambana nao huanza kujiandaa kukabiliana na hatari hiyo.

“Mwili utaachilia homoni na mhusika ataanza kukabiliana na ile hatari, kuna njia mbili ambazo muhusika ataweza kuzitumia ama kupambana na simba huyo au kukimbia, hofu ya namna hii ni ya kawaida kabisa,” anasema.

Kwa nini ni kawaida

Dk. Lema anasema kwa kuwa ni hali ya hatari na macho yamepeleka taarifa kwenye ubongo, nao utatuma taarifa kwa mwili ujiandae kupambana, ni hali ya kawaida.

“Cha kwanza mwili utahitaji muhusika avute pumzi ya kutosha ili kuweza kujiandaa, kisayansi mwili huvuta hewa ya oksijeni na kutoa nje hewa ya kabonidioksaidi,” anasema.

Anasema hewa hiyo huenda hadi kwenye mapafu na ikifika huko kuna mabadiliko ambayo hutokea katika pumzi iliyoingia ndani.
https://img.planespotters.net/photo/083000/original/5h-mwh-air-tanzania-airbus-a320-214_PlanespottersNet_083238.jpg
Kuna watu wanaogopa hata kupanda ndege

“Sasa mtu aliyekutana na simba, huanza kuvuta pumzi nyingi kwa nguvu, kwa kuwa anavuta kwa nguvu ile oksijeni inafika pale kwenye mapafu ambapo hata hivyo si kituo chake cha mwisho.

“Pumzi hiyo inatakiwa isafirishwe kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili. Kwa kuwa anavuta pumzi kwa nguvu, matokeo yake ni kwamba mapigo ya moyo huanza kuongezeka, kuwezesha pumzi yenye oksijeni ifike sehemu zote za mwili,” anasema.

Hofu inavyogeuka kuwa ugonjwa

Dk. Lema anasema hofu hugeuka kuwa ugonjwa iwapo inatokea pasipo kuwa na kisababishi chochote cha hali ya hatari.

“Yaani, inakuja katika hali ya ghafla na inakuwa nje ya uwezo wa mtu husika kuweza kuitawala hiyo hofu na katika mazingira ambayo hakuna sababu ya muhusika kupata hofu,” anasema.

Anatoa mfano “Ni sawa na alarm ya gari inapopiga wakati hakuna kitu kilichoigusa gari husika. Hii inamaanisha alarm husika ina tatizo. Hofu inapompata mtu bila kuwapo kwa kisababishi cha hatari inakuwa si hofu ya kawaida tena (tuliyoumbwa nayo) bali ugonjwa wa wasiwasi.

Aina za magonjwa ya wasiwasi

Daktari huyo anasema wapo watu ambao hupata wasiwasi wa kuhamaki kitaalamu hali hiyo huitwa Panic- disorder.

“Unakuta mtu yupo mahali ghafla anapatwa na hofu, anahamaki, anakuwa kwenye tafrani kweli kweli na hata akafikia hatua ya kukung’ang’ania wewe uliyekaribu naye. 

"Lakini ukiangalia mazingira unaona kabisa hakuna kitu ambacho kinaweza kumfanya mtu kuingiwa na hofu namna hiyo,” anasema.
http://1.bp.blogspot.com/-0HioG6bRTUM/Vfn0uCIzbwI/AAAAAAAAtX8/iMiSqW5_oWk/s1600/MMGM1143.jpg
Wapo wanaoogopa kupanda au kupita kando kando ya majengo marefu au kusafiri baharini

Anasema wengine hupata wasiwasi ambao huendana na wao kuona vitu fulani fulani kwa mfano wadudu, wanyama, mabonde na vingine vingi.

“Kwa mfano kuna mtu akipanda lifti anapatwa na wasiwasi, anahisi akiingia kwenye lifti atakosa pumzi, joto litakuwa kali na matokeo yake atapoteza uhai wake, hivyo anashindwa kabisa kupanda lifti. Au mwingine anaogopa kupanda kabisa ndege,” anasema.

Anasema mwingine akikaa juu ya ghorofa au akienda sehemu ambapo pana mwinuko mrefu huhisi hali ya kizunguzungu .

“Wapo wengine wakiona damu wanapatwa na hali ya wasiwasi, kuna kundi la tatu la wasiwasi wa kijamii, unakuta kuna watu wanahisi kukaa katika kundi la watu wengi kuna kitu kinaweza kutokea.

“Hawa ndio wale ambao wakipewa nafasi ya kuzungumza mbele za watu wanahisi huenda kuna jambo baya linaweza kutokea au watamfikiria vibaya au atatokewa na vitu vya ajabu ajabu,” anasema.

Anasema wengine hupata wasiwasi wa kila kitu kilichopo mbele yake.

“Yaani wanakuwa si watu wa kuwa na uhakika wa kila jambo wanalofanya, wanahisi lazima watakosea, kwa sababu ni mambo ambayo huanza katika hali ya kawaida ili tuseme ni tatizo lazima dalili zisiwe za siku mbili tatu,” anasema.

Anasema lazima muhusika afanyiwe uchunguzi na wataalamu na dalili hizo awe ameziona kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu.
http://a57.foxnews.com/images.foxnews.com/content/fox-news/us/2014/05/30/man-sentenced-to-life-for-shooting-that-claimed-life-seton-hall-student-from/_jcr_content/par/featured-media/media-0.img.jpg/876/493/1422712432124.jpg?ve=1&tl=1
Mara nyingi mtu hutumia mikono yake kuficha uso pindi anaposhikwa na uwoga

Dalili za ugonjwa

Anasema wakati ni hali ya kawaida kwa mtu anayekabiliana na hali ya hatari kuvuta na kutoa pumzi haraka haraka kwa mtu ambaye anapatwa na hali hiyo bila kuwa na kisababishi cha hatari hali huwa tofauti.

“Yule anayekabiliana na hatari ataona anavuta hewa katika hali ya kawaida lakini huyu ambaye hakabiliani na hatari yoyote atapata shida mno, ataanza kujiuliza kwanini mapigo yake ya moyo yamebadilika na kwenda kasi na anaanza kuhisi kifua kinakuwa kizito, hilo ni tatizo,” anabainisha.

Zimegawanyika

Daktari huyo anasema dalili za ugonjwa huo zimegawanyika katika makundi makuu matatu, ya kwanza ikiwa ni dalili ya mwili ambayo wengi huanza kuipata.

Mara nyingi muhusika huona ile pumzi anayoivuta ni ndogo, haimtoshi, kwa hiyo anaijitahidi kuivuta kwa nguvu na ndiyo maana anakuwa anahisi kama vile kifua kinabana na wakati huo huo mapigo ya moyo huanza kwenda kwa kasi,” anasema.

Anasema kwa kuwa wakati hali hiyo inatokea huwa kunakuwa na nguvu ambayo imeachiliwa ndani yake anaanza kutetemeka mwili.

“Wengine huanza kutokwa jasho jingi kiasi cha kulowanisha nguo zao, wapo wengine huhisi kabisa kama vile kuna kipepeo kinaruka ruka ndani ya tumbo,” anasema.

Huathiri kibofu.

Dk. Lema anasema mara nyingi inapotokea mtu akapatwa na ugonjwa wa wasiwasi humsababishia athari katika kibofu chake cha mkojo.

“Kibofu hulegea na ndiyo maana mtu hujihisi kwenda haja ndogo, kila anapopatwa na hali ya wasiwasi, wapo ambao huhisi kizunguzungu, wengine tumbo huunguruma na wapo ambao huishiwa kabisa nguvu mwilini na hata kupoteza fahamu kabisa,” anasema.
http://topnews.ae/images/mental-workspace-in-human-brain.jpg
Dalili za kiakili

Anasema hili ni kundi la pili la dalili, kwamba mtu huwa na hofu kuu, huhisi huenda kuna kitu kibaya ambacho kitatokea katika maisha yake.

“Unakuta anatafakari mno juu ya hayo anayodhani huenda yatamtokea matokeo yake mapigo ya moyo yanabadilika, yaanza kwenda kasi kwa hofu anayokuwa ameijenga ndani yake juu ya hayo anayohisi yatamtokea,” anasema.

Dalili za kitabia

Anasema watu wanaougua ugonjwa wa wasiwasi huanza kuepuka kukaa katika maeneo au vitu vyote ambavyo huwasababishia kukumbwa na hali hiyo.

“Kwa mfano utakuta mtu anakwepa kukaa au kusimama mbele ya kundi la watu, kupanda lifti, kupanda gari, ndege na vitu vingine vingi vinavyomsababishia hali ya wasiwasi,” anasema.

Anaongeza “Kuna tabia fulani tunaziita za kiusalama, kwamba mtu anaona ili awe salama ni vema aepuke mazingira yote yanayoweza kumsababishia kupata wasiwasi.

Si rahisi kugundua tatizo

Anasema kwa sababu suala hilo linalohusisha mwitikio au mabadiliko ya kimwili wengi hudhani wanakabiliwa na tatizo la pumu (athima).

“Wengine hudhani wanasumbuliwa na shinikizo la damu, wanakwenda hospitalini lakini wakitibiwa hawaponi kwa sababu si ‘pressure’ ya kawaida,” anasema.
http://pic.pimg.tw/mulicia/1342404351-3402839975.jpg
Kundi linaloathirika zaidi

Anasema ni vijana, ambao kawaida huwa wamefunzwa mambo mengi kipindi cha utotoni na uishi kwa kuamini katika kile walichofundishwa.

“Tatizo lina vyanzo vingi, jinsi tunavyokuwa tumelelewa, kwa mfano walizoea kukutishia tishia, unajikuta unakuwa mtu mwenye wasiwasi kila wakati tangu ukiwa mtoto.

“Lakini wakati mwingine kuna malezi ambayo yanatuweka katika mazingira ambayo ni ya kuogopa kila wakati, kwa mfano mtu anayeogopa mende ukimuuliza kwanini anamuogopa mende wengi huwa hawana majibu ya kujitosheleza,” anasema.https://www.ohsu.edu/xd/education/schools/school-of-medicine/departments/clinical-departments/surgery/residency-and-fellowships/general-surgery-programs/images/20141029_092850-small-main-hospital-entrance.jpg

Tiba

Anasema wagonjwa wa wasiwasi hupewa matibabu ya kibaiolojia ambapo hupewa dawa zinazowasaidia kurejea katika hali yao ya kawaida wanapopatwa na wasiwasi.

“Kuna tiba za kisaikolojia pia, kwa mfano mtu alipata tukio fulani likamjengea hali ya wasiwasi, tiba hizi huwa zinatusaidia kumfanya mtu arejee katika hali yake ya kawaida,” anasema.

Eckobank Tanzania leo imewahakikishia wateja wake kuendelea na shughuli zake nchini Tanzania Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict amefanya mkutano na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, na kueleza kwamba hawana dhamira ya kusitisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo makubwa waliyojiwekea ya kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

“Hii ilikuwa ni ahadi yetu tangu tulipoanza kufanya shughuli zetu hapa nchini miaka saba iliyopita na itaendelea kuwa ahadi yetu mpaka hivi sasa,” alisema Benedict.

Licha ya kukiri kwamba kumekuwapo na ongezeko la wateja kushindwa kurejesha mikopo yao mwaka jana, alisema benki hiyo imejiwekea utaratibu mzuri na hatua sahihi za jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

Alisema, “Tumechukua hatua muhimu ili kuwezesha urejeshaji wa mikopo mbalimbali ndani ya miezi mitatu iliyopita na tunaamini kwamba mfumo tuliouanzisha utatuletea mafanikio makubwa ndani ya miezi michache ijayo.”

Aliongeza kuwa, nguvu ya msingi ya benki hiyo ina ungwa mkono na wanahisa wakubwa ambao wanaifanya benki kuwa imara, madhubiti na kuaminika na hivyo kuwa moja ya chombo cha fedha kinachoweza kuendana na hali yoyote ya dhoruba.

Washirika wakubwa wa Ecobank ni pamoja na Nedbank ya Afrika Kusini( asilimia 21), Qatar Nation Bank (asilimia 20), Public Investiment Corporation ya Afrika Kusini ( asilimia 14) na International Finance Corporation iliyopo chini ya Benki ya Dunia (asilimia 14).

Benedict aliongeza kwamba Ecobank ina shauku kubwa ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendeleza uchumi kupitia huduma zake. Hata hivyo, mwaka 2016 ilishuhudia ongezeko la kutokulipwa kwa mikopo, jambo ambalo liliisukuma benki hiyo kubadilisha mbinu na kuja na mikakati mipya ya kukabiliana na hali hiyo.

Alielezea kwamba Ecobank Tanzania haina lengo la kufunga huduma zake na badala yake imeanza kufanya mabadiliko katika shughuli zake ili kuweza kukabiliana na hali ya sasa.

Pia aliongeza kwamba ili kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa ufanisi zaidi, benki hiyo imewekeza zaidi kwenye huduma zake za kimtandao na malipo ili kuweza kuwahudumia wateja wake kwa urahisi zaidi na taifa kwa ujumla.

“Hivi karibuni tulizindua app ya Ecobank Mobile Banking ambapo wateja watapata huduma ya Xpress Akaunti.

Huduma ya Xpress Akaunti inawawezesha wateja kufungua na kutumia akaunti zao bila ya kufika kwenye matawi yetu, huku wakiokoa muda, pesa na kuongeza ufanisi na usalama, hii yote ikiwa ni mikakati ya Ecobank kwa Afrika.

Malengo mazuri ya Ecobank ya baadaye ni kuwa taasisi imara iliyojikita kwenye msingi mzuri.

Kwa mara nyingine ninapenda kuwahakikishia tena wateja wetu na wadau kwamba tutaendelea kuwepo hapa.
 


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwahakikishia wateja wa benki hiyo na umma wa ujumla kuhusu dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa huduma zake hapa nchini. Kushoto Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja wa benki hiyo, Ndabu Lilian Swere.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo yao. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati.
Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa EcoBank Tanzania Raphael Onyango akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake hapa nchini kutokana na ahadi na mikakati madhubuti waliyojiwekea. Wa pili kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati (kulia).
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Ecobank Tanzania, Respige Kimati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na malengo yake. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za biashara za ndani Ndabu Lilian Swere.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na mikakati waliyojiwekea. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati na kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja.

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AFANYA ZIARA YAKE YA KWANZA BABATI-MKOANI MANYARA


Na Mary Gwera, Mahakama
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma amesifu kasi ya uondoshaji wa Mashauri katika ngazi za chini za Mahakama nchini akitaja kuwa ni Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Wilaya.
Alisema hayo mapema Mei 9 katika ukumbi ya mikutano ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara alipokuwa akiongea na Watumishi wa Mahakama Mkoani  humo,akiwa katika ziara yake ya kwanza kufanya tangu kuteuliwa kwake Januari, mwaka huu.
Mhe. Jaji Mkuu amewapongeza Mahakimu wote nchini ikiwa ni pamoja na Mahakama- Manyara kuhusiana na kasi ya kuondosha mashauri katika Mahakama za ngazi za chini licha ya idadi kuonekana kuwa kubwa.
Mhe. Jaji Prof. Juma alisema kuwa wananchi wengi bado wana Imani na Mahakama yao, hivyo idadi kubwa ya mashauri imeendelea kufunguliwa katika Mahakama zetu hususani Mahakama za Chini ambazo ni Mahakama za Mwanzo na Mahakama za Hakimu Mkazi.
“Kwa takwimu tulizo nazo Mahakama kwa mwaka jana, asilimia 71 ya mashauri yalifunguliwa katika Mahakama za Mwanzo, huku Mahakama ya Wilaya ikiwa na asilimia 14 ya kesi zilizofunguliwa kwa mwaka jana, Mahakama za Hakimu Mkazi asilimia 7, Mahakama Kuu asilimia 5 na Mahakama ya Rufani ikiwa na wastani ya asilimia 0.5,” alieleza Kaimu Jaji Mkuu.
Aliendelea kusema kuwa takwimu hizo zinaonesha dhahiri kuwa wananchi bado wana Imani kubwa na Mahakama zetu na hivyo kuwataka Mahakimu na watumishi wote wa Mahakama kwa ujumla kuongeza bidii katika kuwatumikia wananchi.
Mbali na pongezi hizo, Mhe. Kaimu Jaji Mkuu amewataka Watumishi wa Mahakama-Manyara kufanya kazi kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Mahakama ambao ndio dira ambayo itawawezesha kufikia azma ya kuwa Mahakama bora yenye kutoa huduma bora kwa wananchi.
“Wengi wenu mnafahamu kwa sasa, Mahakama ipo katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, wenye lengo la kuboresha maeneo mbalimbali Mahakamani ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya utoaji haki nchini pamoja na kurejesha imani ya wananchi kwa chombo chao,” aliwaambia watumishi hao akiwataka kila mmoja kushiriki kikamilifu katika utekelezaji huo.
Aidha, Mhe. Jaji Prof. Juma aliwataka watumishi wa Mahakama pia kujikita katika Matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha utendaji kazi huku akitilia mkazo kwa Watumishi pia kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi.
Awali akisoma hotuba yake mbele ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora alisema kuwa Mahakama katika mkoa huo zimekuwa zikifanya kazi ya uondoshaji mashauri kwa jitihada ili kuhakikisha kuwa inaondokana na mlundikano wa kesi.
“Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, kwa upande wetu, Mahakama kanda ya Manyara tumejiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kesi yoyote inayoletwa katika Mahakama ya Mwanzo/Wilaya isizidi miezi mitatu mpaka kukamilishwa kwake, na hili tunalisimamia kuhakikisha tunaondokana na mlundikano wa mashauri katika Mahakama zetu,” alisema Mhe. Kamuzora.
Ziara ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu imelenga katika kuangalia utendaji kazi wa Mahakama hizo, mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo na hatimaye kushughulikia changamoto hizo kwa ustawi wa Mahakama.
Mhe. Kaimu Jaji ametembelea Mahakama kadhaa mkoani humo ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Wilaya Babati, Mahakama ya Mwanzo/Wilaya Hanang, pia kukagua Jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na anaendelea na ziara katika Mkoa wa Arusha.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Juma akiongea na Watumishi wa Mahakama mkoani Manyara (hawapo pichani), miongoni mwa vitu alivyzungumzia ni pamoja na kuzingatia maadili katika ufanyaji kazi, utoaji wa taifa sahihi kwa manufaa ya umma, na matumizi ya TEHAMA.
 Mhe. Prof.Ibrahimu Juma akiendelea kuzungumza na Watumishi wa Mahakama-Manyara, aliyeketi kushoto ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi, kulia ni Mhe. Rumisha, Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora (aliyeketi pembeni wa kwanza) pamoja na baadhi ya Watumishi wengine wa Mahakama mkoani humo wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu pindi alipokuwa akizungumza nao.
Miongoni mwa Watumishi wa Mahakama waliohudhuria kikao hicho pamoja na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.
 Mmoja wa Watumishi akiuliza swali.
Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, akifafanua jambo.
 Kaimu Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof.Ibrahim Juma (wa tatu kushoto), Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi (wa tatu kulia), Katibu wa Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, Mhe. Eliazar Luvanda (wa pili kulia) na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Mkoa Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wa Mahakama wa mkoani Manyara.
 Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika kikao cha Watumishi na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama walioshiriki katika kikao cha Watumishi na Mhe. Kaimu Jaji Mkuu.
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu aliowahi kuwafundisha chuoni, wa kwanza kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
Mhe. Kaimu Jaji Mkuu akikagua jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi/Wilaya Manyara lililopo katika ujenzi, kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama hiyo kutasaidia kuondokana na changamoto ya uchakavu wa jengo wanayokabiliana nayo katika Mahakama ya sasa. (Picha zote na Mary Gwera wa Mahakama)

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudu...